:lying:Bocho! Hujasoma historia vizuri lii ujue akili ya kuzaliwa kwa mama ndio namba one ikifuatiliwa na elimu dunia na hiyo ya darasani inakuperfect tu. Ndio maana kuna wasomi wenye madigree na wengine maprofessor lakini ukiwapa waongoze watu kumi ni shughuli kubwa. Watu wengi waliofikisha dunia hapa ilipo hawakuanzia darasani au walipata kisomo kidogo tu kama huyo wa form four unayemsema. Mifano ni mingi mno na nina hakika unaifahamu mingine lakini moja mzuri ni Bill Gates.Watu walobarikiwa kugenerate ideas ndio watu muhimu sana hapa duniani. Kuna wasomi wengi ambao ni wa vyeti tu na hakuna lolote wamejifanyia au kufanyia nchi yao. Huyo unayemsema Mbowe ni mtu mwenye uwezo wa kugenerate ideas hata kama ana udhaifu wake. Ukweli kwamaba aliweza kibuni Club Billicanas kwa kuona ombwe la sehemu za starehe za vijana hauwezi kupingika. Leo hii maelfu ya watu wa Dar wamepata burdani yo kupitia Billicanas na hii ni juhudi ya huyo unayemuita ana akili ndogo. Si hivyo tu ila akili hiyo ndogo ndiyo iliyofanya Chadema ikakubalika nchi nzima na kupata wabunge kutoka 11 hadi 48 achilia mbali madiwani, na wenyeviti lukuki. Bila shaka ni wakati sasa ujilinganishe wewe na yeye na ujiulize maswali kama kweli akili ndogo hiyo imelala kiasi hicho. La msingi ni kwamba kama kiongozi huyo ana mapungufu basi awekwe sawa na mambo yaendelee.