Prof. Baregu aitahadharisha CHADEMA kuhusu Zitto

Prof. Baregu aitahadharisha CHADEMA kuhusu Zitto

Ndani ya Katiba ya Chadema toleo la 2006. Katika Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama. Sura ya 10, Ibara ya ix, imeandikwa: "Kiongozi asijihusishe au kushiriki na vikundi vya kuchonganisha au kuzua migogoro ndani ya Uongozi wa Chama au Wanachama wake."

Na katika Katiba hiyo hiyo Sura ya 7 kuhusu kazi za Kamati Kuu, Ibara ya 7, Ibara ndogo t, imeandikwa: "Kufanya uamuzi juu ya mapendekezo ya kufukuza Mwanachama." Na Ibara ndogo v, imeandikwa: "Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume na Katiba, Kanuni na Maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake."

kwani kuna aliyehitaji vifungu hivyo?
 
Mwananchi ni kipeperushi kama vipeperushi vingine halinatofauti na Kiu, ijumaaa au hata uhuru haliaminiki tena machoni pa wenye akili

Ila Tanzania Daima, gazeti la udaku ndo unaliamini?
 
wafuasi wa CHADEMA mitandaoni, je mmempuuza Dr Slaa?
 
baregu kawa wazi kama wasipomsikiliza chabama kitakuwa vipande vipande chama hiki kimeshakuwa cha misiba na matukio hakina sera tena za kimaeneleo.
 
Prof Baregu anafaa kuwa kiongozi, lkn kwa ukabila na ukanda wa Chadema hatopata.

Hongera prof kwa kuwa na mawazo huru na si kuwa kibaraka wa Mbowe.

Baregu ni kiongozi wa CHADEMA ni mjumbe wa kamatu kuu.

Au kwako wewe kiongozi ni mwenyekiti tu.

Akili nyingine kama kondoo jike.
 
Mwananchi ni kipeperushi kama vipeperushi vingine halinatofauti na Kiu, ijumaaa au hata uhuru haliaminiki tena machoni pa wenye akili

Akili yako imezoea kusoma gazeti la udaku la tanzania daima huwezi kujua uzuri wa gazeti la mwananchi.
 
Baregu alitakiwa kumtahadhalisha Zitto kuhusu mipango yao ya mapinduzi.
Ila kama kawaida, alikaa kimya akidhani mipango ile ingetimia.
Sasa anatapa-tapa kujaribu kumuokoa Zitto.
Zitto ameshakwisha, anachoweza kufanya Zitto ni kukimbilia mahakamani. Kesi itanguruma mpaka baada ya uchaguzi mwaka 2015.
Hataweza kugombea wadhifa wowote ule, na akishinda, sana sana atabaki kuwa mwanachama wa Chadema, bila ubunge wala cheo chochote kile.
Zitto kwisha kazi yake, akadai mafao yake CCM, atulie.

si bure naamini umerogwa kama huu ndo uchambuzi wako,plz rudi shule kk
 
Dar es Salaam. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu amewataka viongozi wa chama hicho kutafakari na kudhibiti madhara yanayoweza kukikumba hasa baada ya hatua yake ya hivi karibuni ya kumvua nyadhifa zote, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na wenzake wawili.

“Bahati nzuri wamevuliwa uongozi siyo uanachama, binafsi nadhani viongozi wanatakiwa kutafakari na kudhibiti madhara zaidi kwa chama, wakishupaza shingo, lolote litakalotokea watakuwa ni sehemu ya lawama,” Profesa Baregu alisema Dar es Salaam jana.

Zitto, aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walivuliwa uongozi Novemba 22 mwaka huu, kwa tuhuma za kuandaa waraka wa Mkakati wa Mabadiliko 2013, uliolenga kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho kinyume na katiba, sheria na itifaki za chama.

Profesa Baregu alisema pamoja na viongozi hao kuvuliwa madaraka, mema waliyokifanyia chama hicho hayawezi kuyeyuka na kwamba makosa yao yasikuzwe kiasi cha kufuta mazuri yao katika kujenga chama hicho.

“Ni vigumu kuamini kwamba makosa ya Zitto, Dk Kitila na Samson Mwigamba yanaweza kuyeyusha mema waliyokifanyia chama kama barafu inavyoyeyuka juani.”

Profesa Baregu ambaye alikuwapo katika kikao kilichowavua uongozi Zitto na wenzake alisema kinachotakiwa kufanyika sasa ni kujenga uhusiano ndani ya chama na hasa kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ambao umeanza Novemba 22 na unatarajiwa kumalizika Juni mwakani.

Alitaka hatua dhidi yao zizingatie Katiba ya chama hicho ili kuhakikisha kuwa hazivurugwi na mamlaka nyingine zilizopo ndani ya Chadema akisema mkutano wa Baraza Kuu unaweza kubadili uamuzi wa Kamati Kuu.

“Kinachotakiwa kufanywa ni kuwatangazia wanachama misingi, taratibu na kanuni za kuzingatia katika harakati zao ili kuondoa hali ya watu kufanya mambo kwa kificho,” alisema na kuongeza:

“Ni wazi wengi wapo katika kampeni, ichukuliwe kuwa walioshughulikiwa wamebambwa na iwe njia ya kuonyesha ukomavu katika kustahamiliana.”

Alisema asingependa kuona siasa za kulipizana visasi na kusisitiza kwamba hata kama mwanachama ana chuki binafsi na mwenzake, hatakiwi kutumia chuki hiyo kumhukumu.

