Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

Willie JM, umenishangaza sana unapoelekea kuunga mkono hoja ya kuongeza posho kwa Wabunge.
Mbunge yeyote, wa Chama chochote ambaye kwa mwaka mmoja ana hakika ya kuishi Dodoma kwa miezi minne kwa mwaka na miaka karibu miwili ndani ya miaka mitano na kila anapohudhuria Mikutano ya Bunge anakaa Hotelini kwa miezi hiyo minne kwa mwaka, NATUHUBUTU KUSEMA Mbunge huyo atakuwa na matatizo ya akili na hana hadhi ya kuwa Mbunge.
 
Kaka William hivi hii attitude ya kuwapa wapiga kura pesa ni priority in your thinking??? Ungepata ubunge ungetupa wote wenye shida tukikufuata hapo Arusha mathalani??? Kuna fedha za mfuko wa jimbo.......why not sustainable projects huko majimboni? Kumpa nyavu au samaki mwenye shida ya kitoweo nini bora kwako??? With all due respects.......umekuja hapa kitaani (Tanzania) recently......watu tumesomea chini.....tumepigwa mabomu ya machozi.....wake zetu wamejifungulia hospitali kwa utata na watoto wetu wanasoma kwa mbinde so we know better mkuu......if to speak of reality you would need more than five years to feel the pinch that is within the nerves na kwa kuwa you have a base for the rest of your life huwezi jua ugumu wa maisha watu wanaoongelea na ndo maana huwezi jua kwa nini suala la posho kuongezwa ni kilio cha wananchi wote


- Really? Duh!

William.
 
Willie JM, umenishangaza sana unapoelekea kuunga mkono hoja ya kuongeza posho kwa Wabunge.
Mbunge yeyote, wa Chama chochote ambaye kwa mwaka mmoja ana hakika ya kuishi Dodoma kwa miezi minne kwa mwaka na miaka karibu miwili ndani ya miaka mitano na kila anapohudhuria Mikutano ya Bunge anakaa Hotelini kwa miezi hiyo minne kwa mwaka, NATUHUBUTU KUSEMA Mbunge huyo atakuwa na matatizo ya akili na hana hadhi ya kuwa Mbunge.

- Sure ni baada ya kuyaona maisha yao kule Dodoma, bado ninasema hii hoja inajadilika tena ni vyema sana ikajadiliwa sasa kuliko late!

William.
 
- Unajua itatuchukua muda mrefu sana kwa mataifa masikini kujifunza kutoka kwa wachina, wao kila sheria zao zinajali mazingara yao zaidi kuliko siasa za kimtaifa, nimetoa hoja kutokana na niliyoyaona na ni kawaida yetu sisi waafrika kwa wananchi kuwafuata wabunge Dodoma kwenye kikao kuwaomba misaada!

- Sasa yes, inapotaka kutatua tatizo la posho za wabunge lazima uliangalie hilo cause ni reality, Wabunge wetu pesa tunazo walipa atleast nusu zinaishia kwenye mikono ya wananchi wa majimbo yao, hiyo ni FACT, lakini mimi naongelea niliyoyaona Dodoma as a reality, sio hadithi za mtaani!

William.

Talking about china last year nilikuwa kule mji flani unaitwa xian ... nilikwenda kutembelea chuo kimoja kinaitwa xian jaotong ...! hu jintao alikuja kutembelea pale chuoni akiwa ndani ya coaster BUS lenye vioo vya tinted .. ndani akiwepo yeye na baadhi ya viongozi na walinzi ! HUYU NI RAIS WA CHINA nchi tajiri kuliko sisi..!? iweje sisi maskini tulilie maisha ya kifahari ..?! AMKA MKUU!
 
Ni hoja ya msingi, ila inahitaji mtazamo mpana na siyo kwa wabunge tu,
Ugumu wa maisha dodoma tusiuweke kwa wabunge peke yao, mimi nadhani wabunge wanatakiwa wajiweke kwenye maisha ya kawaida (standard), hasa wale wanaotegemea posho tu.
Fikiria mfanyakazi wa serikali ambaye naye huenda kwenye kikao Bungeni Dodoma (kumpiga tafu waziri/wizara) , naye huishi hapohapo dom, naye hutakiwa kulsa na kulala hoteli nzuri kwa kuwa anakuwa na nyaraka muhimu kwa nchi... je tujiulize yeye alale wapi? Sipingi heshima ya mbunge , ila naamini kwa kipato cha mbunge ( 80,000 perdiem, posho ya kikao 70,000/=) hivyo kwa siku hukusanya takribani 150,000/= si haba!!!. H
Hebu rudi kwa mtumishi wa serikali -(afisa mwandamizi) hupata posho ya Tsh 80,000/= tu kwa siku. Je mbunge bado hajapewa heshima yake tu...
Kwa uzoefu wangu dodoma kuna hoteli nzuri tu za Tsh 30,000-50,000. tusitengeneze matabaka ya wenye nacho na wasio nacho. Tunapolingalia hili tuangalie watumishi wote na siyo wabunge tu, maana wote hunda soko moja, petrol station moja, n.k.... huo ndio mtazamo wangu
 


Talking about china last year nilikuwa kule mji flani unaitwa xian ... nilikwenda kutembelea chuo kimoja kinaitwa xian jaotong ...! hu jintao alikuja kutembelea pale chuoni akiwa ndani ya coaster BUS lenye vioo vya tinted .. ndani akiwepo yeye na baadhi ya viongozi na walinzi ! HUYU NI RAIS WA CHINA nchi tajiri kuliko sisi..!? iweje sisi maskini tulilie maisha ya kifahari ..?! AMKA MKUU!

- Huna uhakika na unchokikubali au kukitaa, hapa ni kwamba unakubaliana na mimi kwamba Serikali ya China wamempa Coaster, sasa na sisi tuwape malazi kuwapa hela nyingi za posho!


William.
 
willy,

naona utakapokuja kuzinduka tayari kutakuwa kumekucha! tanzania yetu ya sasa unahitaji akili kama ya mwendawazimu kuweza kuwaombea nyongeza ya posho wabunge!

ubarikiwe
 
Niulize tuu swali moja kwa William
Mwananchi ambaye anaishi chini ya dola moja hapa kijijini kwangu Hungumalwa ambaye hana uhakika wa kesho wala hajui mtoto wake atapata wapi shs 2000 ya kulipia ulinzi wa shule au debe la mahindi kwa ajili ya uji anapata wapi nauli ya karibu laki kwenda na kurudi kutoka hapa hungumalwa kwenda kumfuata mbunge dodoma
Na je akienda dodoma kumuona mbunge wake huyo anarudishiwa nauli yake na kupewa pesa nyingine kutokana na shida yake au ndo anaenda kumuona mbunge na anapewa elfu ishirini na kuambiwa asante
Je kwa nini kama huyu mwananchi ana shida zake hizo nauli na matumizi ya kukaa pale dodoma kumuona mbunge si yanagetosha kusolve matatizo yake
Hivi hao wananchi katika hali ya kawaida wanawafuata wabunge kweli kwenda kuwalilia shida au wameitwa na hao hao wabunge kwa sababu zao binafsi za kisiasa
Maana kwa mbunge ambaye toka achaguliwe hajawahi kufika jimboni mwake na wala hajui maisha ya wananchi wake sidhani ni busara kumsemea kuwa huyo ameenda dodoma kwa shida
 
William weka hii video kwenye post yako ya mwanzo kabisa.

 
Last edited by a moderator:
willy,

naona utakapokuja kuzinduka tayari kutakuwa kumekucha! tanzania yetu ya sasa unahitaji akili kama ya mwendawazimu kuweza kuwaombea nyongeza ya posho wabunge!

ubarikiwe

Hilo halijamwingia akilini bado! Dawa hakuna mahospitalini, vitendea kazi duni, hospitali nyingine za mkoa hata chumba cha upasuaji hakuna! Wanafunzi kukaa chini, walimu hakuna Wa kutosha, mishahara ya watumishi ndo usiseme, kweli ni sawa kusema posho ya wabunge iongezwe? William hajafikiria vizuri kwa hili
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

- Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani,
infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

- Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.



William John Samwel Malecela @DSM City!
Hapo kwenye highlight; Hata Tanzania mradi kama huo upo mbioni. Kwa kuanzia, unit kama 200 hivi zitajengwa Dodoma kwa ajili ya makazi ya wabunge. Lakini, wabunge weng hawaufurahii mradi huu kwa sababu kuna argument kwamba iwapo watapewa nyumba, basi perdiem zao zipunguzwe, na wengi hawataki kulisikia hilo
 
hizosehemu 'very dangerous ni zipi?'

ina maana wakishachaguliwa kuwa wabunge wanakuwa very special wanaogopa wapiga kura wao? Unataka kusema wakati wa kupiga kura wanaweza kujichanganya nao, wakishapata ubunge wanakuwa 'special' kujichanganya nao ni 'hatari kwa usalama' wao?

Ndo maana miaka 50 yote ya madaraka ya ccm maendeleo majimboni hakuna

Halafu sehemu kama Simba mbona ni hoteli nzuri na wanajazana pale chungu nzima na hoteli sh 20,000-25,000 wakati hoteli ya 'hadhi ' ipo jirani hawaendi?

Unataka kusema hawalipwi perdiem? Maana kama wanaliowa perdiem sh 80,000 perday, inawatosha sana tu, sh 65,000 unalipia hoteli sh 15,000 unakula......

Tatizo sio bei za hoteli, tatizo sio hadhi za hoteli tatizo ni uroho na uchu wa fedha..........
Kujali matumbo yao binafsi kuliko wapigakura wao.....???

Au nataka kusema wabunge waliopinga hilo wao hawakai hotelini?

Bila kusahau pia kuwa hawa jamaa ni wapenda anasa - Ngono na Pombe.

Wanalipwa accomodation ya Tsh 70,000 and meals Tshs 80,000; jumla ya Tshs 150,000 kwa siku. Iweje useme hii hela haitoshi? Huyu William anataka hawa watu waishi maisha ya peponi kwenye taifa hili la watu wa maskini wa kutupa.

Nadhani ungeanza kuongelea umaskini unaowakabili wagogo kuliko kudandia hoja ya posho. Posho za wabunge si muhimu kiasi hicho.

Tuna wanafunzi kuanzia chekechea hadi chuo kikuu wana shida nyingi ambazo hazijatatuliwa. Wanajiuza ili kuweza kujikimu kimaisha wawapo vyuoni. Hili haujaliona kuwa ni tatizo bali posho za wabunge.

Je posho za wanafunzi vyuoni zinatosha? Je unajua wanalipwa shilingi ngapi kwa siku? Je wanazipata kwa wakati ama ni mpaka waandamane?

Kujadili vitu vingine ni upuuzi.
 
Mbunge analipwa per diem kama wafanyakazi wengine kwa viwango vya kawaida ambavyo vimekuwa calculated kulingana na hali ya uchumi wa nchi na kuangalia bei halisi za vitu. Hizi rates za per diem haziwekwi na bunge.

Mbunge analipwa posho ya mafuta ya gari kwa kila siku kwa ajili ya usafiri wake.

Watu walichopigia kelele ni SITTING ALLOWANCE. Kwa nini ilipwe sitting allowance kwa kukaa vikao ambavyo mbunge amesafiri kwenda kuvifanya na akalipwa hela ya kujikimu? Ni sawa na Engineer asafiri kutoka Dar kwenda mtwara kujenga daraja, alipwe posho ya kujikimu akiwa huko mtwara, halafu akishafika kule anapoenda site alipwe tena posho ya kwenda site!! Watu wanauliza hiyo ni posho ya nini?

Kama posho haitoshi, basi suala liwe ni posho ya kujikimu! Hii ikiongezwa mfanyakazi yeyote itaongezwa. Wabunge waliona waongeze sitting allowance kwa sababu kuongeza posho ya kujikimu hawakuwa na uwezo nayo! Hiyo ikiongezeka huwagusa wafanyakazi wote. Sasa wakaona waongeze ile posho inayowahusu wenyewe tu!!

Hiki kinachoitwa SITTING ALLOWANCE ni conduit ya kuibia kwani hakuna mfumo unaoeleweka wa ni nani anatakiwa alipwe posho hii, wakati gani na kwa nini? Mara nyingi kwenye vikao vya maofisa wakubwa wakubwa serikalini (wale wenye uwezo wa kutumia fedha za serikali) ndo posho hizi hulipwa na viwango vyake ni "arbitrary". Kila ofisi wanaamua kulingana na kina cha mifuko yao (Yaani pesa za walipa kodi zilizoko chini yao). Hili ndo tatizo la sitting allowance! Huwezi kujua ni vikao gani vinatakiwa hii posho ilipwe na viwango vyake vikoje, na ni nani anapanga!

Hili la wabunge kuwashughulikia shida za wapiga kura binafsi, ni uamzi wa wabunge wenyewe. Haliwezi kuwekwa kama sehemu ya majukumu ya wabunge kwani hakuna mwongozo wowote unaomtaka mbunge kutatua shida binafsi za wapiga kura wao. Mbunge binafsi akiamua kufanya hivyo, na afanye; lakini isiwe sababu ya kudai malipo. Tena hili inatakiwa lidhibitiwe isiwe chanzo cha wabunge kuwahonga wapiga kura wao. Wabunge hawachaguliwi ili kutatua shida binafsi za wapiga kura wao!!
 
- Huna uhakika na unchokikubali au kukitaa, hapa ni kwamba unakubaliana na mimi kwamba Serikali ya China wamempa Coaster, sasa na sisi tuwape malazi kuwapa hela nyingi za posho!


William.

Kwa hiyo kwa akili yako wakipewa hela nyingi ya posho ndo utakuwa umetatua tatizo.

Je, hela huwa inatosha?

Je, hela nyingi ni kiasi gani?

Je, hizo hela zinatoka wapi?

Je, hakuna vipao mbele vingine kwa taifa zaidi ya kutunga sheria?

Je, ukiwapa hela nyingi wabunge ndio watatunga sheria nzuri na kuisimamia vyema serikali?

Je,..........?


Nakushauri urudi Marekani bwana mdogo William.

 
- Mimi nimeongelea Wabunge niliowaona tayari na wewe ongelea hao uliowaona, hii hoja ya posho za wabunge inajadilika bro, kama sio leo itakwua kesho tena ikiwa very ugly, badala ya kuwapa 200, 000 tutaishia kuwapa zaidi ha hizo!

- Mengina huwa ninaita kelele za mlango!

William.

Mkuu naona unaandaa posho ili inshallah mwaka 2015 ukiwin kuwe na maslahi siyo?

Huwezi zungumzia hao maana huna mpango wa kuja kuwa polisi, mwalimu, nurse nk,
unampango wa kuwa mh sana mp
 
hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku;
Mkuu ndio nini hii Hadhi ya wabunge...?
Kwa kutumia pesa zao wenyewe hata wakikaa kwenye hoteli ya hadhi ya mfalme no body cares.., lakini kwenye kodi zetu hakuna cha hadhi hapa....

Hii issue ya ku-underline matabaka ndio kunapelekea kuwa na mabwana na watwana kwa watu wanaojifanya kuwawakilisha wananchi (ambao wengi wao ni masikini na hawana hata shuka la kujifunika let alone kuta na paa la kujikinga na mvua
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

- Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani, infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

- Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.



William John Samwel Malecela @DSM City!

Nimekaa pale NAM hotel pana vyumba vya elf25 pana security nzuri tu na mbunge anaweza kuishi hapo bila Tatizo labda sijajua vizuri unaposema hadhi ya Mbunge unamaanisha nini maana kwa mtazamo wangu Mbunge namuona ni mtumishi wa Umma kama Mimi. Hiyo Dodoma hotel ni another level kama Watalii nakadhalika na siyo Mtumishi wa Umma. Ukisema Dodoma Hotel ni hadhi ya Mbunge unamaanisha Waziri atafute hotel ya juu zaidi ya Dodoma Hotel. Hizo Dodoma hotel tuwaachie wafanyabiashara kama Riziwan na Rostam
 
Ugumu wa maisha ni kwa kila mtanzania, Mbunge, mhandisi, mwalimu, shehe, padri, mwanafunzi, mkulima, mfugaji, mwizi, kahaba, mfungwa na kadhalika.

Hakuna sababu ya kuwachukulia wabunge Kama watu ambao wake affected zaidi ya wengine, wananchi wote wanapigika sana mtaani, wanapigika mpaka wanaichukia CCM, kwa sera zake ambazo zinadhana kwamba Mtu anayepata posho ya 200,000/= kwa siku ana maisha magumu hivyo inabidi aangaliwe kipekee na Yule mkulima anayeshindia alfu kwa siku anasahaulika.

Maisha ni magumu huku mtaani, ondokeni Dodoma Hotel, tokeni bungeni kwa masaa, tokeni ofisini na kwenye magari yenu muone watu wanavyopigika huku mtaani.

Ubhakufifye!!!
 
- Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?


William.

Kuchukua Rushwa ni Tabia siyo ugumu wa maisha. Ndiyo maana ukiwauliza baadhi ya machangudoa kwanini wanafanya hiyo kazi wanadai kwasababu ya maisha magumu, hebu tafakari ugumu wa maisha ingekuwa ndiyo sababu pekee ya kufanya umalaya tungekuwa na Machangudoa kiasi gani nchini?
 
Back
Top Bottom