Kiongozi, naona unajitahidi kumtetea Prof lakini naona kama utetezi wako hauja kaa sawasawa
Mfano; Mimi nikiwa shambani hula papai moja zima (msimu wa papai) pengine lenye uzito wa 750g
Sasa kama nikiwa nyumbani kikachanganya matunda na kupata pengine uzito wa 350g nikala
ni yupi amekula sukari nyingi?
Itoshe kusema kuwa, Kuchanganya matunda hakuna madhara yoyote ILA KINACHOTAKIWA ni kula kwa kiasi - ule tunda la aina moja au mchanganyiko (yasiwe mengi sana). Wakati wa msimu, wakulima huku mashambani hula tunda la aina moja hadi kushiba kabisa kwa hiyo bora hata wangechanganya.
Nafikiri Prof sio mtaalam wa lishe ILA anaijua lishe kiasi kutokana na kuwa mbobezi wa masuala ya moyo hivyo, lishe ya prof ni respect to heart health na sio Afya ya kawaida ya mwili wa binadamu.....
Kuhusu sucrose (sukari ya jikoni, miwa nk) nafikiri ni vizuri kutumia Sucrose kuliko Glucose anayoitumia ambayo ni sukari iliyochakatwa...
Maongezi ya Prof. hayalengi watu kama wewe ambao mnafanya kazi za kutumia nguvu mashambani (au wale ambao wanashughulisha mwili mara kwa mara). Wewe hata ukila mapapai matatu kwa siku, yanabadilika tu kuwa energy na unayatumia kwenye kazi unazofanya.
Prof. ni mtaalamu wa moyo uko sahihi, na hakuna afya ya mwili bila afya ya moyo.
Sukari za aina zote kama hazitatumika kama energy zikishachakatwa kwenye umengenywaji, end product yake ni fat, ambayo itaenda kutunzwa kwenye mwili, utanenepeana, utapata fatty liver, utakuwa na high cholestrol, utajaa mafuta kwenye mishipa ya damu na matatizo mengineyo mengi.
Umesema vizuri kwenye kula kwa kiasi. Kuchanganya matunda hakuna madhara ya moja kwa moja, ila ukishachanganya most likely utakula mengi kuliko ukila moja na utakula yenye viwango tofauti tofauti vya sukari. Fructose, sukari inayotokana na matunda inachakatwa na ini, small amounts kutoka kwenye matunda hazina shida kabisa ila ukiwa na tabia ya kuzidisha bila kujua, tegemea matatizo.
Shida ya magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na ulaji wa hovyo ni slow progression conditions, inaweza kuchukua miaka 10-20 tokea umeanza kutengeneza tatizo mpaka utakapoona symptoms. Kuna sababu kwanini watu wengi Tanzania wanakufa in their 60's. Mara nyingi shida ya afya utakayoipata ukiwa na miaka 50 au 60, imetokana na ulivyoishi ukiwa na miaka 20, 30, na 40. The body keeps a count,
Again, za kuambiwa changanya na zako!
Cc:
Hassanjk
Poor Brain