Mkuu Mkandara, ulaya ni ulaya na bongo ni bongo!. Ingawa sisi Tanzania tumeridhi mfumo wetu wa sheria toka comon law ambako Canada, India, na nchi zote zilizotawaliwa na Muingereza ndio zinatumia, the right to privacy iko well defined!. Kama mahakamani hairuhusiwi kuingiza camera kuwapiga picha/video watuhumiwa, kila siku tunashuhudia tena sio tuu picha/video za mahakamani, pali polisi wana wa parade watuhumiwa mbele ya waandishi wa habari!, ndio itakuwa majina ya matokeo?!.
Kwani ulaya unaona majina ya waliiomba kazi?. Nimewahi kuomba kazi ofisi fulani ya ulaya, wanakuuliza, if you don't mind your current employer akijua, hapa ukiomba kazi, ukiwa short listed tuu, jina gazetini, akipita interview, jina gazetini, kazi inatangazwa sio tuu na ngazi ya mshahara, mpaka figures!.
Kama jina linatangazwa publically kwenye gazeti siku unachaguliwa, why not matokeo yasitangazwe siku yanatoka?.
Nikiwa UDSM niliwahi kupata Disco 2nd year, hata kabla majibu hayabandikwa, darasa zima walishajua kina nani wamedisco, kupitia hizo hizo number, majirani zako alphetically wanajua nikitoka mimi nani anafuatia, hivyo within no time darasa zima linajua nimedisco, kubandikwa kwa matokeo ndio salama yangu kwa vile watu wataoana` nimediscoje!.
Kilichotokea kwa huyu binti wa mkuu ni kimoja tuu, kwa vile hizo Fedha schools hazikubali kuadmit vilaza, ili kumaitain positions zao kwenye top schools, inaonekana binti alipata addmission kwa jina la baba, na Fedha huwa hawanaga Div iv, that means huyu binti ni kilaza mpaka basi, hapo ndio walimu/wazazi wametumia all efforts they could possibly can na hapo ndipo ame endup, matokeo hayo ni plus kwa JK, kwanza kusomesha watoto wake nchini, pili kuonyesha watoto wa rais ni watu wa kawaida tuu nothing special kuhusu wao. Na tatu imeonyesha NECTA ni watu wa ukweli, kama wamekutana na jina kubwa, limebunda, lina bunda tuu bila kujali ni mtoto wa nani.
Nikiwa UK kwenye kijikozi fulani, tukafanya study tour Oxford na Cambridge, pale Cambridge, aliyetutembeza ni kibibi cha over 60!, kikatuambia zamani the royals walikuwa lazima wasome hapo, akashusha sauti kama kunong'ona, "they are always not bright,"but they have to pass, apart from lectures, walipatiwa special tutorials lazima wapasi wasiaibishe familia!. Kwa matokeo ya binti yao, JK na mama Salma wamejionyesha wako miongoni mwetu, kwa sababu wangeweza kumpepea hadi kumbembesha, lakini wamemuacha apate anachoweza!. Its a big plus to them!.