Prof. Baregu aitahadharisha CHADEMA kuhusu Zitto

Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.

“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.

Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.

Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.

“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”

Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.

Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.

“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:

“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”

Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.

“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”

Source Mwananchi
Pamoja na madudu yote yaliyofanywa na Chadema dhidi ya Zitto, ila pia lazima nikiri kuwa, angalau Chadema bado kuna baadhi ya viongozi wenye busara!.

Pasco
 
Zitto anajaribu kuonesha kuwa anajua,zitto anaaminisha kuwa yeye anasubira,
Nitoe wito kuwa magazeti, vyombo vya habari na wanasiasa wanaochipukia sasa,wajue kuwa Mungu amesema "Pando asilolipanda baba litang'olewa"
Zitto 30 hivi alikuwa na nafasi ya kuongoza nchi,alikuwa na ndoto nyingi tu kuliko Mbowe.

Kinachomsumbua ni kujiona yeye bora kuliko kundi kubwa,Mvumilivu hula mbivu,

Biblia inasema" uwe mpole,mwerevu huku ukiwatanguliza wenzako," Zitto hili linamsumbua na kama anadhani kuwa Chadema kinaminya Demokrasia,namsihi aende Ccm

Siku moja wana jf mtajua kuwa,ccm ni mbaya kuliko chadema,Chadema wamemvumilia kukiweka chama katika tawi jembamba,ipo kudra na njia chadema,Mungu wa zitto na vibaraka wake ndio Mungu wa chadema,ipo siku rangi halisi tutaijua tu asisingizie Escrow
 
Maji na mafuta siku zote havichanganyiki! Tatizo la CHADEMA ni akili ndogo kuongoza akili kubwa.

Sasaa unategemea nini kipofu akiongoza? Leo hii professor anaongozwa na mhitimu wa elimu ya secondari eti kwa vile tu ni mfadhili wa chama!

Hili ni tatizo kwa siasa za Tanzania sio chadema tu.

Naomba isieleweke kuwa watu wasio na elimu hawezi kuongoza, au wenye elimu tu ndio wanaweza kuongoza. Kuna wenye elimu ambao ni viongozi wabovu na wasio na elimu wenye kipaji cha kuongoza.

Mpaka leo Tanzania tunashindwa kuweka uwiano kati ya haya mawili.
 
Hili ni tatizo kwa siasa za Tanzania sio chadema tu.

Naomba isieleweke kuwa watu wasio na elimu hawezi kuongoza, au wenye elimu tu ndio wanaweza kuongoza. Kuna wenye elimu ambao ni viongozi wabovu na wasio na elimu wenye kipaji cha kuongoza.

Mpaka leo Tanzania tunashindwa kuweka uwiano kati ya haya mawili.

Mkuu hii issue. Niliuliza jana kwenye thread flan,inawezekana vipi Mbowe form 6 tena div 0 awaongoze akina Tundu lisu,professor safari,Halima mdee,Albert Msando,pro Beregu na wengine ati tu kwa sababu chama cha baba mkwe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom