TimeOut
JF-Expert Member
- Sep 20, 2022
- 3,893
- 8,483
100%? Aisee one thing you should know 100% is something that is not likely to be used in many scientific experiments as a result. Ni unrealistic, 100% ni kwamba katika hali yoyote matokeo yanayotarajiwa yatakuwa sawawasa bila kuwa na punje ya kasoro kitu ambacho ni rare.
Tukirudi kwenye Drake's equation sijui unajua kiasi gani lakini Drake equation ni hoja yenye probabilities. Katika parameters zinazounda equation hii, Drake ameweka makadirio mengi ambayo value zake hazina namba kamili bali range tu kutoka kiasi fulani mpaka kiasi fulani. Kwa hali hii huwezi kupata jibu ambalo litakuwa ni kamili bali litakuwa ni uwezekano tu na majibu mengi sana yanaweza pia kuwa matokeo ya kukokotoa equation hiyo. Hilo moja lakini pia equation yenyewe haikokotoleki kirahisi kwa maana parameters nyingi bado hazina majibu wala si rahisi kukadiria. Utaona bado hatujui kuna nyota ngapi zenye sayari katika Milkyway galaxy, hata average ya sayari zilinazoweza kusupport life katika galaxy yetu bado ni changamoto kujua kwa hakika lakini hata tukipata average na makadirio mengine ya parameters zote katika equation bado jibu la equation litakuwa too vague lakini at least liwe juu ya moja na si chini ya moja. Mfano kama N ambayo ni number of civilizations katika galaxy hii ni zaidi ya moja (+1), hii ina maana hatuko peke yetu. Lakini kama N ikiwa ni ndogo kuliko moja(-1) hii ina maana hakuna uwezekano wa kuwepo extra life katika galaxi hii, hivyo katika Milkyway lote na majinyota bilioni mia mbili kuna uhai katika Dunia tu.
Mfano rahisi kusaidia kumeza: Mtu mmoja mwanakijiji ana kuku wa blue peke yake anajaribu kujua kama kuna kuku wengine wa blue duniani. Parameters anazotumia ni kama ili kujua idadi ya kuku wa blue lazima ajue average ya wafugaji wote duniani, average wafugaji wenye kuku, sehemu ya kuku wenye uwezekano wa kutaga mayai yenye vifaranga wa blue, sehemu ya mazingira yanayopelekea kifaranga awe wa blue na labda muda wa unaotokana na yeye kupata habari hiyo kabla kuku hajachinjwa. Si mfano unaolingana lakini unaweza kupata picha ya equation hiyo ilivyo ngumu. Akiweka values ndogo za makadirio kwenye parameters zake atapata jibu negative kwamba chance za kuku wengine wa blue duniani hamna. Akiweka value kubwa kwenye makadirio yake katika parameter za equation atapata jibu kwamba kwamba kuna zaidi ya kuku mmoja wa blue. Jibu lolote linategemea values za parameters, bahati mbaya hana values hizo na ni mwanakijiji hana reseources za kufanya sensa ya wafugaji dunia nzima ili kupata angalau makadirio ya parameters zake. Kwa sasa kaangalia pale kijijini (Solar system) kaona hamna kuku wa blue wala mfugaji.
Ngumu zaidi ni kwamba Drake equation inaangazia intelligent life na sio just life maana inatakiwa viumbe wawe na uwezo wa kutuma signals au kufanya activity fulani ambayo vifaa vyetu vitaweza kudetect. Katika mifano hapo juu nimerahisisha tu lakini in reality life inayoangaliwa ni ile inayoweza kutuma ishara fulani ili sisi nasi tuzione tujue kuna wenzetu. Hapo utakutana na mambo magumu sana katika parameter za equation hii maana kuna suala la muda na uwezo wa kuwasiliana wa viumbe hao kama wapo. Lakini sio uwezo tu je wana interest ya kuwasiliana nasisi? Je kama mawasiliano yao ni tofauti sana na radio signals au any of which we have, how can we detect them? Au vipi kama ni mijidudu yenye kuwinda uhai mwingine katika galaxi hii na kuutokomeza alafu sisi hatujui tunatuma signals tu! Kwa hiyo hizo parameters nyingine mbili ambazo kwenye mfano wa kuku wa blue hazifit. Ni ngumu kuzikadiria lakini zipo na zinakadiriwa na tunakwenda mbele. SETI walichofanya na kuona uwezekano upo, kwa njia fulani lakini msingi ukiwa ni Drake's equation wakaona hebu tutume signals huko angani tusubiri majibu.
Drake equation haipo kutoa jibu lakini inajenga msingi na inafaa katika utafutaji wa maisha mengine katika galaxi, at least pa kuanzia. Kuna marekebisho pia maana wataalam wengine hawaoni baadhi ya vigezo muhimu na inakuwa si budi kuweka sawa au kuongeza baadhi ya parameters. Tunazungumzia galaxi moja tu (Milkyway) kwanza katika Drake kwa sababu ukiingiza next spiral galaxy kama Andromeda ugumu unakuwa maradufu. Ni kama yule mkulima hajafanya utafiti wa kuangalia kuku wa blue Duniani na anapanga kuangalia mwezini au vyote kwa pamoja. Sijui kama unanielewa mkuu, uliza tu kama hunipati.

mkuu! Upo NASA au SpaceX 




Sent from my TECNO LB6 using JamiiForums mobile app