wale waliosoma sheria watatusaidia. Tafsiri ya sheria lazima uichukulie na ifit kwenye socio economic, cultural and political developments katika jamii. Kama kifungu kinaonekana kutoendana na moja wapo wa hayo aidha kwa kutoprogress au kuslow basi watekelezaji watatumia njia nyingine ya kuitafsiri kifungu hicho ambayo tunaiita mischivious yaani intention ya watunzi badala ya literal interpretetion. Kazi hii ni ngumu. Wanaotasfiri sheria kuangalia intention tunawaita bold spirit minded na waliobaki narrow spirit minded au waafidhina. Mabold swali linalowajia kwenye kutafsiri sheria ni what is the end result, wakati manarrow wanasema liwale na liwe regardless the impacts. Bush alikuwa na mind ya liwalo na liwe ila kidogo obama yuko kwenye group la mabold, on issues za taliban, syria na iran.
Ndio corner hiyo ya political development na mambo mengine baregu hamumuelewi.
Siasa ni zaidi ya maandishi ya Sheria kwenye makaratasi,inatakiwa usome kasi ya mchezo ya watu wako,pia sio 1+1 ni 2,na haina adui wa kudumu,Zuma alikuwa na kashfa nyingi leo Rais.Dr. Mwakyembe na Nape walitaka walianzisha Chama ndani ya Chama ilibidi wafukuzwe lkn busara zikaangaliwa,wakaangalia mabaya yao yanaweza kufuta mazuri yao yote,leo hii mmoja anakamua katika Chama na Dr. anawakimbiza Miundombinu na wanakamua vizuri.Siasa Sayansi.
SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.
Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao."
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.
Alisisitiza, "kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi."
Akaongeza, "Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti."
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.
Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
"Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?" alihoji.
Aliongeza, "Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu."
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa "kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe."
Katika kujibu hilo, Shida anasema, "Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.
"Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM."
Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
"Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.
"Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama," alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.
Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.
Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
MIDA EIGHT, yaani hapo umejidhihirisha kuwa wewe ni -------- wa hali ya juu. yaani huamini kuwa PROF BAREGU anaweza kuongea hayo? au kwa upande wako aliyoongea Baregu hayana maana?
BILA shaka baada ya press conference pale serena imeprove wazi kuwa mh ZITO HANA CHA KUJIBU mbele ya kamati kuu
1. waraka ambao kimsingi umeandikwa samson mwigamba ni vipi zito ahusishwe
2 waraka umehaririwa na dk kitila ni vipi zito ahusishwe
3 wote mwigammba na dk kitila wamekiri MH ZITO KUTOJUA CHOCHOTE KUHUSU HUO WARAKA KWAN NDIO WALIKUA KWENYE PROCESS YA KUMTAFUTA ILI KUMSHAWISHI hivo zito atahukumiwaje kwa makosa ya watu wengine
my take
akiguswa zito kwa hili la waraka wa siri basi moyo wa chadema utakua umeguswa na fikiri hatari ya moyo unaposimama kufanya kazi yake
BILA shaka baada ya press conference pale serena imeprove wazi kuwa mh ZITO HANA CHA KUJIBU mbele ya kamati kuu
1. waraka ambao kimsingi umeandikwa samson mwigamba ni vipi zito ahusishwe
2 waraka umehaririwa na dk kitila ni vipi zito ahusishwe
3 wote mwigammba na dk kitila wamekiri MH ZITO KUTOJUA CHOCHOTE KUHUSU HUO WARAKA KWAN NDIO WALIKUA KWENYE PROCESS YA KUMTAFUTA ILI KUMSHAWISHI hivo zito atahukumiwaje kwa makosa ya watu wengine
my take
akiguswa zito kwa hili la waraka wa siri basi moyo wa chadema utakua umeguswa na fikiri hatari ya moyo unaposimama kufanya kazi yake
wale waliosoma sheria watatusaidia. Tafsiri ya sheria lazima uichukulie na ifit kwenye socio economic, cultural and political developments katika jamii. Kama kifungu kinaonekana kutoendana na moja wapo wa hayo aidha kwa kutoprogress au kuslow basi watekelezaji watatumia njia nyingine ya kuitafsiri kifungu hicho ambayo tunaiita mischivious yaani intention ya watunzi badala ya literal interpretetion. Kazi hii ni ngumu. Wanaotasfiri sheria kuangalia intention tunawaita bold spirit minded na waliobaki narrow spirit minded au waafidhina. Mabold swali linalowajia kwenye kutafsiri sheria ni what is the end result, wakati manarrow wanasema liwale na liwe regardless the impacts. Bush alikuwa na mind ya liwalo na liwe ila kidogo obama yuko kwenye group la mabold, on issues za taliban, syria na iran.
Ndio corner hiyo ya political development na mambo mengine baregu hamumuelewi.
