Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

Hivi wewe Wiliam ndivyo unavyofikiri. Hivi ni wabunge tu ndio wanaoishi dodoma, hao wananchi wengine wanaokwenda kikazi dodoma wanalipwa kiasi gani? Suala la kuwepo resthouse za wabunge ni zuri, lakini baadaye unasikia zimeuzwa kwa wabunge hao hao. Hauna jipya zaidi ya kujenga matabaka. Kama ni suala la per diem wanapata, halafu wanapata seating allowance na allowance nyingine. Wafanyakazi wengine kama madaktari wanashindwa kulipwa. Hawa wabunge wana kitu gani tofauti na binadamu wengine. Eti wanategemewa na wapiga kura wao, nini, kutoa rushwa? nani asiyetegemewa katika nchi hii. Nani asiyejua wafrica tuna extended farmilies. Tuache mambo ya kujikomba kutafuta nafasi binafsi. Tuufikirie umma kwanza. Umeona hizo picha za watoto wetu wanaposomea? Afadhali hata ubunge uliukosa. Uzi huu utakushusha sana. Nimesikitika sana, nimesononeka sana. Basi tu. Hivi unajua kuna fungu la mbunge kwa ajili ya jimbo lake, hizo fedha kazi yake ni nini? Tusiendekeze umatonya, tufikirie kuwawezesha wananchi kujitegemea.
 
Pole mzee..bt tusikilize hoja zake na kumuelimisha kuhusu hali halisi ya watanzania. Unaezakuta hana picha halisi mtanzania anaishije ukizingatia amekulia familia gan.
 
Tatizo posho Hisiwe kwa kundi fulani tuu ( hasa wabunge ) iwe pia kwa makundi mengine then tuone faida yake.
 
Naona michanganyo mingi. je, kwa mbunge hiyo elfu 70 anayolipwa inategemea kulipia nini?
Nafikiri perdiem siyo part ya hii, hii ni posho juu ya perdiem, mwenye ufahamu atujuze ili tujadili tukiwa na ufahamu.
 
Nilijua utatetea tu Posho na kutoa sababu za kutosha kuwalaumu wale wabunge wapinga posho. Kwangu mie nadhani utatuzi wa kudumu ni kuwa na mpango mkakati unaotekelezeka wa serikali kujenga hostels au nyumba za wabunge hapo Dodoma. Niliwahi kuusikia huu mpango japo sijui uliishia waapi. Taarifa ninazokuwa nazo ni kuwa wamiliki wakubwa na wengi wa hizo mansions ni walewale vigogo na ndo wale wale wanaopinga au kuchelewesha ujenzi wa nyumba za wabunge hapo Dom. Ukiangalia gharama kwa mwaka na ukajumlisha mwa miaka kumi utaweza kusema hii serikali yetu inaelekea wapi!!!!!!
 
- Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?


William.
Ubunge ni utumishi na sin ufalme, kazi hiyo niya kujitolea kutumika sio mahali pa kuneemekea, tatizo tumefanya ubunge kama ufalme ndio maana kila wakati wanajadili maslahi yao badala jinsi ya kuwatumikia wananchi.
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

- Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani, infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

- Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.



William John Samwel Malecela @DSM City!

Sio lazima kuwa mbunge. Kama hiyo kazi wanaona haiendani na kipato wanachokipata, ziko kazi nyingine za kufanya. Umeshawahi kujiuliza kwanini huwa wanaacha kazi zao za maana na zenye kipato kikubwa na kukimbilia ubunge ambao wanajua ni kipato gani watakachokuwa wakikipata?

Mkuu usiyaangalie maisha ya watanzania kwa 'majicho' ya kimarekani au ulaya ulaya. Kama hiyo kazi wanaona ni kupigika, ni vyema wakajitoa ili wenye lengo la kutuletea maendeleo kwa kiasi hicho hicho cha posho ya 70,000/= kwa siku wachukue nafasi zao. Kazi ziko nyingi za kufanya sio lazima ubunge!

Mkuu usianze kujitengenezea mazingira ya 'ulaji' kabla hata hujafikia lengo lako la kuwa mbunge. Inatia shaka pindi ukiingia huko mjengoni kama kabla ya kuwa mbunge tayari umeanza kuwa na mtazamo wa kimaslahi zaidi!
 
- .......... ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi......................

William John Samwel Malecela @DSM City!

..........kweli mtanzania hata ukimfundisha namna gani nzuri ya kujenga taifa lake, atafanya hayo akiwa huko huko ughaibuni pindi akirudi tu Bongo..........usitegemee mabadiliko yoyote! Bado navuta taswira ya utendaji wa Gavana Balali na hili unaloanza kuliongelea na kulijengea hoja..........stil downloading, mweeeeeeee!
 
siasa za maji taka ili kuwafurahisha wabunge wa ccm....damn idiot....hivi ile safari ya kutembelea vijijini kwenu ugogoni kwenye umaskini uliokithiri ilikusaidia kweli we????..au kwa vile sasa uko dar umeshasahau vijijini kwenu wanaishije wagogo wenzako????????....by the way..hivi we unafanya kazi kweli we???..maana ungekua unafanya kazi na unakatwa kodi usingekuja hapa na haya mashonde.......Angalizo tu kwako: mwenyekiti wako wa chama (JK)alizikataa nyongeza za hizi posho.......sasa we hapa unaongea kwa niaba ya nani???....nani amekutuma?????....unamfanyia nani udalali hapa we????
Ebu kwa kukusaisaidia tu...(maana naona huna kazi ya kukufanya busy we)..nenda pale NIMR kamwombe dada yako Mwela angalau kazi ya udereva....hata ya kumwendesha tu...maana wanasema...'an idle mind(like yours).is a devil's workshop'....very true........

Mkuu taratibu aisee. Jamaa bado ana matongotongo ya marekani akikaa walau kwa muda akijiandaa na mikakati yake ya 2015 anaweza kubadili hiyo kauli yake.

Gia anayoingia nayo inamdhalilisha yeye na Mzee pia maana kwa uelewa na nguvu alokuwa nayo Mzee Malecela inaonekana ni kinyume kabisa na damu yake inayojaribu kufuata nyayo zake. Mkuu unajivua nguo, tuliza akili fikiria kitanzania zaidi na sio kukurupuka kama msukule!
 
- Europe ukishitakiwa na kesi ya rape, jaji huwa anataka kujua jinsi victim alivyokuwa amevaa kwanza, kama hakuvaa inavyotakiwa unaanchiwa kwamba aliyataka, sasa mbunge akipewa rushwa inatakiwa tujiulize mazingara yakoje?

William.

mpendwa,

wewe ni muongo na unapaswa kutubu!

europe gani hiyo unayoizungumzia wewe ambayo wengine hatujafika? nenda basi kesho club ukamkamate queen dancer mwenye bikini halafu uone kitakachokupata!

kaka willy,

ubarikiwe sana mpendwa

Glory to God!
 
- Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.


William John Samwel Malecela @DSM City!

Hivi kule MTERA anapotekea Mbunge wako wa MTERA hii hotel ipo?

Je wakati wakampeni mukienda huko vijijini hii hotel ipo?

Igunga na Arumeru tumeona watu wanalala sehemu za ajabu kabisa na hatukuona DODOMa hotel huko,

Hii haina tofauti na lile la magari , Mkipata UWAZIRI mnadai mnataka V8 kisa njiaa azipitiki lakini mkiwa wabunge mkipewa mkopo wa magari mnanua RV4 na Corrrola.

Yani we jamaa tokea Ufungue ile PONOGHRAPHIC Blog nimekushusha sana na kwa hili ndio kabisa.
Ushahuri w abure RUDI BAHARINI tu ndugu yangu.
 
Mtanzania hata aelimike vipi, akiona kichaka lazima akikojolee! hili linajidhihirisha hapa
 
Ubunge ni utumishi na sin ufalme, kazi hiyo niya kujitolea kutumika sio mahali pa kuneemekea, tatizo tumefanya ubunge kama ufalme ndio maana kila wakati wanajadili maslahi yao badala jinsi ya kuwatumikia wananchi.

Hawa ndio walitoa ile NDUGU. na kuweka MHESHIMIWA, Puzii kabisa anawaheshimu nani hawa wezi?
 
William Malecela,
Mkuu wangu nadhani suluhisho la mgogo wote huu lingewezekana tu kama serikali ingeweza kuunda mfumo mzuri zaidi wa malipo kwani wanapokuwa Dodoma na Dar pia hupokea mishahara yao japokuwa hawapo majimboni ama hawashughuliki na kazi za jimbo lao.

Kweli maisha yamepanda sana kiasi kwamba hizo Tsh 70,000 kwa siku hazitoshi, lakini hilo ongezeko la kufikia 200,000 kwa siku bado hujachanganya na posho nyinginezo, mishahara na kadhalika - huoni kama wabunge wetu wanatubeza hasa walimu na madaktari wetu ambao hupokea mshahara mzima kwa mwezi mdogo kuliko pato la mbunge akiwa Dodoma kwa hizo siku chache.


Halafu Mutuz, hawa wabunge siku zote wanaishi Dar sii majimboni ina maana kama hakuna vikao vya bunge inakuwaje wanaweza kuishi Dar wakaacha kukaa majimboni maana maisha ni magumu zaidi ugenini? Sasa ugumu wa maisha yao wakiwa Dar mbona hatuusikii isipokuwa ktk vikao vya bunge.

Maisha magumu kote, kinachotakiwa kufanyika ni wabunge wote lazima wagombee sehemu wanazoishi ili kupunguza gharama za maisha, au makao makuu yahamie Dodoma ofisi zote za serikali zihamie huko bila shaka hawa wote watalazimika kuhamishia familia zao Dodoma badala ya kukaa Dar wakivizia mawaziri na manaibu kuomba na kubembeleza wapelekewe maendeleo majimboni.
 
Most, if not all, CCM members think the same!

Wananchi kuomba/kumtaka mbunge ashughulikie mambo yao ya binafsi ni zao la kutowajibika kwa wabunge wa CCM. Kushindwa kwao kuisema/kusoa/simamia/wajibisha serikali na badala yake kuisifia/kumbatia huku wakitegemea iwajaze mapesa ya kuhonga majimboni kutazidi kuwatesa daima.

Huwezi maliza shida za wananchi kwa kuwagawia pesa.
 
Sio lazima kuwa mbunge. Kama hiyo kazi wanaona haiendani na kipato wanachokipata, ziko kazi nyingine za kufanya. Umeshawahi kujiuliza kwanini huwa wanaacha kazi zao za maana na zenye kipato kikubwa na kukimbilia ubunge ambao wanajua ni kipato gani watakachokuwa wakikipata?

Mkuu usiyaangalie maisha ya watanzania kwa 'majicho' ya kimarekani au ulaya ulaya. Kama hiyo kazi wanaona ni kupigika, ni vyema wakajitoa ili wenye lengo la kutuletea maendeleo kwa kiasi hicho hicho cha posho ya 70,000/= kwa siku wachukue nafasi zao. Kazi ziko nyingi za kufanya sio lazima ubunge!

Mkuu usianze kujitengenezea mazingira ya 'ulaji' kabla hata hujafikia lengo lako la kuwa mbunge. Inatia shaka pindi ukiingia huko mjengoni kama kabla ya kuwa mbunge tayari umeanza kuwa na mtazamo wa kimaslahi zaidi!


- Sio lazima kuwa na Muungano, tuliyasikia hayo nyuma kule lakini sasa muafaka wa CUF na CCM, hoja ya posho inajadilika sana, sema tuta-delay lakini kuna siku itakuja kututafuna taifa!

- Otherwise kwa wengine wote kama nilivyosema kule nyuma, Machame nilienda tu kutembea kwa a good friend nothing to do na kujiunga na Chadema kama wengi walivyotegema na wengine wameenda mpaka kunishitaki kwa wakubwa wa chama changu! ha! ha! ha! ha!

- JAMANI HUKU BONGO NI USIKU SAA HIZI NAWAHI MSONDO NGOMA KUONA WANANCHI WAKIONYESHA TALENTS ZAO ZA SANAA, HA! HA! HA! USIKU MWEMA WENGINE SIWEZI KUWAJIBU MAANA HOJA ZENU HAZINA MASHIKO KABISAA, WENGINE MNAKUWA KAMA WATOTO WA CHEKECHEA BANA, HA1 HA! HA!

William.
 
Mkuu posho ya wabunge ni kubwa sana kulinganisha na mahitaji unayosema. Kwanza mbunge ana 80,000/= kwa kila siku (DSA) kila anapokuwa Dodoma aingie bungeni au la. Halafu anapata 70,000/= kila anapohudhuria kikao kila siku. Hivyo jumla anapata posho tu 150,000/= kwa siku ukitoa 50,000/= ya chumba anabakiwa na 100,000/= kwa siku. Hizo hazitoshi kula?
.
Mkuu umesahau 50,000 za mafuta kila siku. Sijui dod6a matembea km zote hizo kwenda wapi. Hizo ni nje ya mafuta ya kila mwezi lita 1,000.
 
- - JAMANI HUKU BONGO NI USIKU SAA HIZI NAWAHI MSONDO NGOMA KUONA WANANCHI WAKIONYESHA TALENTS ZAO ZA SANAA, HA! HA! HA! USIKU MWEMA WENGINE SIWEZI KUWAJIBU MAANA HOJA ZENU HAZINA MASHIKO KABISAA, WENGINE MNAKUWA KAMA WATOTO WA CHEKECHEA BANA, HA1 HA! HA!

William.

Mkuu W. J. Malecela, naona unaanza kula matapishi yako kwa kuwa personal tena. Mara nyingi wadau wakikwambia maneno kama hayo juu, wewe uanza kulalama kwa kusema that's personal.
Walk the talk mzee.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom