Possible Intelligent Life out there

Monstgala

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
1,079
1,034
Wakuu,

Nimepata maswali mengi sana kuhusu dhana ya viumbe anga za mbali. Baadhi nitayajibu hapa kadri ya uwezo wangu.

Utata:

Wana-anga na wanasayansi wamekuwa wakiangalia mienendo ya nyota, sayari, miezi na vitu vingine vilivyoko mbali nasi(outer space) na hata jirani na Dunia yetu au katika ya mfumo wa Jua (Solar system) ili kuhakiki kama kuna maisha kwa sasa, au kuliwahi kuwa na maisha kabla. Baadhi, kwa mazingira zilizonayo maisha tuyajuayo hayawezi kutokea, hamna hewa, hamna ardhi , joto ni kubwa sana au dogo kabisa etc. Lakini pia baadhi ya sayari na miezi (moons) zina ardhi, atmosphere, na aina fulani ya kiwango cha hewa ingawa si sawa na uwiano sawia na ule wa Dunia.

Mbali na kuangalia sayari pia kuna utafiti wa ku-trace signals from outer space kama SETI na science institutions nyingine zile za wazi na za siri wanavyofanya na sasa ni muda mrefu utafiti wa aina hii unaendelea. SETI wanabase katika Drake's equation kutambua ni nini kinahitajika katika kujua maisha katika anga za mbali. Mbinu nyinginezo nyingi zinatumika kutafuta alama au ishara fulani ambazo zinaweza kuwa ni either mawasiliano ya viumbe hawa wenyewe kwa wenyewe au labda pia wao kama wanatafuta kujua kama kuna wengineo kama jinsi sisi tunavyodhani.

Msingi

Na kama tujuavyo ni ukweli usio na shaka kwamba kuna nyota nyingi sana zinazofanana na jua letu katika maeneo mengine ya mbali sana kutoka sisi tulipo katika universe. Wanasayansi wanasema nyota zinazofanana na Jua letu ni kati ya asilimia tano hadi ishirini (5% - 20%) ya nyota zote katika Universe tunayoweza kuiona (observable universe). Hili neno la universe tunayoweza kuiona lina maana kwamba pale tusipoona basi kuna uwezekano universe inaendelea au kunavitu vingine tusivyovijua lakini makadirio yanayofanyika ni ya ulimwengu tunaoweza kuuona.

Sasa ukumbuke katika mada ile ya Ukweli wa kustaajabisha kuhusu Nyota, nilisema nyota zinakadiriwa kuwa sextillion 100 au zaidi katika ulimwengu tunaoweza kuuona sasa tukisema mfano tuchukue tu asilimia 5 yake, basi tutakuwa tunaongelea nyota bilioni-bilioni 500 zinafanana kimazingira (joto, ukubwa, umri, aina, uwepo wa sayari) na Jua.

Kwa hiyo basi kama kuna nyota zinazoshabihiana na Jua, na pia zina sayari zinazozizunguka tena baadhi ya sayari zina mazingira kama ya Dunia. Kwa probability na scientific evidence, sayari zinazofanana na jua ni lukuki hii inafanya pia uwezekano wa kuwepo Earth-like planet au sayari zifananazo na Dunia kuwa mkubwa. Kama kuna sayari nyingi zenye ardhi na zenye mazingira yanayofanana na dunia basi inakaribisha zaidi dhana ya kuwepo uhai sehemu nyingine katika ulimwengu.

Cha kushangaza:

Hamna ushahidi uliotangazwa "wazi" kuhusu kuonekana kwa viumbe wengine/uhai so far kutoka kwa institutions hizi, serikali za nchi au mamlaka nyinginezo. Lakini theoretical views, scientific projections, personal claims, and philosophical reviews zinaleta information nyingi tofauti kuhusu possible intelligent beings out there.

Wanaofikiri kuhusu dhana ya viumbe vingine nje ya sayari yetu hawatarajii sana kuwepo na binadamu wanaofanana na sisi, viumbe wa kawaida au uhai kama tunavyoujua. Ingawa hilo linawezekana lakini kumbuka kisayansi mazingira yanachangia sana mwonekano au matokeo ya viumbe. Kama mazingira yakiwa tofauti kidogo basi matokeo ya maisha au viumbe yatafuata mkondo. Hili tunaliona hata katika viumbe wa kawaida wa duniani jinsi wanavyokuwa na vigezo vinavyoendana na wao kumudu mazingira yao. Kwa kuwa hata hizi sayari zinazofanana na dunia haziwezi kuwa na mfanano pacha yani circumstance zile zile basi tusitegemee kukutana na viumbe wanaofanana asilimia mia na sisi. Jinsi kila kitu kinavyoonekana leo hii ni matokeo ya jinsi mazingira yalivyokuwa miaka milioni iliyopita na vivyo hivyo kadri muda unavyoenda.

Kuwa na akili zaidi yetu au kuwa na maendeleo na technology kubwa sana zaidi yetu hili ni wazi na lina sababu zake.

Kwanza kuna uwezekano wa utofauti wa maisha kuanza mapema au baadae hivyo kufanya viumbe wengine kama wapo basi wengine wanaweza kuwa wame-evolve zaidi yetu kwa kuwa na muda mrefu zaidi katika ulimwengu au vice-versa. Kama tukichukua mfano wa dunia yetu (Earth), maisha yanakadiriwa ku-evolve kutoka katika simple form kati ya miaka bilioni 3.5 iliyopita hii ni kutoka kwa evolutionists. Kuna sayari zilizo na muda mrefu zaidi ya dunia na hapa lazima utaona katika hali ya kawaida sisi ndo tunaanza na kuna wengine waliokwisha piga hatua kubwa sana. Na hata tukisema katika sayari nyingine kuna viumbe waliumbwa au walitokea mamilioni ya miaka kabla yetu alafu sasa tujilinganishe nao lazima watakuwa wametuzidi mbali.

Pili, kama kuna viumbe wataweza kufika katika sayari yetu basi hii ina maana technology inayowezesha kusafiri umbali huo si ya kawaida. Kuna umbali mrefu sana kati ya nyota moja na nyingine hasa zile ambazo haziko katika mfumo wa nyota panya au nyota kundi. Hata nyota iliyo jirani yetu si rahisi kuifikia kwa technolojia ya usafiri tuliyonayo sasa.

Kwa kuwa maswali yaliyoulizwa yamekuwa na uwigo tofauti basi ni vyema kuyajibia hapa kwa ujumla wake, pale nipatapo nafasi au mtu mwingine ajuaye achangie.

Karibuni

CC: juve2012 kadoda11 NICOLAX fyddell mtoto wa mjini neo1 Mjuni Lwambo Eiyer CYBERTEQ
 
Daaaaaaah mkuu Monstgala/Mgalanjuka nimefurahi kuiona hii post hapa jukwaani nilikua naisubiri sana,
Mkuu umesema kuna institution ambazo ziko open na ambazo ziko secretly kidogo but all of them deal with possible intellince which are far from us, sasa kwanini institution zingine zinafichwa fichwa, au kuna maslahi kwenye hizi mambo???
Tuanzie hapo mkuu

.made in mby city.
 
Mkuu kabla sijafikiria vizuri kuhusu hili, niulize kwanza,
umesema idadi ya nyota inakadiriwa kuwa sextrillioni 100 na umri wa dunia ni miaka bilioni takribani tatu, unaweza kuwa na Idea walikadiria vipi figure hizo?
 
Mkuu Mjuni Lwambo, Kwa lugha nyepesi, makadirio ya idadi ya nyota katika ulimwengu wote yamebase kwenye vigezo vya standard za observable universe. Hii ina maana average ya nyota katika galaxi moja [galaxi ziko aina tofauti na size tofauti, ndogo (dwarf galaxies) zinaweza kuwa na maelfu ya nyota kwa kila moja na zile kubwa kabisa (giant elliptical galaxies) zinakuwa na kuanzia trillioni moja mpaka trillioni mia moja kwa kila galaxi], eneo la universe ambalo ni miaka 13.8 bilioni ya mwendo wa mwanga,(Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.) kadirio la idadi ya galaxi ambazo ni zaidi ya bilioni 100 na kwa makadirio ya karibuni ni galaxi 170 bilioni katika observable universe.

Kwa lugha ngumu itabidi niweke calculations za wataalam hao jinsi walivyokokotoa hizi approximation. Sijui hii inatosha?

NB:Lakini pia inawezekana universe ni kubwa maradufu ya hiyo tunayoweza kupima au pia inawezekana haina ukomo (infinite).
 
Last edited by a moderator:
Daaaaaaah mkuu Monstgala/Mgalanjuka nimefurahi kuiona hii post hapa jukwaani nilikua naisubiri sana,
Mkuu umesema kuna institution ambazo ziko open na ambazo ziko secretly kidogo but all of them deal with possible intellince which are far from us, sasa kwanini institution zingine zinafichwa fichwa, au kuna maslahi kwenye hizi mambo???
Tuanzie hapo mkuu

.made in mby city.

Kuna baadhi ya scientists wanafanya utafiti kwa kufadhiliwa na mamlaka fulani kwa maslahi ya mamlaka hizo na vivyo tafiti na reports zake humilikiwa vyombo vilivyowaajiri na hazitolewi kwa umma.
 
Mwanaanga Monstgala umekuja tena na haya makitu magumu kuelewa? Matamu kuyasoma, magumu kuyaelewa na kuyaamini.

Huu uzi na ule wa maajabu ya kustaajabisha ya nyota, na ule mwingine wa UFO ingawa uliushika kama mchangiaji niliona kama story za kuaminika tu. Ila tupo pamoja.
 
Nimekuja tena Ziroseventytwo, na kama kawaida tutaelewana tu kama una swali lolote. Unajua cha msingi si kuamini ila kujua angalau kidogo nini kilichopo juu ya dhana hizi.
 
Kwa kweli mkuu inabidi uwe mvumilivu, hapa unadeal na mtu ambaye hajawahi kusoma kabisa kuhusu hivi vitu, shule za kata mkuu ni shida.

Naomba niulize tena, kwenye thread yako kuhusu nyota, umesema kuwa kipenyo au kutoka mwanzo mpaka mwisho wa galaxi tunayoishi, ni umbali wa miaka 100,000 kwa mwendo wa mwanga, hapa umesema eneo la universe ni miaka bilioni 13.8, vile vile kwa mwendo wa mwanga, hapa mkuu umemaanisha umemaanisha pia kipenyo chake au kwa kusema eneo umemaanisha nini?

Ni nini tofauti kati ya galaxi tunayoishi na universe?

Hizo calculations za kitaalamu ziweke tu mkuu, If you have the time, na pia mkuu ningependa kujua sources za information hizi, kama hutojali.
Mkuu Mjuni Lwambo, Kwa lugha nyepesi, makadirio ya idadi ya nyota katika ulimwengu wote yamebase kwenye vigezo vya standard za observable universe. Hii ina maana average ya nyota katika galaxi moja [galaxi ziko aina tofauti na size tofauti, ndogo (dwarf galaxies) zinaweza kuwa na maelfu ya nyota kwa kila moja na zile kubwa kabisa (giant elliptical galaxies) zinakuwa na kuanzia trillioni moja mpaka trillioni mia moja kwa kila galaxi], eneo la universe ambalo ni miaka 13.8 bilioni ya mwendo wa mwanga,(Mwanga husafiri kwa mwendo wa kasi kuliko mwendo wa kitu kingine chochote tunachokijua. Kwa mfano katika sekunde moja mwanga unasafiri umbali wa kuzunguka dunia mara saba.) kadirio la idadi ya galaxi ambazo ni zaidi ya bilioni 100 na kwa makadirio ya karibuni ni galaxi 170 bilioni katika observable universe.

Kwa lugha ngumu itabidi niweke calculations za wataalam hao jinsi walivyokokotoa hizi approximation. Sijui hii inatosha?

NB:Lakini pia inawezekana universe ni kubwa maradufu ya hiyo tunayoweza kupima au pia inawezekana haina ukomo (infinite).
 
Kwa kweli mkuu inabidi uwe mvumilivu, hapa unadeal na mtu ambaye hajawahi kusoma kabisa kuhusu hivi vitu, shule za kata mkuu ni shida.

Naomba niulize tena, kwenye thread yako kuhusu nyota, umesema kuwa kipenyo au kutoka mwanzo mpaka mwisho wa galaxi tunayoishi, ni umbali wa miaka 100,000 kwa mwendo wa mwanga, hapa umesema eneo la universe ni miaka bilioni 13.8, vile vile kwa mwendo wa mwanga, hapa mkuu umemaanisha umemaanisha pia kipenyo chake au kwa kusema eneo umemaanisha nini?

Ni nini tofauti kati ya galaxi tunayoishi na universe?

Hizo calculations za kitaalamu ziweke tu mkuu, If you have the time, na pia mkuu ningependa kujua sources za information hizi, kama hutojali.

Mkuu asante nadhani sikufafanua vizuri juu ya eneo hili nilililotaja. Katika thread ya kuhusu nyota niliongelea kipenyo cha MilkyWay galaxy, miaka "laki moja" 100,000 ya mwendo wa mwanga kutoka point ya mwanzo upande mmoja wa galaxy hii hadi point nyingine ya mwisho upande wa pili.

Katika eneo la universe ninalomaanisha hapa ni lile lenye kukadiriwa kuwa na galaxies bilioni 170. Eneo hili ni miaka "bilioni 13.8" ya mwendo wa mwanga kutoka hapa tulipo kwenda pande zote. Utaona hapa kuna tofauti kubwa sana unapoongelea "laki" na "bilioni". Chukulia dunia kama center ya kipimo chako, na mfano inakuwa na source ya mwanga ambayo kwa kila upande itakaosafiri mpaka kufika point nyingine katika kipindi cha miaka bilioni 13.8, ndio eneo hili linalokadiriwa kuwa na galaxy bilioni 170.
 
Kuna baadhi ya scientists wanafanya utafiti kwa kufadhiliwa na mamlaka fulani kwa maslahi ya mamlaka hizo na vivyo tafiti na reports zake humilikiwa vyombo vilivyowaajiri na hazitolewi kwa umma.

Mkuu Monstgala/Mgalanjuka ahsante kwa reply yako
Mkuu kwa mtu kama mimi nikiangalia benefits za hizo information from secret institution huwa naona ni kama PRICELESS vile, naomba ujaribu kunipa angalau benefits kadhaa za hizo information ambazo zinafichwa kama unaweza kunidokeza japo kwa uchache ili nami nilidhie kua hizi mambo zipo sana
Nahitaji ushirikiano wako hapa mkuu

.made in mby city.
 
Asante mkuu,ngoja nikuitie na wadau wengine ili mjadala huu uwe mtamu zaidi

Kwa heshima na taadhima nawaiteni Mkuu wa chuo , Ishmael , Lisa Valentine kaka km String Theorist Nicholas christine ibrahim Kongosho MTAZAMO Ntuzu Basluma Original njooni tujadili hili kwa pamoja!

Mkuu Asante kwa wito wako!

Nimeona mkuu Ishmael ametoa hoja nzuri kidogo labda tusubiri tuone km ataendelea!

Na Mimi Ngoja nichagize kidogo!

Daniel 12:4

"But you, Daniel, shut up the words, and seal the book until the time of the end; many shall run to and fro, and knowledge shall increase."

Ktk hili fungu tunaona Maarifa kuongezeka! Ni yapi hayo wakuu maarifa yatakayo ongezeka?
 
Last edited by a moderator:
Sasa mkuu Monstgala kwa mtazamo wako wewe unaona kuna uwezekano wa "vyote vilivypo" vikawa vina aliyeviweka na sio kutokea tu kwa asilimia ngapi?

Pia kwa namna unavyoona wewe kuna uwezo wa hayo yote kutokea yenyewe kwa silimia ngapi?
 
Mkuu Ntuzu , thank you for your comments and bringing Daniel as part of our discussion. Ngoja nirudi shule kwenye makabrasha yangu ya Prophecy of Daniel.

