Wamesahau kwamba huyo Gisella ni sehemu ya mtandao mrefu wa wizi. Kwa kufanya hivyo haitakuwa mwisho. suala hapa ni kuukata mtandao mzima kuanzia chini kwenda juu. Ni sawa sawa na Rais wa nchi anayesema atapambana na mafisadi wakati yeye ni zao ama "product" ya mtandao wa mafisadi na yupo kwa ajili ya kuwatetea na kuwalinda.....Kwa hiyo suala hapo ni kusafisha tuu. Sio longo longo la kutuchezea cheusi chekundu wavuja jasho wa nchi hii..
PPF ni wezi kuanzia Mkrugenzi Mkuu bwana William Erio na wakurugenzi wake wote.
1. Erio ni bilionea kupitia 10% za kwenye miradi, ndio maana akina Gisella nao wameamua kukamua wanako weza. Miradi mibovu ya Bunge na UDOM ni juhudi za kifisadi za Erio
2. Erio ni mwizi wa fedha za umma, alilazimisha kulipwa milioni 540 eti mafao ya mwisho wa mkataba wakati bado anaendelea na kazi. Wadogo nao wamejifunzia kwake na kuanza kuwakamua wastaafu maana ndipo nao wanapoweza kupafikia.
3. Erio ni mwizi na analinda wezi papa hapa PPF kama mifano michache hapa chini
A. Meshaki Bandawe: Alikula hela za wastaafu wa mashamba ya Mtibwa sugar zaidi ya milioni 20. Alipoona soo Erio akamhamishia Mwanza, na kumbambikia Kamanga hela chache zilizobaki. Walipotaka kumfukuza Kamanga naye akamtaja mwizi mkuu kuwa ni Bandawe ambaye ni kipenzi cha Bw, Erio. Erio akalipotezea na Kamanga kufutiwa mashtaka. Sasa kwa nini na wengine nao wasijichotee panapowezekana?
Huyu Meshaki akiwa uhasibu alikula sana pesa ya kodi za majengo na hakufanywa kitu, kutokana ushirika wake na DG Erio. Uhusiano wao nikiutaja hapa hii thread itafutwa leo hii.
B. Martin Mmari: Mkurugenzi wa Fedha ameweka vibaka wake idara ya fedha wanatafuna michango na kumgawia, hili sio siri wafanyakazi karibu wote wanajua. Hata hili la Gisella ni michongo ya MMari lila Gisella hakumgawia akalala nazo mbele.
Mwaka 2004 alitengeneza mazingira na kufanikiwa kununua viwanja vinne vya PPF vilivyokuwa na thamani ya Tshs 56Milion lakini akanuna kwa Tshs 16milion vyote vinne.
C Hosea Kashimba: Huyu ni Chief Internal Auditor. Kila akigundua huwafuata waharifu wamgawie na kulizima soo. Wanaomkomalia huchochea wafukuzwe
Mwaka 2004, Mkurugenzi wa fedha aliponunua Viwanja vinne kiujanja ujanja, akagawiwa viwili ili asihoji. Vijana wanaangalia tu ndio maana nao wakipata mwanya wanavuta kwenye shamba la bibi PPF
Mwaka 2008 Alilipwa Tshs 220 milioni kinyume na taratibu za PPF malipo ya Group endowment ambayo hulipwa kwa mstaafu tu sio aliyekazini kama yeye. Vijana wanaangalia tu. Kama serikari inawaogopa wakubwa basi na wao wakaamua kudokoa mafao ya wazee wasio na hatia. Tatizo in kutamani jinsi mabosi wanavyo ifaidi PPF wakati wadogo wanakufa njaa na kuscramble kwenye daladala.