Possible Intelligent Life out there

Possible Intelligent Life out there

"haya niliyogusia naweza nikakueleza kwa undani wala hayafichwi"

Basi tuendelee kutiririka hapo ulipo ishia mkuu Monstgala/Mgalanjuka ili 2pate mengi ndugu, nipe hiyo kitu kwa undani basi
Am so interestf

.made in mby city.

Mkuu NICOLAX hayo niliyoandika kwa uchache hakika ni maeneo mazito ya utafiti na makubwa haswa, ili niwe specific we kuwa huru tu uliza kipengele kimoja au kitu kimoja-kimoja tu nami nitajitahidi kufafanua.
 
Mkuu Mjuni Lwambo, Kwa lugha nyepesi, makadirio ya idadi ya nyota katika ulimwengu wote yamebase kwenye vigezo vya standard za observable universe. Hii ina maana average ya nyota katika galaxi moja [galaxi ziko aina tofauti na size tofauti, ndogo (dwarf galaxies) zinaweza kuwa na maelfu ya nyota kwa kila moja na zile kubwa kabisa (giant elliptical galaxies) zinakuwa na kuanzia trillioni moja mpaka trillioni mia moja kwa kila galaxi], eneo la universe ambalo ni miaka 13.8 bilioni ya mwendo wa mwanga,(Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.) kadirio la idadi ya galaxi ambazo ni zaidi ya bilioni 100 na kwa makadirio ya karibuni ni galaxi 170 bilioni katika observable universe.

Kwa lugha ngumu itabidi niweke calculations za wataalam hao jinsi walivyokokotoa hizi approximation. Sijui hii inatosha?

NB:Lakini pia inawezekana universe ni kubwa maradufu ya hiyo tunayoweza kupima au pia inawezekana haina ukomo (infinite).

brother Monstgala hongera na asante sana kwa uchambuzi wako yakinifu juu ya maswala ya anga,galaxy and UFO.binafsi najivunia sana hapa jf kuwa na mtz mwenye kipawa cha hali juu kuyaeleza mambo haya ya kisayansi yaliyo jificha,kwa lugha nyepesi ya kiswahili.nina hakika elimu hii labda hata vyuoni maprofesa hawaifundishi.niruhisu nimtag /nimualike rafiki yangu lawmaina78 toka kenya aje aongeze maarifa na kuuliza maswali pale itakapo bidi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu NICOLAX hayo niliyoandika kwa uchache hakika ni maeneo mazito ya utafiti na makubwa haswa, ili niwe specific we kuwa huru tu uliza kipengele kimoja au kitu kimoja-kimoja tu nami nitajitahidi kufafanua.

Sawa mkuu basi tuendelee
Huko nyuma kwenye mabandiko kadhaa kwenye maada zilizo pita uliniahidi kua utakuja na ishu ya "possible intelligence" and "ROSSWELL INCIDENT" please mkuu naomba unielezee hii kitu ya pili(roswell incident) ni nini hasa?

.made in mby city.
 
Monstgala nina swali dogo sana kuhusu aliens.samahani kama nitakuwa nje ya mada.kuna tetesi kuwa kwa miaka mingi taasisi za kijasui za mataifa makubwa zimekuwa zikifanya tafiti kuhusu aliens na hata kushirikiana na viumbe hao.je kuna ushirikiano huo kati ya binadamu na aliens,emewahi kuleta manufua ya teknolojia kwa wanadamu au hasara?
 
Possible intelligent life ndio mada hii na nilikuwa nataka niieleze hii dhana kwa mtindo wa kujibu maswali, hoja, na maelezo yanayohusiana nayo kwa kuwa tayari kulikuwa na maswali mengi tu hapo kabla. Kwa mtindo huu tungeweza kuzungumzia maswala mengi kwa kuwa specific kwa kila eneo bila haja kuandika kurasa ndefu sana za focus ya pande moja zenye kuchosha kusoma.

Utaona katika ile mada nilijitenga na vitu vilivyohusiana na UFO's maana hivi baadhi ni conpiracy theories, wakati mwingine confusion tu na si uhakika. Roswell incident ingawa ni issue ya kweli lakini si kwamba ilikuwa ni unidentified flying object bali military balloon katika harakati za kuchunguzana wakati wa cold war. Pia utaona wakati ule wa cold war habari za UFOs zilikuwa nyingi zaidi kutokana na usiri wa majeshi ya Marekani na USSR kwenye mambo ya anga, mbinu za kijeshi, technology, na nuclear weapons.

Searching for Possible intelligent life inahusisha very serious researches ambazo katu haziwezi kubeba habari zisizo na grounds. Kama kutakuwa na signs, sightings au signals kutoka nje ya sayari yetu zinachukuliwa kwa uzito sana. Hapa ndipo tunaweza kujadili baadhi ya mambo ambayo yanatafutwa, yanaangaliwa baadhi ya reports zake, theories, hypothesis, projections na mengineyo. Mfano uhai gani unaangaliwa na kuna hatari gani kama kutakuwa na intelligent beings out there, kwa nini hamna jibu lililotangazwa mpaka sasa, etc. Ni tafiti zinazoendelea mpaka sasa hivi tunavyojadili.
 
Monstgala nina swali dogo sana kuhusu aliens.samahani kama nitakuwa nje ya mada.kuna tetesi kuwa kwa miaka mingi taasisi za kijasui za mataifa makubwa zimekuwa zikifanya tafiti kuhusu aliens na hata kushirikiana na viumbe hao.je kuna ushirikiano huo kati ya binadamu na aliens,emewahi kuleta manufua ya teknolojia kwa wanadamu au hasara?

Mkuu kadoda11 Uko ndani ya mada. Ndio kuna tafiti nyingi kuhusu uwezekano wa kuwepo maisha nje ya dunia yetu, nyingi sana. Kuna zile za wazi kabisa na kuna zile ambazo ziko chini ya mamlaka fulani na hivyo mwenendo na ripoti zake si za umma na hazitotewi kwa watu wala machapisho yake hayaendi kuwa published kwenye science journals. Kuna sababu zao. Kuhusu kushirikiana na Aliens kwa kweli hili halipo.

Pamoja na uwezekano mkubwa wa kuwepo aina za maisha huko katika sehemu tofauti za regions za universe au hata katika galaxi yetu hii ya MilkyWay bado kuna vitendawili vizito sana kuhusu swala hili. Vitendawili hivi vitapata step moja ya kutatuliwa pale chochote kuhusu kuwepo kwa aina ya maisha sehemu nyingine ya nje ya sayari yetu. Iwe mabaki ya uhai, uhai katika simple form au sign za mawasiliano au mwonekano halisi wa viumbe hawa basi kila kitu kitabadilika katika maswali makuu magumu waliyonayo binadamu. Impact yake ni kubwa sana na ingawa jamii itachelewa kujua pale itakapothibitika lakini mwisho tutajua tu na tutaandaliwa sana kabla ya kuambiwa.

Hatuna ushirikiano na Aliens na hawajafika kwetu.

Kwa nini?

Technolojia tuliyonayo ni primitive kabisa kama wataalamu wanavyoweza kukadiria kiumbe aliyeendelea zaidi kwa miaka milioni mia tano zaidi ya tulipo sasa. Kama unavyoona sisi bado hatujaweza hata kwenda sayari jirani ingawa tumefikia hatua ya kutuma vyombo tu. Kama tungekuwa tunashirikiana na kiumbe/viumbe waliotoka nje ya dunia lazima watakuwa wametoka kwenye mfumo mwingine wa nyota [solar system is not likely]. Viumbe wanaotoka kwenye mfumo mwingine wa nyota technologia yao lazima iwe ya hali ya juu sana maana umbali uliopo kati ya mfumo wa nyota moja na nyingine ni balaa. Chombo cha kawaida hakifiki kwa sayansi tuliyonayo sasa. Hivyo basi technolojia yao lazima ingekuwa kubwa kiasi kwamba hatuwezi kuvuka hilo gap la uelewa na hatuwezi kushirikiana wala kuitumia. Ni sawa na kumpa nyani laptop awasiliane na mwenzie.

Kutokana na nature ya maisha kama kuna Possible Intelligent beings hawawezi kuwa marafiki tu kirahisi kwamba waje duniani waanze kutufundisha uelewa wao labda iwapo watafaidika kwa jambo hilo. Asili ya viumbe ni kushindana either ni kimoja kimoja au jamii kwa jamii. Kama kuna ushirikiano basi ni kwa faida ya fulani. Wakiingia intelligent beings lazima tutakuwa watumwa au tutawakamata wawe watumwa lakini ushirikiano haupewi nafasi na wataalam wa mambo haya.
 
Angalau nime gain kitu hapo
Mkuu kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaonyesha wazi kuwa wewe ni mmoja kati ya sisi tunao amini kuwa kuna viumbe wanaoshi anga za mbali
Sasa mkuu kutokana, na peruzi zako, kusoma, kuambiwa, kusikia, kutafiti n.k.
Je umeweza kupata feedback yoyote kuhusiana na hawa ndugu waishio anga za mbali katika ulimwengu wetu?
Nikimaanisha tabia zao, maendeleo, tamaduni, lugha, maumbo, n.k.
Natanguliza shukrani mkuu wangu

.made in mby city.
 
brother Monstgala hongera na asante sana kwa uchambuzi wako yakinifu juu ya maswala ya anga,galaxy and UFO.binafsi najivunia sana hapa jf kuwa na mtz mwenye kipawa cha hali juu kuyaeleza mambo haya ya kisayansi yaliyo jificha,kwa lugha nyepesi ya kiswahili.nina hakika elimu hii labda hata vyuoni maprofesa hawaifundishi.niruhisu nimtag /nimualike rafiki yangu lawmaina78 toka kenya aje aongeze maarifa na kuuliza maswali pale itakapo bidi.

Kama kuna kitu nawapendea baadhi ya Watanzania, ni uwezo wa kuchambua mambo magumu kwa matumizi ya Kiswahili. Kuna jamaa yangu moja Bongo, mjaluo ila wale wa Musoma. Yule jamaa aliniwezesha kuelewa issue fulani kwenye fani yangu, kwa muda nilikua natatizika sana na hiyo concept. Baada ya kujuana naye, yaani alinipeleka taratibu hadi nikaelewa neno kwa neno.

Hawa ndio watu hufanya nakua na matumaini na Kiswahili. Fani yangu ya software engineering Kiswahili huwa hakina umaarufu, lakini huwa najaribu sana kukihusisha.

Haya sasa niingie kwenye mada, hivi huwa kuna uvumi kwamba Marekani wamehifadhi UFO fulani ilioanguka humu, ipo ndani ya area 51.
 
Angalau nime gain kitu hapo
Mkuu kwa jinsi nilivyosoma maelezo yako inaonyesha wazi kuwa wewe ni mmoja kati ya sisi tunao amini kuwa kuna viumbe wanaoshi anga za mbali
Sasa mkuu kutokana, na peruzi zako, kusoma, kuambiwa, kusikia, kutafiti n.k.
Je umeweza kupata feedback yoyote kuhusiana na hawa ndugu waishio anga za mbali katika ulimwengu wetu?
Nikimaanisha tabia zao, maendeleo, tamaduni, lugha, maumbo, n.k.
Natanguliza shukrani mkuu wangu

.made in mby city.

Maisha tunayoyajua yanaendana moja kwa moja na mazingira tunayozaliwa na kuishi. Kwa kuwa hata asili ya miili yetu ni hapa hapa duniani basi dunia ndio msingi wa mwonekano ha uhai huu tunaouona sasa. Kama kuna uhai sehemu nyingine nje ya dunia basi uhai huo utakuwa matokeo ya mazingira ya sehemu hiyo. Tofauti ndogo tu ya mazingira ya dunia yanaweza kubadilisha line nzima ya viumbe vikawa vitu tofauti kabisa na vilivyo sasa. kwa mfano mabadiliko ya hali ya hewa ya sasa yanapelekea viumbe vitakavyoishi duniani miaka laki moja ijayo viwe tofauti kama hali hii isingebadilika.

Tamaduni na lugha wanazo binadamu na viumbe katika maeneo mengine ya universe wanaweza wasiwe kama binadamu, labda ni minyoo fulani, labda ni vijidudu au labda ni viumbe vyenye akili sana na nguvu sana zaidi yetu. Kutokana na hili na pia uwingi wa uwezekano kutoka katika machaguo basi wataalam wakaweka mpangilio huu wa viumbe katika makundi ili iwe rahisi kuzungumzia mambo haya. Hivyo possible intelligent beings/civilization zimewekwa katika makundi au aina. Niliwahi kubadika aina hizi katika mada moja na ninaweza kuziweka hapa kwa faida ya wengine ambao hawakusoma mada ile.
 
Vitu vingine tumuachie mwenyezi mungu muumba wa vyote juu na chini ya jua..ni makusudi yake kuumba na ni siri yake pekee..ukifwatilia in deep utaamini kuwa mungu hayupo..
 
Kwakweli mkuu Monstgala/Mgalanjuka sijapata ile ladha kamili ya uzi kama nilivyokuwa nikiutegemea na kuusubiri kwa hamu
Mimi naweza kusema sababu ni kutokuwepo kwa lile bandiko ambalo uliweza kuwa categorize hawa mabwana, kuna baadhi ya maswali naogopa hata kuuliza kwa kuhofia nitaleta mkanganyiko wa hizi maada
Basi mkuu weka lile bandiko hapa kati tuanze kutiririka vyema
Fanya hivyo mkuu ikiwezekana ongezea yaliyokua yame miss pale kati, kwani lile bandiko ndilo lililo nifanya nitengeneze account hapa jf nilikua mpitaji tu mimi
Natanguliza shukrani

.made in mby city.
 
Nitajibu kulingana na mwandishi wa vitabu ambaye pia vitabu vyake vimejenga imani ya dhehebu langu. Anaandika na kusema, katika safari moja, alionyeshwa malimwengu mengine ambayo watu wake wanaishi pasipo dhambi, maana wao hawakukubali madanganyo ya shetani katika kipindi cha kutafuta makazi baada ya kutupwa toka mbinguni, na anaendelea kwa kusema, hata katika safari ya kwenda mbinguni, tutapita katika malimwengu hayo, ili waone namna mwana wa Mungu alivyofanya kazi kubwa kuokoa viumbe wake.
 
The only intelligent life out of this world is of God and I can prove it to you.
If you come to me with evidence that there is god, how should I respond?
a)Start going to church every sunday?
b)Learn meditation so that I can can contact god myself?
c)study the evidence, and if it seems compelling, then try to figure out what sort of god this is?

If you said c), you are my type.

If you said b), I will ask you why you want me to be in contact and worship a god I dont know?

If you said a) then I am curious to know why you think I should leap to the conclusio that the evidence will favor a christian god?

Now let me warn you, be carefull how you answer, this is not areligious topic, we are disscusing aliens and UFO, you will have to be conscious not to spoil our topic, if you start insults i will report abuse.

For you Monstgala, thanks for your knlwledge about aliens and UFO's,I am currently reading IF GOD WERE A SPACE ALIEN, ADIFFERENT KIND OF ATHEISM, it is actually talking about UFO's and aliens, I am getting the same explainations, without your introduction, I would have grasped nothing from the book!
 
naona wazee wa "thibitisha" mnajitahidi "ku-volte-face" maudhui ya mada.teh teh
 
Mkuu kwa kuwa umeuliza mtazamo wangu binafsi kuhusu vyote vilivyopo (nadhani universe kwa ujumla wake) ni wazi mimi nasimamia kwenye nguvu zaidi ya universe ndio iliyo nyuma ya kila kitu kilichopo ila sina asilimia maana hakuna utafiti niliousoma wenye maudhui ya asilimia katika hili.

Asante sana mkuu,jibu lako lina maana kubwa sana ........!!
 
If you come to me with evidence that there is god, how should I respond?
a)Start going to church every sunday?
b)Learn meditation so that I can can contact god myself?
c)study the evidence, and if it seems compelling, then try to figure out what sort of god this is?

