Prof Janabi awekwa mtu kati

Prof Janabi awekwa mtu kati

Sio kuchambuliwa, simple tu angesema ukweli, Sukari ya Nyumbani ni mchanganyiko wa Glucose na Fructose ,sio lazima ataje formulas

Ila kutulisha uongo kuwa ni Glucose hapo lazima ahojiwe
Sasa ndugu yangu hiyo si Biology ya form two?

Mbona mnakuza kama kitu kinachohotaji maarifa makubwa mno
 
Prof.Janabi akiambiwa uongo wake na Mkali wa Bio-Chemistry View attachment 3309840
Dr Janab ni Binadamu na muda mwingine anafanya makosa, Yes

ila inatakiwa apewe sapoti na wapatikane wakina Janab wengi

Mchango wake katika mambo ya lishe na kupunguza magonjwa yasiyoambukiza ni mkubwa

Kwa mtu ambaye ameshadeal na changamoto hizi atakubali kisukari, presha, kansa, magonjwa ya moyo, figo, stroke nk yapo juu sana

Kwa Bahati mbaya haya magonjwa kwa asilimia kubwa yanasababishwa na ulaji ovyo na sisi tumezoea kula ovyo

Shida ya wabongo hatuappreciate juhudi zake ila tunasubiri sehemu ya kukosoa tu

HAKUNA NJIA YA KUPUNGUZA/KUEPUKA MAGONJWA YA MOYO/YASIYOAMBUKIZA ISIPOKUWA LAZIMA TUANZE NA LISHE/ULAJI
 
Chatgpt
1000033181.jpg
 
Shida yako ujuaji mwingi, ukifuata ushauri anaoutoa kwa kiwango Fulani ( angalau 50%) magonjwa ya moyo huyapati
Angewaacha wataalam wa lishe watoe maelezo ya nini mtu anatakiwa kula na nini hatakiwi kula. Ndio maana kaambiwa hapo akasome biochemistry ili asichanganye watu.

Unanifahamu sana hadi kuniita mjuaji?
 
alisema kwanza KULA ni umama, mwanaume ukimaliza kunyonya maziwa ya mama yako, mwili wako hauhitaji tena msosi ni mwendo wa maji na mwanga wa jua tu kama JADUU wa koy mil gaya,....😳😳🙌😂🤣🤣🤸
😂 zee liongo sana hili,
 
Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.

Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.

Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).

Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".

"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073
Thanks
 
Back
Top Bottom