Prof Janabi awekwa mtu kati

Prof Janabi awekwa mtu kati

Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.

Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.

Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).

Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".

"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073
Hata hio ya kuchanganya Matunda Mzungu kadanganya, kuna Matunda Ukichanganya yana Madhara,

Inshort Tiktok si sehemu ya kupata taarifa sahihi, mtu ana tafuta viewers hapo apige hela na wapuuzi puuzi kama hamis77 wanaingia kichwa kichwa na kuwa chawa wa kujitegemea kumuongezea views.
 
Amesoma wapi
Japan University of osaka, moja Ya vyuo Bora zaidi Duniani (Kipo Top 100) na Queens land Australia (Nacho kipo top 100).

No way uwe na Elimu ya Kuunga unga usome hivyo vyuo, unaongelea Vyuo level za Oxford, Havard etc huko ni top cream zinasoma, jamaa kasoma ni wivu tu wa Watanzania kushindwa kuelewa hili.
 
Maongezi ya Prof. hayalengi watu kama wewe ambao mnafanya kazi za kutumia nguvu mashambani (au wale ambao wanashughulisha mwili mara kwa mara). Wewe hata ukila mapapai matatu kwa siku, yanabadilika tu kuwa energy na unayatumia kwenye kazi unazofanya.

Prof. ni mtaalamu wa moyo uko sahihi, na hakuna afya ya mwili bila afya ya moyo.
Sukari za aina zote kama hazitatumika kama energy zikishachakatwa kwenye umengenywaji, end product yake ni fat, ambayo itaenda kutunzwa kwenye mwili, utanenepeana, utapata fatty liver, utakuwa na high cholestrol, utajaa mafuta kwenye mishipa ya damu na matatizo mengineyo mengi.

Umesema vizuri kwenye kula kwa kiasi. Kuchanganya matunda hakuna madhara ya moja kwa moja, ila ukishachanganya most likely utakula mengi kuliko ukila moja na utakula yenye viwango tofauti tofauti vya sukari. Fructose, sukari inayotokana na matunda inachakatwa na ini, small amounts kutoka kwenye matunda hazina shida kabisa ila ukiwa na tabia ya kuzidisha bila kujua, tegemea matatizo.

Shida ya magonjwa yasiyoambukiza yanayotokana na ulaji wa hovyo ni slow progression conditions, inaweza kuchukua miaka 10-20 tokea umeanza kutengeneza tatizo mpaka utakapoona symptoms. Kuna sababu kwanini watu wengi Tanzania wanakufa in their 60's. Mara nyingi shida ya afya utakayoipata ukiwa na miaka 50 au 60, imetokana na ulivyoishi ukiwa na miaka 20, 30, na 40. The body keeps a count, Again, za kuambiwa changanya na zako!

Cc:
Hassanjk
Poor Brain
Mshangazi wewe ni dactar pia bila shaka...
Sasa nakuongeza kwenye list ya mashangazi wenye hadhi kubwa hapa tanzania...🙏🙏🙏🙏🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🫶🫶
 
Au tunashadadia kwa vile amesema mzungu? Ina maana Tanzania hatuna wasomi waliokuwa wanafahamu hizo hoja anazokuja nazo mzungu? Ni vipi kama Janabi alikuwa anazungumzia hakuna ulazima wa kuchanganya matunda kama kote unaweza kupata fructose, maltose na sucrose? Hatuoni kama ukiyachanganya unaweza kuzidisha kiwango kinachojitajika na mwili? Wacha nisubiri wanafunzi wa Prof. Janabi wanavyoweza kumnasua mwalimu wao katika hili!
Mkuu ukila kipande kidogo Cha embe ukala kipande kidogo Cha papai au ndizi na mwingine Akala embe Zima au ndizi nzima je nani atakuwa amezidisha hicho kiwango unachosema?

Kiuhalisia Janab kachemka ni muongo kama embe na papai Lina sukari ileile tu je kosa LI wapi nikila huku kidogo na kule kidogo Ili Hali wapo watu hula embe Zima au hata matatu Kwa mtu mmoja
 
Sio anachanganya ila ni vile anarahisisha communication...
Hv unajua kumuelekeza mtu ambaye ajasoma hayo mambo deep zaidi ni kupoteza muda ndio maana kuna mda anaongelea juu juu tu...

Kuna vitu ana skip ili kutokupoteza mda..
Mtu na uprofessa wake kusema ashindwe kujua ishu ya sugar seriously
Huna akili. Poor brain as you call yourself
 
Au tunashadadia kwa vile amesema mzungu? Ina maana Tanzania hatuna wasomi waliokuwa wanafahamu hizo hoja anazokuja nazo mzungu? Ni vipi kama Janabi alikuwa anazungumzia hakuna ulazima wa kuchanganya matunda kama kote unaweza kupata fructose, maltose na sucrose? Hatuoni kama ukiyachanganya unaweza kuzidisha kiwango kinachojitajika na mwili? Wacha nisubiri wanafunzi wa Prof. Janabi wanavyoweza kumnasua mwalimu wao katika hili!
Janabi is a fraud. Alifeli biochemistry somo ambalo ni basic science katika medicine. Janabi sio nutritionist anaingilia sehemu asioyoijua. Kimsingi Janabi hajanyooka kishuleshule. Ni vile mfumo unambeba alafu watu wanahofia kumcrash waziwazi lakini katika medicine ni takataka.
 