If you said c), you are my type.

If you said b), I will ask you why you want me to be in contact and worship a god I dont know?

If you said a) then I am curious to know why you think I should leap to the conclusio that the evidence will favor a christian god?

Now let me warn you, be carefull how you answer, this is not areligious topic, we are disscusing aliens and UFO, you will have to be conscious not to spoil our topic, if you start insults i will report abuse.

For you Monstgala, thanks for your knlwledge about aliens and UFO's,I am currently reading IF GOD WERE A SPACE ALIEN, ADIFFERENT KIND OF ATHEISM, it is actually talking about UFO's and aliens, I am getting the same explainations, without your introduction, I would have grasped nothing from the book!
Why are you whining?

I am not talking about a diabolical "a god" but The God. Your "a god" is dead and I don't care about him/her. When you talk to me you need to grow up.
 
Why are you whining?

I am not talking about a diabolical "a god" but The God. Your "a god" is dead and I don't care about him/her. When you talk to me you need to grow up.
Na nilijua tu utashupalia "God" na "god" badala ya kujibu hoja, kwa sababu huna hoja.

Nilishawahi kusema kuwa bilievers can not manage any intellectual argument, because, most of them are not intelligent.

Sorry, so long!!
 
If you are not interested in my views from that perspective, please just say so. I would rather not waste the time. I'm not looking to argue points of view, just share. If you want that kind of debate, I'm not your man. I'll wait to hear from you before I write and post anything else.

There is no scientific method in depicting someones beliefs unless you have a creepy dude follow you around for a month to see if you live life according to your beliefs

Wherefore, start and learn to answer questions and stop whining, furthermore,
you haven't shown us how is your claim a statistically probable.
 
Jamani wanajukwaa hii maada haikuwekwa kwa ajili ya malumbano ya kuprove nani ni nani
Hata wakipita watu kutoka kule MMU watatucheka sana kwa jinsi tunavyoshindwa kusimamia maada husika na kuingiza maada ambazo ni infinite, jaribu japo kwa bahati mbaya kwenda MMU au JLS uone jinsi watu walivyo makini na maada zao, ila sisi maintelijensia hatuna jipya zaridi ya kubishana about the same thing everytime
Hapa jf kuna nyuzi nyingi sana za ku prove blablah is blablah or is not blabiah
Naomba tunaopenda kurumbana tuende kule na tusio hitaji hayo mambo "LET'S GO BACK TO TOPIC PLEASE"

Welcome back Monstgala/Mgalanjuka

.made in mby city.
 
Kama kuna kitu nawapendea baadhi ya Watanzania, ni uwezo wa kuchambua mambo magumu kwa matumizi ya Kiswahili. Kuna jamaa yangu moja Bongo, mjaluo ila wale wa Musoma. Yule jamaa aliniwezesha kuelewa issue fulani kwenye fani yangu, kwa muda nilikua natatizika sana na hiyo concept. Baada ya kujuana naye, yaani alinipeleka taratibu hadi nikaelewa neno kwa neno.

Hawa ndio watu hufanya nakua na matumaini na Kiswahili. Fani yangu ya software engineering Kiswahili huwa hakina umaarufu, lakini huwa najaribu sana kukihusisha.

Haya sasa niingie kwenye mada, hivi huwa kuna uvumi kwamba Marekani wamehifadhi UFO fulani ilioanguka humu, ipo ndani ya area 51.

Ufo area 51? Uvumi tu. Unajua UFOs ni kwa kiasi kikubwa ni madai kwamba wameona kitu wasichokitambua kikipaa hewani most often duniani, sasa kutotambua kitu hakukifanyi kiwe Alien spacecraft. Kuna vifaa fulani ambavo si vya kawaida sana kwa watu vikionekana basi vitahusishwa na Aliens na hii imefanya UFO iwe saturated sana na conspiracy pia zimo nyingi tu ukijumuisha na confusion.

Mimi nimejikita kuelezea dhana ya Possible inteligent civilizations kwa kuwa hii siyo conspiracy bali kuna utafiti mzito wenye theories makini na first class cosmologists wanahusika.
 
Back
Top Bottom