Prof. Kabudi nachelea kukuamini kama kweli mlishinda kesi Afrika ya Kusini, tusipende kuona uongo kuwa sehemu kubwa ya siasa za Tanzania

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
8,181
Points
2,000

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
8,181 2,000
Kwanza naomba niombe radhi kwa balozi wa Canada nchini Tanzania kama kweli ulimuita na kumzungumzia yale uliyozungumza leo.

Pili siamini kama hujui kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Marekani na Canada kwani Canada yupo jumuiya ya madola wakati Marekani haipo.

Sasa basi, tuje kwenye hoja ya mkulima kufungua kesi kule Afrika ya kusini na hatimaye akakamata ile Air bus. Sijui mawakili wako wa serikali walienda kule kuzungumza nini kwani inaonekana dhahiri kuwa mkulima huyu ana hoja kwenye madai yake ya USD 33 million. Na dalili za wazi zinaonyesha kuwa mkulima huyu alishinda kesi hiyo.

Ni kwa maana hiyo basi mkulima ametumia moja ya kipengele muhimu sana kwenye mkataba wa jumuiya ya madola ambacho kinatoa uhuru wa hukumu iliyoamuliwa na mahakama moja ya nchi mwanachama kutumika kwenye nchi yoyote ile mwanachama ndani ya jumuiya ya madola. Afrika kusini ni mwanachama wa jumuiya ya madola kama walivyo Tanzania na Canada. Sasa hoja ifuatayo inanifanya nimuone Kabudi kama muongo wa kutupwa na kweli nimeendelea kumshushia heshima kama ambavyo nimefanya hivyo hapo kabla.

1. Kama serikali kweli ilishinda kesi huko Afrika kusini, mkulima huyu ametumia hukumu ipi kwenda kuzuia ndege Canada? Ikumbukwe kuwa asingeweza kuzuia ndege pasipo hukumu halali ya kimahakama, hukumu ambayo mnadai mlimshinda na akakata rufaa mkamshinda tena.

Ninaamini kuwa kwa Canada mkulima huyu anaenda kupata haki yake pasipo ubabaishaji wowote ule. Naipongeza Canada kwa kufuata kikamilifu mkataba wa jumuiya ya madola. Kupitia nchi za aina hii wengi wetu tunapona dhidi ya ukandamizaji wa mabeberu weusi ambao wanaua mamlaka zingine ili wasisumbuke.

Aidha Tundu Lissu alishatushauri kama kweli tunataka kuwa kama tunavyotaka basi tujiondoe kwenye mikataba yote ya kimataifa ikiwemo jumuiya ya madola. Otherwise tutaendelea kunyolewa. Na naamini tukijiondoa basi tutaumia zaidi.
 
jd41

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
3,373
Points
2,000

jd41

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
3,373 2,000
.... hiyo mikataba ya kimataifa itaendelea kutubana hata kama tutaacha kutengenezea ndege zetu Canada, tukihamia nchi nyingine kama nayo ili_sign hiyo mikataba bado tutaendelea kubanwa tu, issue kama tunajiamini huyo mkulima hana anachotudai, basi tumuache aendelee kubadilisha tu hizo mahakama aende kila nchi, kwani tutampiga tu!, but kama ni vinginevyo, bora kuongea nae tu, ili hizi vurugu za ndege kukamatwa mara huku mara kule ziishe.
 
Wanajifanya wajuaji wakati wao ndiyo chanzo cha makosa.
 
KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Messages
1,273
Points
2,000

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2019
1,273 2,000
umesema mwenyewe kama kesi imefunguliwa upande mmoja Wa jumuiya ya madola inaweza kusikilizwa nchi nyingine ya jumuiya hiyo kama aliyefungua kesi kakata rufaa. sasa hapo tatizo liko wapi? kwani kesi ikiamriwa na nchi moja ya jumuiya ya madola, haiwezi kufunguliwa kwa nchi nyingine tena?

Kwani afrika kusini ,serikali haikushinda kweli? kama ni haki kukata rufaa nchi nyingine yoyote mwanachama Wa jumuiya, uongo Wa Kabudi unakujaje? Hivi kwa mawazo yako Canada itampatia tu hiyo ndege?

Naamini katika uwezo Wa Kabudi na zaidi ya yote Nina imani na nia na dhumuni la Mhe.Rais ,ninaamini Tanzania tuna wanasheria wazalendo na waaminifu wenye uwezo Wa kusimamia kesi yoyote ya kizandiki, kilaghai na kizushi inayofunguliwa mahakama yoyote duniani kwa maslahi mapama ya taifa letu
 
Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Messages
8,392
Points
2,000

Consultant

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2008
8,392 2,000
Kumsummon Balozi wa Canada ni kutaka kumuonea tu. Wenzetu kule wanaheshimu mihimili yao. Kabudi anabwabwaja tu ili bosi wake aone kama hili "limemuudhi" na kwamba yupo "analifanyia kazi". I believe anajua kabisa kinachoendelea na uwaziri aliopeewa baada ya kuokotwa jalalani haujaformat ubongo wake na kudelete the little he knew about Laws.
 
G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
8,181
Points
2,000

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
8,181 2,000
hukumu haiwezi kukatiwa rufaa katika nchi nyingine hata kama rufaa take ilisikilizwa katika nchi nyingine?
Wasingeweza kufikia hukumu pasipo Tanzania kuhusishwa. Unless tuambiwe walipuuza tena. Ninachojua mkulima katumia ile hukumu ya mwanzo kukamata ndege. Kumbuka kuwa serikali walienda A. Kusini na excuse kuwa ndege ni ya Rais. Hawakwenda kupambana kwenye kubatilisha hukumu ya mwanzo.
 
Maboso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Messages
4,743
Points
2,000

Maboso

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2013
4,743 2,000
Unataka umuamini Prof Kabudi au hukumu iliyotolewa? Maana hati ya hukumu iliwekwa hapa JF na watu tuliisoma sasa unachotaka kuanza kupindisha pindisha lugha hapa ni nini?
 
Kilatha

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Messages
1,650
Points
2,000

Kilatha

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2018
1,650 2,000
Mambo kama haya ndio maana kwenye yale ya msingi baadhi ya watu wanaona Magu awe anafanya tu kuliko kujibizana na watanzania.

Watanzania 100 wakionyeshwa picha ya punda wapo wengi kati yao watakao sema kwenye hiyo picha wao wanaona farasi wala si jambo la kushangaza wachache wakaona Simba. Sasa watu kama hao wakujibizana nao si kupoteza muda tu.

Hivi S.A ata kesi ilisikilizwa si walipoenda mahakamani ikabainika hiyo nchi hawana jurisdiction ya kusikiliza kesi yenyewe na sinema ikaishia hapo hapo.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
20,569
Points
2,000

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
20,569 2,000
.... hiyo mikataba ya kimataifa itaendelea kutubana hata kama tutaacha kutengenezea ndege zetu Canada, tukihamia nchi nyingine kama nayo ili_sign hiyo mikataba bado tutaendelea kubanwa tu, issue kama tunajiamini huyo mkulima hana anachotudai, basi tumuache aendelee kubadilisha tu hizo mahakama aende kila nchi, kwani tutampiga tu!, but kama ni vinginevyo, bora kuongea nae tu, ili hizi vurugu za ndege kukamatwa mara huku mara kule ziishe.
Kuongea naye walishaongea, na ndo maana alishusha deni .... na ndo hapo kwenye technical mistake aliyoifanya mkulima... kwamba mahakama zinatimiza hukumu za nchi nyingine zilizotolewa na mahakama ya nchi husika na si makubaliano ya mdai na mdaiwa... HAPO NDO SERIKALI YETU INAPOSEMA WALISHINDA...

Dawa ya deni ni kulipa tu
 
G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
8,181
Points
2,000

G Sam

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
8,181 2,000
Kuongea naye walishaongea, na ndo maana alishusha deni .... na ndo hapo kwenye technical mistake aliyoifanya mkulima... kwamba mahakama zinatimiza hukumu za nchi nyingine zilizotolewa na mahakama ya nchi husika na si makubaliano ya mdai na mdaiwa... HAPO NDO SERIKALI YETU INAPOSEMA WALISHINDA...

Dawa ya deni ni kulipa tu
Mkulima anaenda kulipwa.
 
tindo

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
26,539
Points
2,000

tindo

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
26,539 2,000
Kumsummon Balozi wa Canada ni kutaka kumuonea tu. Wenzetu kule wanaheshimu mihimili yao. Kabudi anabwabwaja tu ili bosi wake aone kama hili "limemuudhi" na kwamba yupo "analifanyia kazi". I believe anajua kabisa kinachoendelea na uwaziri aliopeewa baada ya kuokotwa jalalani haujaformat ubongo wake na kudelete the little he knew about Laws.
Yeye Kabudi anadhani Canada nchi yao inaendeshwa kwa maagizo toka juu. Kule ni utawala wa sheria, nidhamu yake ya woga kwa wenzetu haina nafasi.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Messages
4,820
Points
2,000

Kalamu1

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2018
4,820 2,000
1. Kama serikali kweli ilishinda kesi huko Afrika kusini, mkulima huyu ametumia hukumu ipi kwenda kuzuia ndege Canada? Ikumbukwe kuwa asingeweza kuzuia ndege pasipo hukumu halali ya kimahakama, hukumu ambayo mnadai mlimshinda na akakata rufaa mkamshinda tena.
Moja wapo ya ishara kwamba kesi hatukushinda huko Afrika Kusini ni "Kuzuia ndege zisiende huko."
Ile sababu ya 'vurugu' za wakati huo ilikuwa ni gheresha tu.
 
Forum statistics

Threads 1,389,914
Members 528,056
Posts 34,038,496
Top