Siku zote nawambia mapriof. wa tz ni vilaza wakubwa hamuelewi!
Angalia hata wakupewa uongozi, wanaishia kuvurunda na kuwa machawa tu. Kama mnabishi niwataje!
 
Ningetamani sana kama Janabi angejibu uongo wake kwa maelezo kama hayo ya huyo jamaa.

Mi najiuliza kwanini wana mnadi Afrika nzima? Akishinda tunapata faida gani, kuna upigaji au kujipendelea ?

Na gharama za kumzungusha Afrika nzima zinatoka mfuko gani nchi hii? ni zake binafsi au za umaa?

CAG atueleze mwakani tulitumia Bilioni ngapi kumnadi Janabi Afrika na tumepata faida gani au hasara kiasi gani.
Tunarudisha "shukrani" kwa Dokta.
Nadhani umeelewa.
 
Mchakato unaisha lini.Mbona nilimsikia akieleza kwenye usaili.Matokeo bado?
 
Hajui bio chemistry yule mzee, anawambia watu wanywe kijiko kimoja cha ujii😂, wakati mtu mume, anatakiwa ale calories si chini ya 2700 Sasa pigia kijiko kimoja ninkama mls 20 ivi, si ni bangi hiyo

Kuna vijana wengi wa pale Muhimbili huwa wananiambia kuwa Janabi kavamia chaka la Cardiology ameanzisha uchawa kwenye taaluma ya watu lakini wanamstahi kwani yupo na mbeleko ya hao wanaozunguka naye kumnadi duniani, Janabi nakushauri kaa pembeni vijana wako Moto na wanaenda na wakati achana na enzi za akina Shaba, Mclarity, Mtulia etc...
 
Dr Janab ni Binadamu na muda mwingine anafanya makosa, Yes

ila inatakiwa apewe sapoti na wapatikane wakina Janab wengi

Mchango wake katika mambo ya lishe na kupunguza magonjwa yasiyoambukiza ni mkubwa

Kwa mtu ambaye ameshadeal na changamoto hizi atakubali kisukari, presha, kansa, magonjwa ya moyo, figo, stroke nk yapo juu sana

Kwa Bahati mbaya haya magonjwa kwa asilimia kubwa yanasababishwa na ulaji ovyo na sisi tumezoea kula ovyo

Shida ya wabongo hatuappreciate juhudi zake ila tunasubiri sehemu ya kukosoa tu

HAKUNA NJIA YA KUPUNGUZA/KUEPUKA MAGONJWA YA MOYO/YASIYOAMBUKIZA ISIPOKUWA LAZIMA TUANZE NA LISHE/ULAJI
Janabi kichwani mweupe ndio maana sasa kwasababu tunaumwa ndio tutume ujinga kutatua shida zetu?
 
Janabi kichwani mweupe ndio maana sasa kwasababu tunaumwa ndio tutume ujinga kutatua shida zetu?
Shida mnajifanya ujuaji huku sio wafuatiliaji wa mambo

Kwenye swala la ulaji wanasayansi wamekanyagana sana, pia hata waliosoma lishe kwenye swala la ulaji ni wana shida sana

Asilimia kubwa ya watu wanaofuata ushauri wao hawatoboi

Mimi nishafanya research kwenye mambo hayo, unakuta mtu wa lishe anakushangaa unavyompangia ulaji mtu wa kisukari anakuambia hajui mfumo huo.

Mfumo mnaokaririshwa vyuoni umefeli kwenye uhalisia hasa magonjwa yasiyoambukiza.
 
Watanzania tujifunze namna ya kuchakata taarifa siyo kila tunachokiona mitandaoni tunakibeba tu.
Sasa huyu mzungu ameonyesha uongo gani wa alichosema Janabi? mbona kwenye video ameenda tu expand na kutolea maelezo zaidi yale aliyoyasema Prof.

Tuzingatie kwamba Janabi alikua naongea kwenye hadhira ya watu ambayo angeanza kubreak down hizo molecules wasingemuelewa, ametumia glocose kwenye maelezo kwa sababu ni aina ya sukari inayojulikana zaidi na watanzania kuliko hizo nyingine.

Kwenye Muktadha wa nutrition, kula mchanganyiko wa matunda (fruit salad) kunasababisha kuconsume kiasi kikubwa cha sukari kwa sababu matunda yanatofautiana viwango vya aina za sukari zilivyonavyo. Kijiko kimoja kidogo cha sukari ni gramu 5, sasa fikiria ukijaza bakuli la mchanganyiko wa matunda umeweka ndizi, zabibu, embe, nanasi na machungwa, unakula gramu ngapi za sukari kwa mlo mmoja (matunda yana virutubisho na faida nyingi kwenye lishe hasa kwenye kutengeneza mlo kamili, ila ni muhimu yaliwe kwa kiasi).

Huyu mzungu anawapotosha na watu mnashupaza vichwa tu kijinga jinga, "za kuambiwa changanya na zako, sivyo utapoteana mjini hapa".

"Jedwali la kiwango cha sukari kwa kila gramu 100 ya matunda"
View attachment 3310073
Usibishane na vilaza...waache na tope zao kichwani.....
Kwanza hata huyo mzungu anaonekana amepangwa na vilaza.....
 
Back
Top Bottom