Bush was damna right ni watu wenye fikra mixed km baregu na waliokuwa wakiadhibiwa kwa ugaidi wao ndio walikuwa walikuwa waki mdemonise.Well nani hajui kuwa Baregu ana play politically correct...sasa si asem km hatakai kipengele cha mtu kufukuzwa,kwani akaishataka zitto asifukuzwe nani tena atakaa afukuzwe,bila kurudi na kusema mbona Zitto hakufukuzwa.Sasa si itakuwa mwanzo wa sheria kutofuatiliwa
Siasa ni zaidi ya maandishi ya Sheria kwenye makaratasi,inatakiwa usome kasi ya mchezo ya watu wako,pia sio 1+1 ni 2,na haina adui wa kudumu,Zuma alikuwa na kashfa nyingi leo Rais.Dr. Mwakyembe na Nape walitaka walianzisha Chama ndani ya Chama ilibidi wafukuzwe lkn busara zikaangaliwa,wakaangalia mabaya yao yanaweza kufuta mazuri yao yote,leo hii mmoja anakamua katika Chama na Dr. anawakimbiza Miundombinu na wanakamua vizuri.Siasa Sayansi.
Ndio maana leo CCM hawawezi fukuza mtu kwani walishasilence sheria kwa wengi kiasi kila muovu ktk CCM ana ushahidi wa mwana CCM mwingine ambaye alifanya kosa km hilo ila kubwa zaidi ha hakufanywa kitu.Sheria haina cha busara.Busara hutumika pale mkosaji km nae alijitahidi kutofiti ktk sheria fulani kabisa na hivyo kurudi ktk hukumu inayoweza tatauliwa kwa busara.Zitto alishajisahau na kusema anakwenda zipangua tuu hoja za watu.Na hii ni wazi kuwa alifanya intentionally na hivyo kustahili adhabu fully.
NIlimpenda sana Bush....alikutana na changamotoa mbazo leo obama angechemsha....YULE JAMAA AMBAYE ALIFANY AMAUJI NA ALIPASWA HUKUMIWA KIFO,ILA KIPINDI AKIWA KTK GEREZA MCHAKATO UKIENDELEA JAMAA AKABADILIKA SANA NA KUANZA FANYA MAMBO MAKUBWA SANA YA KUBADILI WAOVU WENGIN TUU KURUDI KTK MSTARI,PAMOJA NA KUBADILI WATU KTK MAGEREZA.Hukumu yake ikalenga ktk makosa ambayo wengi walipata hukumu stahiq kwa mujibu wa hiyo sheria.
Watu wa haki za binadamu na wengine ambao wanaitwa Politically correct, useful .i.d.i.o.t.s ambao bado wanaamini kuwa tunatakiwa kaa na kuwabembeleza magaidi.Wakaanza piga kelele kuwa bush asiweke sahihi,wakaja na theory kibao km hizi.Bush akasema no..km kweli kakosa na sheria inasema hivi then hakuna ujanja...hata km na yeye anasikitika kwa hilo na kwa jamaa ,ila ukweli ni kwamba sheria za nchi hazipaswi chagua mtu.
Bregu atuambie: HIVI HUYO KIJANA WAKE NA MTU MWINGINE YOYOTE ANGEGUSA WIRE WA UMEME WA VOLTS ZA KUTOSHA KM ANGESAMEHEWA.IMAGINE HUO UMEME ULIKUWA UNAINGIA KTK OFFICE ZA CDM JE NAO UNGEMSAMEHE KIJANA WA MZEE KWA VILE ALIIFANYIA CDM MENGI NA WENGINE KUADHIBIWA KWA VILE WALIIFANYIA CDM MADOGO?what a logic?
Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.
Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama, Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.
Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.
Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.
Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.
Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.
Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.
Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho, alisema na kuongeza:
Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.
Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.
Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.
Maadam anakubali kuwa Zitto ana makosa, ni bora akiachie chombo (CHAMA) husika kimpe adhabu stahiki. Ni kazi ya Zitto kupima na kuona kama kweli amepewa adhabu stahiki au la na baadae achukue hatua za ziada iwapo kutakuwa na haja hiyo.
Hata hivyo inatakiwa ikumbukwe kuwa; ni wazo kinzanifu kwa mtu huyo huyo ajenge nyumba vizuri na kwenye hatua za mwisho katika ujenz,i kwa makosa yaliyokusudiwa ajaribu kuibomoa.
mwananchi wako kazini badala ya zitto ndiyo maana kila kukicha ni kampeni .wanatafuta huruma ya cc muda huu .mbona wakati akiwatumia kmwandika na kuwalipa huwa hawampatii ushauri juu ya madhaa kwa chama na taifa ? Walicheza na watu wenye nia sasa wamesha ona kwamba ukiharibu kila kitu chako kizuri kinapotea na mabaya pekee yanaonwa .zitto kaanza muda mrefu sna kusaliti chama hakuanza juzi .baregu ulimweleza zitto ? Mwananchi mliandika ?
profo baregu: Sisi wanachama wa kawaida tulianza kuona mabadiliko kwa huyu kijana tangu mwaka 2008.wewe ulianza kuyaona lini?au hujayaona kabisa?miaka 5 anakiharibu chama mnamnyamazia tu.kuna watu wametoa mchango mkubwa sana chadema.wengine wamekifia.ni kitendo cha kushangaza sana kusikia wasomi kama dr mkumbo na zitto wanataka kukiua chama.hawaogopi laana za watanzania????wao watakimbilia ccm.mamilioni ya wanachadema watakimbilia wapi?hawa watu wamesoma nini?tafakari.WANACHADEMA TUWE MAKINI NA WACHUMIA TUMBO WALIOJAZANA CHADEMA.NAWAOMBENI SANA JAMANI.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.