PPF yamfukuza kinara wa kuomba rushwa

PPF yamfukuza kinara wa kuomba rushwa

Status
Not open for further replies.
nssf ubungo wandungu ndo inatisha.
kwanza hapo mapokezi hawana kauli nzuri na wala hawajali wateja wao.

Yes, wale akina mama wawili wa mapokezi (sehemu ya ku-renew kadi/masjala) ni watata sana. Wana kauli mbovu sijapata kuona, sijui kama NSSF wanalijua hilo. Ila lazima kiwawakie watupwe Nkansi, waliniboa sana
 
Nilimweleza yule dada kwamba jasho langu litakumaliza maana maana ya mafao ni kwamba hata ukiwa kijana unayachukua inamaanisha ushazeeka! Sasa msichana anakulaje mafao ya mtu mzee hivi hivi bila uoga jamani? Si alijitakia lazi huyu?
 
Alinaswa vipi? Alitegeshewa na takukuru au alitaka kulamba mpunga wa mtu mfu?
 
ndaga baba, nitaelekea hapo kesho asubuhi na mapema!

Ndagha fijo malafyale! Linga siliko lepo wise umbulege nanune! Linga sikayapo bho tukufwa ni njala popapo!
 
Tupieni picha wakuu tumjue hata kwa sura huyo mla rushwa ya mafao ya watu.
 
NSSF yupo jamaa mmoja pale ubungo ni balaa ila nasikia amehamishiwa Shinyanga!!Nae alikuwa anaendekeza njaa sana kwa jasho la watu!!

Kote huko ni kulundana! Ni dalili kwamba kuna mtandao wa kula na badhi ya wakubwa...
 
Kuna quote moja hapo juu ilisema alitaka alambe Mil 28!
Asante, alitaka alambaje? Ina maana kuna mtu alikuwa na mafao mengi ndo akadai apewe 28M? Au kuna mtu kafariki so yeye ndo akajifanya mrithi? Up date me kama hutojali
 
PPF hawakuwa makini kufanya background checks..huyu alifukuzwa NMB morogoro mwaka 2002 kwa kuiba boom la wanafunzi wa SUA..namjua mwanzo kati mwisho ....kwa kifupi ni jangili la kutupwa
 
Tupieni picha wakuu tumjue hata kwa sura huyo mla rushwa ya mafao ya watu.

Mkuu, picha yenyewe hii hapa.

attachment.php
 
Attachments

  • Gisella.jpg
    Gisella.jpg
    117.9 KB · Views: 135
Mafao yameanza mkuu, we peleka maombi tu wata process
 
Kila anayemdhulumu mtoto, mjane na mzee haki yake atalipwa kwa ubya wake hapa hapa duniani. Bi Gisela ulifanya kitu kibaya sana na malipo yako utayapata hapa hapa.
 
Yule mama alikua mroho kweli...Nakumbuka jamaa yangu ambaye nae alikua akifuatilia mafao alisema yule danda angelikua mzuri halafu apende hela kihivyo angemumwambia wakutane Magomeni amtere kwanza halafu ammegee mafao....Lakini muonekano wa yule dada ulimtisha.....Nadhani waliobaki watakuwa na nidhamu. Kwa vile muda wa mafao yangu umekaribia tena, nitakuja nicheck kama kuna kimbelembele aliebaki..

Zamani nilikuwa najidanganya kwamba wanaume ndio waroho wa mambo yanayo fanana na haya kumbe hata baadhi ya akina mama nao wamo. Yupo hakimu moja mwanamama aliikalia kwa muda mrefu cheki iliyopelekwa mahakamani kwa ajili ya kuwagawia warithi wake. Alikuwa akitoa visingizio/makosa mbalimbali yasiyokuwa na kichwa wala miguu vilivyoashiria kwamba anataka kitu. Msimamizi wa mirathi alimtolea uvivu mbele ya mahakimu/makarani wake, nanukuu"Wewe mama sikiliza hii hela imetolewa na mwajiri wa marehemu na kuletwa hapo mahakama kwa ajili ya kuwagawia wahusika kwa mujibu ya makubaliano yao. Sasa wewe unavyonizungusha hivi ukitegemea nikupe chochote sahau kabisa , maana hata mimi sipati kitu chochote hapa . Kama unataka fedha za mirathi nenda kamuuue mumeo upate hela za mirathi". Ilikuwa siku ya ijumaa, jumanne ilyofuata hakimu akagawanya hela.
 
Huyo jamaa ni shujaa! Siku hizi hata wanawake wamo kwenye hili dimbwi mkuu! Si ndo maana wanataka usawa?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom