Mkuu
Mjuni Lwambo, Kwa lugha nyepesi, makadirio ya idadi ya nyota katika ulimwengu wote yamebase kwenye vigezo vya standard za observable universe. Hii ina maana average ya nyota katika galaxi moja [galaxi ziko aina tofauti na size tofauti, ndogo (dwarf galaxies) zinaweza kuwa na maelfu ya nyota kwa kila moja na zile kubwa kabisa (giant elliptical galaxies) zinakuwa na kuanzia trillioni moja mpaka trillioni mia moja kwa kila galaxi], eneo la universe ambalo ni miaka 13.8 bilioni ya mwendo wa mwanga,(Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.) kadirio la idadi ya galaxi ambazo ni zaidi ya bilioni 100 na kwa makadirio ya karibuni ni galaxi 170 bilioni katika observable universe.
Kwa lugha ngumu itabidi niweke calculations za wataalam hao jinsi walivyokokotoa hizi approximation. Sijui hii inatosha?
NB:Lakini pia inawezekana universe ni kubwa maradufu ya hiyo tunayoweza kupima au pia inawezekana haina ukomo (infinite).