Makangarawe
Senior Member
- Nov 19, 2013
- 101
- 24
Mzee umenena siku zote ukweli umuweka mtu huru,nadhani sasa umekuwa huru kwa kuusema huu ukweli.
Babu Sikonge, kwa ubunifu wa kijasiriamali Mbowe hawashindi akina Mengi na Bakhresa! Hata wanaofanya biashara ya ukahaba wanalipa kodi lakini kwa moral standards hizo biashara hazifai.
Kuna vigezo vingine mlivyotumia kumfanya awe mwenyekiti wenu zaidi ya ushawishi wa mali yake na ukaribu alio nao na Mtei?
Binafsi uanachama wangu kwa chadema uko mashakani! Kwa jinsi ninavomjua Zito Tango UDSM, jamaa ni jembe sana ameamua kuwa mstaarabu kinoma kuacha kumwaga mboga baada ya wenzake kumwaga ugali!
So at the end nikajua hamna cha chadema wala nn, wote wale wako after maslahi! nikifikiria nilivopigwa mabomu halafu leo wanaleta ujinga.
Niko pembeni kwa ss nasoma ramani manake tunatafutia watu umaarufu na kupeleka watoto wao chooni tu! Wajinga sana
Bocho,
Unaongea ujinga na upumbaf!!!
Na hapa ndipo ule msemo wa,''Foolish mind discuss people but intelligent mind discuss issues''
Inasikitisha kuona kwamba mtu unamchukia tu kwasababu ni mpinzani wa chama kilichopo Madarakani! Huu ni uzezeta na uzuzu uliopitiliza. Kwanini watu hamtaki kuzungumzia UASI wa Zitto Kabwe,Kitila Mkumbo na Mwigamba? Yaani kwako tatizo ni Mbowe siyo hawa waliotaka kuleta maasi ndani ya chama!!!!
Kwa taarifa yako Mbowe ni moja ya Viongozi makini katika nchi hii na wasiotetereka. Hata CCM na Serikali yake wanalijua hili ukiwemo na wewe. Watu husema mti wenye matunda ndiyo hupigwa mawe na ndicho kinachotokea kwa CDM na Viongozi wake.
Kusema ati Mbowe alianzisha Klabu za Usiku ambazo hazina tija kwa wananchi ni upumbavu. Kuna Mahoteli makubwa makubwa kuzidi Bilicanas kama Moven pick,Kilimanjaro,New Africa, Bahari Beach n.k.yanaendesha Biashara hizo hizo za Ulevi mbona hamyaisemi???Iweje kwa Mbowe ni nongwa??? Mbona hampigi kelele kwa Makampuni ya yanayotengeneza Pombe kama TBL na Sigara za TCC???
CCM mnatapatapa, mmekamatwa pabaya. Hao Vibaraka wenu kina Zitto,Mkumbo, Mwigamba na wengineo wameshakwaa kisiki. Jipangeni upya lakini Intelijensia ya CHADEMA itawabaini tu!!!!!
Kikwete anamuongoza prof j4 magimbi,prof mwandosya,dr mwaki-embe,prof maji marefu nk...
Wee utakuwa PIMP pekee Tanzania unayekusanya kodi ya Changudoa. Hivi kwa mwaka unakusanya Tsh ngapi Mkuu? Je naweza kupata kazi kwako ili niwe nakusanya kodi hizo kwa Machangudoa? Kazi nzuri sana hii. Mie sikujua kama Tanzania wanalipa kodi hawa ma CD.
Mwisho wa siku, Mbowe kaongoza chama na kimekuwa maarufu, hao jamaa zako wameongoza kampuni tu. Kila mtu na uwezo wake unepofikia na wote ni Matajiri sana tu.
Mwisho ni kuwa nyie mnaojifanya hampendi huduma za a CD, kijua kikizama tu, mnapita kukusanya Midondo ya CD.
![]()
Mimi najua kwamba hili swali achilia mbali wewe hata wapiga domo wengine humu ndani hawawezi kuliibu:
Kuna vigezo vingine mlivyotumia kumfanya awe mwenyekiti wenu zaidi ya ushawishi wa mali yake na ukaribu alio nao na Mtei?
Ujumbe wangu kwenu wakati nahitimisha, CHADEMA inabidi ifanyiwe mabadiliko kutoka SACCOS/ Coy na kuwa taasisi ya umma.
Ni kweli kuwa Kusaga pia alikuwa DJ. Lakini, nani anajali leo hii?
Baregu alitakiwa kumtahadhalisha Zitto kuhusu mipango yao ya mapinduzi.
Ila kama kawaida, alikaa kimya akidhani mipango ile ingetimia.
Sasa anatapa-tapa kujaribu kumuokoa Zitto.
Zitto ameshakwisha, anachoweza kufanya Zitto ni kukimbilia mahakamani. Kesi itanguruma mpaka baada ya uchaguzi mwaka 2015.
Hataweza kugombea wadhifa wowote ule, na akishinda, sana sana atabaki kuwa mwanachama wa Chadema, bila ubunge wala cheo chochote kile.
Zitto kwisha kazi yake, akadai mafao yake CCM, atulie.
Maji na mafuta siku zote havichanganyiki! Tatizo la CHADEMA ni akili ndogo kuongoza akili kubwa.
Sasaa unategemea nini kipofu akiongoza? Leo hii professor anaongozwa na mhitimu wa elimu ya secondari eti kwa vile tu ni mfadhili wa chama!
Unafikiri mimi ni mtu anayeona Mbowe anafaa kuongoza chama? Hapana. Kuna wengine wazuri tu na ningeliona busara kama angelimpisha Dr. Slaa kwenye nafasi hiyo hasa ukichukulia Slaa siyo Mbunge.
Ila kwa wakati tuliopo sasa kuelekea 2015, kubadili uongozi litakuwa kosa kubwa sana. Mie ni mmoja wa wale wanaoona kuwa uchaguzi wa viongozi ufanyike mwaka 2015 December. Ila Zitto kwa sasa, narudia tena, kwa sasa na yeye hafai kabisa kuwa Mwenyekiti kwani kashakosana na watu wengi ndani ya Chadema na Zitto ana ubinafsi sana wa kujijali yeye zaidi kuliko Chama. Mwenyekiti gani huyu atakuwa? Pambo au mwenyekiti wa kujiongoza yeye na M7?
Acha propaganda na uongo.Huwezi kuwanusuru wahaini kwa njia hiiVIONGOZI WA CHADEMA FANYENI HARAKA .
NIMEPITA MOROGORO,IRINGA NA MBEYA,HALI HII YA MVURUGANO IMEKATISHA WATU TAMAA VIBAYA SANA WATU WANACHOMA BENDERA NA KUSAMBAZA VIPEPERUSHI KILA MTAA
ACHENI MPANGO WA KUMSHUGHULIKIA ZITTO KABWE, NAOMBA SANA TANGAZO HILI LIMEBANDIKWA MOROGORO STEND.
TUMSIKILIZE MZEE WETU HUYU
Baregu aitahadharisha Chadema kuhusu Zitto
Friday, 29 November 2013 · Posted in Siasa
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili. Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama, Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.
Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho, alisema na kuongeza: Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.
Lwakatare - Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare alisema chama hicho kipo imara na hakiwezi kuyumba kwa sababu ya uamuzi huo.
Lwakatale ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho alisema: Mfumo wa ulinzi ndani ya chama upo imara, yakitolewa maelezo na ngazi za juu kinachofuata baada ya hapo ni utekelezaji.
Alisema kilichotokea ni kitu cha kawaida na ni mwanzo wa chama kujiimarisha.
Temeke wapinga - Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu na Baraza Kuu la Chadema hicho Wilaya ya Temeke wamepinga hatua iliyochukuliwa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa viongozi hao.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Temeke, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, Joseph Patrick aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mgogoro huo haulengi kujenga chama, bali unakibomoa.
Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia uchaguzi wa ndani. Hii inasababisha kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti na wengine kuwaita wenzao wanatumika kwa lengo la kuwadhoofisha mbele ya wanachama, alisema na kuongheza: Tumeona mifano mingi ya namna hii. Wakati Chacha Wangwe akiwa hai alipotangaza kuwania uenyekiti, mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa majina yote na hakuwahi kusemwa vizuri kwenye chama, hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama, bali viongozi wenzake waliotofautiana kimsimamo.
Alisema hali hiyo ilijitokeza pia kwa Zitto alipotangaza kuwania uenyekiti kama ilivyokuwa wakati wa chaguzi za viti maalumu na mabaraza ya chama.
Alisema ni vyema viongozi wakaitisha mkutano mkuu wa dharura na kuwaeleza wanachama mambo mbalimbali ikiwamo ni kwa nini wameamua kusambaza waraka ambao alisema unakidhalilisha chama badala ya waliouandika.
Katibu Chadema ahojiwa - Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Herry Kilewo amehojiwa na Polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na madai ya Zitto kutishiwa kuuawa.
Katika mahojiano hayo, Kilewo aliongozwa na Mwanasheria wake, Mussa Mfinanga, Mwanasheria wa Chadema John Malya na pia alikuwapo Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob. Mfinanga alisema Novemba 11 mwaka huu, chombo kimoja cha habari kiliripoti kuwa Zitto ametishiwa kuuawa na mteja wake Kilewo.
Mfinanga alisema baada ya madai hayo, Jeshi hilo lilimwita Zitto kutoa maelezo yake na kisha kuona haja ya kumhoji Kilewo shutuma hizo. Alisema mteja wake amejidhanini mwenyewe na yupo nje kwa dhamana bila ya masharti yeyote.
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alikiri kuhojiwa kwa Kilewo akisema ni kawaida kwa jeshi hilo kumuita mtu na kumhoji kwa mujibu wa taratibu na sheria zake.
Habari na Imeandikwa na Fidelis Butahe, Beatrice Moses,
Pamela Chilongola na Editha Majura.
Chanzo - Mwananchi
Tatizo la viongozi wa CHADEMA ni kuwa hawana elimu lakini pia hawana sifa ya kuwa viongozi