G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,555
- 35,880
Kwanza naomba niombe radhi kwa balozi wa Canada nchini Tanzania kama kweli ulimuita na kumzungumzia yale uliyozungumza leo.
Pili siamini kama hujui kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Marekani na Canada kwani Canada yupo jumuiya ya madola wakati Marekani haipo.
Sasa basi, tuje kwenye hoja ya mkulima kufungua kesi kule Afrika ya kusini na hatimaye akakamata ile Air bus. Sijui mawakili wako wa serikali walienda kule kuzungumza nini kwani inaonekana dhahiri kuwa mkulima huyu ana hoja kwenye madai yake ya USD 33 million. Na dalili za wazi zinaonyesha kuwa mkulima huyu alishinda kesi hiyo.
Ni kwa maana hiyo basi mkulima ametumia moja ya kipengele muhimu sana kwenye mkataba wa jumuiya ya madola ambacho kinatoa uhuru wa hukumu iliyoamuliwa na mahakama moja ya nchi mwanachama kutumika kwenye nchi yoyote ile mwanachama ndani ya jumuiya ya madola. Afrika kusini ni mwanachama wa jumuiya ya madola kama walivyo Tanzania na Canada. Sasa hoja ifuatayo inanifanya nimuone Kabudi kama muongo wa kutupwa na kweli nimeendelea kumshushia heshima kama ambavyo nimefanya hivyo hapo kabla.
1. Kama serikali kweli ilishinda kesi huko Afrika kusini, mkulima huyu ametumia hukumu ipi kwenda kuzuia ndege Canada? Ikumbukwe kuwa asingeweza kuzuia ndege pasipo hukumu halali ya kimahakama, hukumu ambayo mnadai mlimshinda na akakata rufaa mkamshinda tena.
Ninaamini kuwa kwa Canada mkulima huyu anaenda kupata haki yake pasipo ubabaishaji wowote ule. Naipongeza Canada kwa kufuata kikamilifu mkataba wa jumuiya ya madola. Kupitia nchi za aina hii wengi wetu tunapona dhidi ya ukandamizaji wa mabeberu weusi ambao wanaua mamlaka zingine ili wasisumbuke.
Aidha Tundu Lissu alishatushauri kama kweli tunataka kuwa kama tunavyotaka basi tujiondoe kwenye mikataba yote ya kimataifa ikiwemo jumuiya ya madola. Otherwise tutaendelea kunyolewa. Na naamini tukijiondoa basi tutaumia zaidi.