1. The Book wa to be sealed until the time of the end. It was then that people would understand the prophecies (knowledge shall increase). In verse 6 the question is asked, "How long shall the fulfillment of these wonders be?" In other words, "When will these prophecies be understood and reach their fulfillment?"

2. Daniel is told two prophecies must be fulfilled before God begins wrapping up the affairs of earth.
The two are:
(a) the 1,290 -day prophecy (vs 11)
(b) the 1,335 -day prophecy (vs 12)

NOTE:
No beginning or ending dates are given for these prophecies. No specific events are attached to them. However, many scholars believe they parallel the periods already covered by the 1,260 - year and 2,300-year prophecies.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Monstgala/Mgalanjuka ahsante kwa reply yako
Mkuu kwa mtu kama mimi nikiangalia benefits za hizo information from secret institution huwa naona ni kama PRICELESS vile, naomba ujaribu kunipa angalau benefits kadhaa za hizo information ambazo zinafichwa kama unaweza kunidokeza japo kwa uchache ili nami nilidhie kua hizi mambo zipo sana
Nahitaji ushirikiano wako hapa mkuu

.made in mby city.

Information za kuwepo au kutokuwepo kwa uhai katika sehemu nyingine tofauti na duniani ni sensitive sana kwa wale wanaojua maana yake. Nitakudokeza kidogo ingawa kuna mengi wao wanayoona ni lazima yawe classified labda kwa muda fulani.

Ikifahamika kwa uhakika kwamba kuna 2nd L. [we are 1st L] basi possibilities nyingine ambazo zinahofiwa sana for future of humanity/life (kikiwemo kiunzi cha uhai, Self replicating Probes, Unfriendly Intelligent beings etc) zitakuwa zimefunguka. Watu wengi hawalijui hili lakini No 2 [other life forms] ina maana maisha yanaweza kutokea au kuumbwa sehemu nyingine nje ya dunia na kwa kuwa sehemu ziko nyingi (trillions) basi kuna maisha mengi sana ya aina nyingi na kwakuwa yanaweza kuanza kwa muda tofauti basi kuna maisha yaliyoendelea sana na kuna yanayoanza.

Information hizi pia zitatengua kitendawili cha kiunzi cha uhai kwa sehemu moja, ambacho kwa sasa kwa kutokuwa na ushahidi wa wazi au uhahika wa 2nd L, ni vigumu kujua kama sisi kama part ya uhai tulishakipita, hatujakipita? (kiko mbele yetu)...kipo? au hakipo?

Hata leo hii SETI wakipata valid signals from space, hawatotangaza kwa jumuia right away. Wenzetu wameshaandaa protocol za kufuata kama wakipata kujua hii kitu na hakika inaweza kuchukua miaka kwa watu wa kawaida kutangaziwa baada ya mlolongo mrefu wa kujiridhisha kuhusu "signals" hizo na mapokeo ya jumuia ya binadamu dunia nzima.

Haya niliyogusia naweza nikakueleza kwa undani wala hayafichwi.
 
"haya niliyogusia naweza nikakueleza kwa undani wala hayafichwi"

Basi tuendelee kutiririka hapo ulipo ishia mkuu Monstgala/Mgalanjuka ili 2pate mengi ndugu, nipe hiyo kitu kwa undani basi
Am so interestf

.made in mby city.
 
Sasa mkuu Monstgala kwa mtazamo wako wewe unaona kuna uwezekano wa "vyote vilivypo" vikawa vina aliyeviweka na sio kutokea tu kwa asilimia ngapi?

Pia kwa namna unavyoona wewe kuna uwezo wa hayo yote kutokea yenyewe kwa silimia ngapi?

Mkuu kwa kuwa umeuliza mtazamo wangu binafsi kuhusu vyote vilivyopo (nadhani universe kwa ujumla wake) ni wazi mimi nasimamia kwenye nguvu zaidi ya universe ndio iliyo nyuma ya kila kitu kilichopo ila sina asilimia maana hakuna utafiti niliousoma wenye maudhui ya asilimia katika hili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom