Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.
Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhara ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.
Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili,
ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).
Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".
"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073