“Tuhuma zinazotolewa dhidi ya Zitto na wenzake kwamba wamenunuliwa na chama fulani cha siasa zinahitaji maelezo na vielelezo vya kina ili kuwaaminisha wengi. Nasema hivi kwa sababu historia yao inadhihirisha kuwa wana uchungu na chama chao. Chama kinachoongozwa kwa demokrasia na kinachotarajiwa kushika madaraka ya kuongoza nchi, lazima kionyeshe uwezo mkubwa wa kuvumiliana, kutafakari, kusamehe, kuaminiana na kujenga umoja wenye lengo la kuelekea kusudio lake.”

Source Mwananchi

Hivi hayo ndiyo yaliyotamkwa na profesa au ni magazeti yamemnukuu vibaya?

Siamini kama kuna msomi anayeweza kukiuka itifaki,kanuni na maadili na kuanza kutoa matamshi au ushauri kupitia vyombo vya habari badala ya vikao ambavyo yeye ni mjumbe

Ndiyo maana Chuoni nilikua na-walk out mara nyingi kutoka kwenye mihadhara kuliko kukaa na kuwasikikiza maprofesa niliokosa nao imani intellectually!
 
Walichokifanya CHADEMA wamenikumbusha mwalimu wangu wa history Tunduru Secondary School(TSS). Mama yule alikuwa anatoa adhabu then anakaribisha utetezi baada ya kuwa umefanya adhabu. Ila yeye alikuwa na busara kidogo anakupa kwanza makosa yako bila kusikiliza upande wako anakuadhibu,cdm wanakuadhibu then makosa yako wanakupa baada ya adhabu. Tehetehetehetehe! Akili kubwa imetawaliwa na akili ndogo kutoa maamuzi. Ninamkubali Lissu lakini kwa hili ameburuzwa

Njaa kitu kibaya sana hata ukiwa Msomi,humuoni sikuhizi anazidi kuwa mfupi ananenepa tu,kampuni yake ndio inayo kula Ruzuku ya CDM ktk kesi zisizoisha Mahakamani,na dada yake damu kapewa Ubunge viti maalum.Wako wengi mungine Mnyika anatoka Mashavu tu kama pusii.Njaa mbaya,Wasomi wazima wanaramba viatu.
 
msibabaike sana,chadema sio chama ni saccoss hayo ndo yalikua malengo ya mzee mtei muasisi!!
 
Hivi hayo ndiyo yaliyotamkwa na profesa au ni magazeti yamemnukuu vibaya?

Siamini kama kuna msomi anayeweza kukiuka itifaki,kanuni na maadili na kuanza kutoa matamshi au ushauri kupitia vyombo vya habari badala ya vikao ambavyo yeye ni mjumbe

Ndiyo maana Chuoni nilikua na-walk out mara nyingi kutoka kwenye mihadhara kuliko kukaa na kuwasikikiza maprofesa niliokosa nao imani intellectually!

ulikua una dodge na kwenda kuchukua vifaa vyako vya upelelezi,sumu na report kisha unampelekea slaa na mbowe report!!
 
Mwananchi ni kipeperushi kama vipeperushi vingine halinatofauti na Kiu, ijumaaa au hata uhuru haliaminiki tena machoni pa wenye akili

tanzania daima ni kipeperushi kama vipeperushi vingine, halitofautiani na kiu, ijumaa, uwazi au hata sani
 
Baregu anatakiwa kuheshimu maamuzi halali ya Kamati Kuu ambayo yeye ni mjumbe na alikuwepo ziku ya kikao.

Hata kama alikuwa na mawazo mazuri na alishauri Zitto asivuliwe vyeo vyake aache demokrasia ya wengi ichukue mkondo wake, huo ndio ustaarabu vinginevyo na yeye atakuwa msomi bogus.
 
Hivi hayo ndiyo yaliyotamkwa na profesa au ni magazeti yamemnukuu vibaya?

Siamini kama kuna msomi anayeweza kukiuka itifaki,kanuni na maadili na kuanza kutoa matamshi au ushauri kupitia vyombo vya habari badala ya vikao ambavyo yeye ni mjumbe

Ndiyo maana Chuoni nilikua na-walk out mara nyingi kutoka kwenye mihadhara kuliko kukaa na kuwasikikiza maprofesa niliokosa nao imani intellectually!

man, mida eight.....think outside the box!!!
u seem to be local and primitive.. can u dare limit peoples mind kwa huu ukibaraka wako?
 
Hivi hayo ndiyo yaliyotamkwa na profesa au ni magazeti yamemnukuu vibaya?

Siamini kama kuna msomi anayeweza kukiuka itifaki,kanuni na maadili na kuanza kutoa matamshi au ushauri kupitia vyombo vya habari badala ya vikao ambavyo yeye ni mjumbe

Ndiyo maana Chuoni nilikua na-walk out mara nyingi kutoka kwenye mihadhara kuliko kukaa na kuwasikikiza maprofesa niliokosa nao imani intellectually!

kumbe!!! ndio mana umemaliza miaka lakini hujaelimika, ulivyoenda ndivyo ulivyoondoka
 
Mwananchi wako kazini badala ya Zitto ndiyo maana kila kukicha ni kampeni .Wanatafuta huruma ya CC muda huu .Mbona wakati akiwatumia kumwandika na kuwalipa huwa hawampatii ushauri juu ya madhaa kwa Chama na Taifa ? Walicheza na watu wenye nia sasa wamesha ona kwamba ukiharibu kila kitu chako kizuri kinapotea na mabaya pekee yanaonwa .Zitto kaanza muda mrefu sna kusaliti Chama hakuanza juzi .Baregu ulimweleza Zitto ? Mwananchi mliandika ?

Hili li-nchi bora mambo yaharibike tuanze upya mijitu tunaiamini lakini inakuwa misariti DCM tutapambana mpaka mwisho so long as sisi ndio wapiga kura wa nchi hii, hao wakina baregu, mkumbo sijui nani kwa maana ya Drs na Profs wachumia tumbo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom