Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Press conference: Lowassa apelekewa ujumbe mzito

Nafasi za wakuu wa mikoa wapya ni lini?
Jamaa anarusha kete
kila la heri ccm kwenye usingizi wa milele
 
Maelezo marefu halafu yanamhusu mtu unayesema apuuzwe! Mbona wewe hujampuuza name uachane nae na uhangaike na ambaye asipuuzwe?
 
Lowasa alihusika na ufisadi ujenzi wa jengo la ukumbi wa mikutano AICC?! Haya si yalijengwa Lowasa akiwa labda primary school? CCM msiruhusu wajinga kama huyu hoza kuvuruga watu. Lowasa atuhumiwe kwa haki si uzandiki kama huu.

Iacc imejengwa kwenye 1975 lowassa alikuwa bado anasoma
 
Mimi nimesoma hadi paragragh ya tatu nikaishiwa appetite. Kwa maana nyingine nikawa nikawa naishiwa hamu ya kuendelea kwa sbb ya kutoelewa jamaa anasema nini sijui!!
 
Lowasa alitemwa na Mwalimu kwa tuhuma za ufisadi, wakati huo Rais ana akili timamu na anasikia. Ili awe hapo alipo sasa akasaidiwa na Lowasa aliyetemwa na mwalinu Nyerere. Akalazimisha amweke kwenye nafasi nyeti ya uongozi, wananchi wakamtema kwa sababu zile zile za ufisadi alizotemwa na Hayati Mwl Nyerere.

Sasa jamani tuwe wa kweli, Lowasa ni mchafu kwa nafasi ya uongozi hata kama anabidii katika kazi.

Sifa kuu za kiongozi yeyote wa Kisiasa, jamii, ambazo ni lazima awe nazo zote alipewa Musa, akiongoza wana wa Israeli ( Kutoka 18:19-22) kama ifuatavyo:
1. Mwenye uwezo - Lowasa hana huo uwezo kwa tabia yake ya kukurupuka kufanya vitu au kutamka.

2. Mwenye kumcha Mungu - Lowasa kwa waganga/,wachawi tumeona yupo; msikitini yupo, kanisani yupo nk haeleweki anamwabudu shetani au nani?

3. Mtu mkweli - Lowasa siyo mkweli, hajawahi kuweka hadharani hata sehemu ya mali zake. Jamii yake ni Zitto Kabwe, watu wenye mioyo iliyojaa hadaa na sura za ukarimu.

4. Mtu mwenye kuchukia mapato ya udhalimu- sifa hiyo Lowasa ni ZERO hakuna mtanzania asiyemfahamu kwa kashifa zinazomwandama.

Kumtetea Lowasa kunahitaji mtu ambaye amefunika macho yake kwa magamba ya kobe.

Pili, ukiangalia hao wanaoitwa wachungaji wanao mchawishi hauwakuti kwenye association hata za wachungaji wa pentekoste. Hawajulikani. Ukiangalia picha zao utaona wengine hata kora shingoni haziwatoshi. Najiuliza hivi walipima hizo kora kabla ya kuzivaa? Inaonekana wameshona mashati ya kichungaji na kuokota watu mtaani kisha kuwapachika kora.

Huo usanii umepitiliza. Na kama Lowasa anafikiri anaweza kumhadaa Mungu kwa kutengeneza watumishi feki wa Mungu ili awaaminishe watanzania kwamba anaungwa mkono anajipalia makaa ya moto juu ya nyumba yake.
Nimemaliza.
 
umetumwa na nani we bwana shindwa pepo "God of mercy guide us"
 
Kweli CCM inajua kutunza kumbukumbu za wafu, Bado baada ya miaka 5 watatengeneza na ya Muongo aliyeshinda kama Mwanasiasa bora wakati hajawahi kufanya siasa wala hajawahi kugombea hata ubalozi wa nyumba kumi. wakati Lowasa anafanya mabaya haya yote walikuwa wapi kushindwa kumthibiti, hii ndio inaoonyesha ya kuwa ukoo wa panya hauwezi kubadilika bila kuuondoa kwa kutumia UKAWA chini ya Dr. W. Slaa.
 
hivi kumbe ndani ya ccm kuna wapuuzi mapapa kwa kiwango hiki? ni kwa nini amewaita waandishi wa habari badala ya kupeleka ushahidi wake TAKUKURU? hivi waandishi wa habari wamepata wapi muda na uvumilivu wa kusikiliza huo uharo? hivi hapo watasema wamepata hata pointi moja ya kuweka kwenye magazeti yao kesho?

hivi huyo kaoza ndiye msemaji mkuu wa chama? ndio tunajua kwamba chama chetu kimechoka lakini kiwango cha uchovu kimezidi na kama huamini kesho soma gazeti la uhuru.

kwa nchi yetu ilivyo, sitashangaa kuona press release kwamba huyu jamaa kateuliwa kuwa naibu mkuu wa wilaya ya kinondoni, nafasi mpya itakayoundwa mahususi kwa ajili yake kama ulivyokuwa unaibu waziri mkuu wa mrema. eh, kazi kweli kweli.
 
Wananchi na CCM yooote wanampenda EL.. isipokuwa watu kama 5 wana ngazi za juu CCM ndio hawamtaki...ndio wana weweseka sana, wanahangaika hadi wame HOZA....na kuoza kabisa...hawauziki...watu hao wakiongozwa na Membe, Nape, Mangula ...wote wanamchafua EL...kwa njia zote ili Membe awe mgombea kupitia CCM....bahati mbaya..Membe hauziki hata kidogo...
Nape mnamjua...has lost reputation long ago...Mangula hajifunzi makosa...alimfanyia JK hivi hivi leo anavyomfanyia Lowassa...JK alivyoingia madarakani alitupa kijijini hadi akawa anatembea na viraka makalioni....Mangula alikuwa anatunzwa na Mwalimu wa kike, baadae baada ya JK kushauriwa na Mkapa, akamrudisha..akamuoa huyu Mwalimu...Mangula alishakwisha...hata nguo alikuwa anavaa viraka...ila hajifunzi..sasa hv anatumika tena...

Lowassa ni tishio sanaaa..yuko mbele sana..ndio maana wanahaha kila kona...na wapinzani wake BILA KUJUA NJIA WANAZOTUMIA NDIO WANAZIDI MJENGA SANA EL...sbb chuki zao zinaonekana dhahiri sana..na wananchi wa leo wanajua ukweli..wanatafakari mambo..
EL ndio chaguo la wengi...je na sisi huku anatulipa..!!? Kila kitu wanamsema Ufisadi...!!! Hakuna hata mmoja atakwambia kaiba nn...au EL ana kesi mahakamani...au PCCB imemkamata kwa Rushwa...hakuna...au Polisi wana kesi nae ya wizi hakuna...!!! wamebaki fisadii fisadiii..ukiuliza wa nn..!? hakuna jibu...!!!

EL ndio chaguo letu...tushaamua...!!
 
C mwanachana wa chama chochote mm ila huyu zito alifutwa uanachama chadema baada ya kuwa na makosa yaliyoridhiwa na chama na kufukuzwa SASA lowasa anayo mengi kwa nn msimfukuze kulingana na katiba ya chama?,mtoeni kwenye chama ndo atakuwa ameisha mbaki nyinyi waadilifu..
 
Kwa sbb huyo sio MSEMAJI WA CCM, kamtuhumu Lowassa...sasa ni muda mwafaka AFUNGULIWE KESI.., athibitishe yoote....na mawakili wa EL mteja wenu huyoooo....kamateni nyama hiyo...

Na atafungwa vibaya huyu...!!!
 
Huku tuendako, ngoja nimshawishi mwenyekiti wa mtaa kwa wajomba zangu kule kazirantemwa aje Dar aite waandishi wa habari atoe tamko.
 
Hizi zote njaa! Mtu anatafuta ujira kwa siasa na maneno ya kuokoteza.
Na bado mtachafuana tu!
 
Back
Top Bottom