Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho za Wabunge na Maisha ya Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 24, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Heshima mbele JF, hivi karibuni nilikuwa Dodoma hili la Wabunge na posho limenishitua sana ukizingatia kwamba nilikuwa mmoja wa wananchi waliopinga sana Wabunge kuongezewa posho, there I was in Dodoma, hotel ya hadhi ya wabunge ni Dodoma hotel, bei ya chini sana kwa chumba ni Sh. 65,000 kwa siku; ukienda mtaani ni sh. 50,000 kwa siku, I mean bado wabunge hawajala na ku-deal na wananchi kutoka majimbo yao ambao humiminika kila siku Wabunge wanapokuwa Dodoma, kuwalilia shida za binafsi.

  - Serikali itafute suluhisho la hili tatizo kwa sababu ni tatizo, tunaawaacha wabunge in an open field ya kupokea rushwa, nimeona Wabunge wengine wakiishi sehemu ambazo ni very dangerous kwa kiongozi wa taifa tunayemtegemea kuishi, halafu unakuta magazeti yakifurahia mbunge apigwa mapanga, mbunge aibiwa, I mean as taifa we have to do something, nchi nyingi Duniani, infact hata Zambia tu Serikali imewajengea Special Hostel wabunge wake kwenye maeneo ya viwanja vya bunge kupunguza hili tatizo la posho, I mean kwa hali niliyoiona hili tatizo halikwepeki ni lazima lizungumzike.

  - Nilichojifunza kule Dodoma ni kwamba wengi wa Wabunge waliokuwa wanapinga posho ni wale wenye uwezo mkubwa sana kipesa kwamba hata hawahitaji hiyo posho ya sh. 70,000 kwa siku maana kwao ni peanuts na ni wachache sana, ninasema hii hoja ijadiliwe tena, tunawaweka wabunge wengi pagumu sana kimaishana hata kutuongoza.  William John Samwel Malecela @DSM City!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana mkuu. Kumbe mwanzoni ulikuwa ukitoa maoni bila kujua hali halisi ikoje! Sasa hili ni funzo kuwa watu wawe wanatoa maoni yao kwa kuelewa hali halisi inayowahusu watu wa site. Kwa maana hiyo kuna mengi ulikuwa huelewi hadi uliporudi nyumbani na kabla hujaelewa vizuri ukajitosa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki. Nadhani umejifunza utakaa na kuelewa hali halisi ya watu, uchumi na siasa kabla hujajitosa tena kugombea. Hii itakupa fursa nzuri ya kuwatumikia watu kama utafanikiwa kwa kuwa utakuwa umejua shida na matatizo yao na matatizo ya nchi kwa ujumla.
   
 3. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwani hizo Special Hostel kwa Tanzania zinashindikana kujengeka???,

  So far, hiyo posho inayotolewa inatosha kuwa-acommodate hao Wabunge; mbona watumishi wengine wa Serikali wanaajiriwa na kupangiwa Vituo vyao vya Kazi ma-Wilayani na Mikoani ambao hakuna nyumba za kuhishi na wala Posho za Nyumba hawapewi lakini wanafanya kazi?????

  Ambaye hataki Ubunge aache hakuna aliyemlazimisha.
   
 4. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Wabunge wa Afrika Mashariki mshahara Tsh. 17m, posho kwa kikao laki 9, mkopo wa shangingi Tsh.90m
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Ugumu wa maisha ni kwa kila mtanzania, Mbunge, mhandisi, mwalimu, shehe, padri, mwanafunzi, mkulima, mfugaji, mwizi, kahaba, mfungwa na kadhalika.

  Hakuna sababu ya kuwachukulia wabunge Kama watu ambao wake affected zaidi ya wengine, wananchi wote wanapigika sana mtaani, wanapigika mpaka wanaichukia CCM, kwa sera zake ambazo zinadhana kwamba Mtu anayepata posho ya 200,000/= kwa siku ana maisha magumu hivyo inabidi aangaliwe kipekee na Yule mkulima anayeshindia alfu kwa siku anasahaulika.

  Maisha ni magumu huku mtaani, ondokeni Dodoma Hotel, tokeni bungeni kwa masaa, tokeni ofisini na kwenye magari yenu muone watu wanavyopigika huku mtaani.
   
 6. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hata kazi yao siijui! Kwa hali hii wabunge wa JMT nao watadai posho zaidi. Inakuwaje tuchangie kuwalipa miposho yote hiyo wabunge wa EALA wakati hakuna wanachokifanya wakati wao wanapambana hadi kufanikisha kuwaondoa mawaziri kwenye uwaziri lakini wanaambulia elfu 70!

  Nina hakika posho za wabunge wa Bunge la JMT zitaongezwa mwezi ujao!
   
 7. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  zipo hotei nyingi tu za tshs 15,000/- kwa siku na wabunge wengi wanazitumia tunawaona! hawa hata wakipewa posho ya laki tisa hawatahama!

   
 8. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Wabunge ni tofauti sana na hao wengine, WAO NI WATUNGA SHERIA! sasa mwenye kutaka sheria mbovu kwa wananchi akiwapa rushwa na kutupitishia sheria mbovu kwa taifa utasema ni sawa na wengine serikalini?


  William.
   
 9. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  wako tisa tu toka tanzania siyo 350+ kama wabunge wa bunge la muungano! halafu mishahara posho zao hazitoki hazina
   
 10. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #10
  May 24, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kaka wewe kila siku ni kustaajabisha umma tu yaani........Hao wabunge wanakuja na kuondoka ila kuna watu wanaishi hapo na wewe unajua hilo as familia yako inaishi kule so maisha hayaishii kupanga Hoteli nzuri tuu

  Watu tungependa kuona haya matabaka ya kitendaji yanapungua sasa........ziko hotel nzuri na salama kwa rate za 35 - 50,000/= hiyo Dodoma Hotel unayoisemea wewe si lazima wakakae pale woooote. Waishi maisha kutokana na uwezo wa nchi kama ambavyo waafanyakazi wengine wanafunga mikanda

  Kwamba eti wapiga kura wanawafuata wabunge wao pale Dodoma.........may be ni kwa sababu hawawaoni huko majimboni.......this is very sad yaani uunganishe hoja hii na posho????? Kweli kaka unaona ni sawa.........waende huko kuwaona wapiga kura wao ili kuepuka adha hii ya kufuatwa bungeni........au wawe na mikutano na wananchi wa majimbo yao wanaoishi Dodoma ili ku-adress mambo yao huko na kupanga jinsi ya kupata maoni ya wapiga kura wao
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  May 24, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 521
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wananchi huwafuata wabunge wao Dodoma????
  Nafikiri ni kwa sababu hawaendi majimboni kwao baada ya kuchaguliwa!!
   
 12. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #12
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Mkuu next time nenda usome historia ya siasa, ni kwamba once kuna hoja tata kwenye taifa ni vigumu sana kuizima, tizama Muungano, tizama katiba, tizama wagombea binafsi,

  - Huwezi zima a valid hoja labda temporary tu, and then itakuja kukuuumiza ina a big way na utakubali in ahrd way, bora kuijadili mapema, yaani sasa hii hoja ni valid na ianatakiwa kujadiliwa tena, kwa sababu haiendi kokote!

  William.
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  May 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hizosehemu 'very dangerous ni zipi?'

  ina maana wakishachaguliwa kuwa wabunge wanakuwa very special wanaogopa wapiga kura wao? Unataka kusema wakati wa kupiga kura wanaweza kujichanganya nao, wakishapata ubunge wanakuwa 'special' kujichanganya nao ni 'hatari kwa usalama' wao?

  Ndo maana miaka 50 yote ya madaraka ya ccm maendeleo majimboni hakuna

  Halafu sehemu kama Simba mbona ni hoteli nzuri na wanajazana pale chungu nzima na hoteli sh 20,000-25,000 wakati hoteli ya 'hadhi ' ipo jirani hawaendi?

  Unataka kusema hawalipwi perdiem? Maana kama wanaliowa perdiem sh 80,000 perday, inawatosha sana tu, sh 65,000 unalipia hoteli sh 15,000 unakula......

  Tatizo sio bei za hoteli, tatizo sio hadhi za hoteli tatizo ni uroho na uchu wa fedha..........
  Kujali matumbo yao binafsi kuliko wapigakura wao.....???

  Au nataka kusema wabunge waliopinga hilo wao hawakai hotelini?
   
 14. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #14
  May 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  unajiandalia mazingira mazuri kuingia bungeni 2015? hao wanaowawakilisha hicho wanachokiona kidogo kwa siku wao hulazimika kutumia pungufu yake kwa mwezi na wako dodoma.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  May 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  William wake up,

  Binadamu wote ni sawa, sio Mimi nayesema hivyo, Katiba yetu inatamka hivyo kutunga sheria tu Ndio kunawafanya wao the best out of the rest? I don't think so.

  Chukulia mfano Wafungwa, wao ni muhimu kwa jamii, kitendo cha wao kuwa isolated na jamii ni social regulator ya Hali ya juu. Hakuna anayemzidi mwingine kwa umuhimu.
   
 16. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #16
  May 24, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  - Unajua itatuchukua muda mrefu sana kwa mataifa masikini kujifunza kutoka kwa wachina, wao kila sheria zao zinajali mazingara yao zaidi kuliko siasa za kimtaifa, nimetoa hoja kutokana na niliyoyaona na ni kawaida yetu sisi waafrika kwa wananchi kuwafuata wabunge Dodoma kwenye kikao kuwaomba misaada!

  - Sasa yes, inapotaka kutatua tatizo la posho za wabunge lazima uliangalie hilo cause ni reality, Wabunge wetu pesa tunazo walipa atleast nusu zinaishia kwenye mikono ya wananchi wa majimbo yao, hiyo ni FACT, lakini mimi naongelea niliyoyaona Dodoma as a reality, sio hadithi za mtaani!

  William.
   
 17. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  Hata hostel zikijengwa, mwisho wa siku watauziana kijanja....
  Waendelee kukaa hotelini......

  Wanataka kutuaminisha maisha magumu, kama magumu mbona mnakimbilia ubunge?
  Si wangeacha?
  Wakatafute wz kuwadanganya....
  Hakuna yenye hoteli nzuri kwa bei rahisi kama dodoma.............
  Kama wanajiona wapo special hawataki kuchangamana na wananchi wajenge hoteli zao hewani...

   
 18. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Mzee W. J. Malecela vipi kuhusu wanaosimamia na kutumia sheria hizo? Hapa naongelea mahakimu,majaji na mapolisi. Hawa unawazungumziaje? Je,hawahitaji hiyo miposho? Je,hawapo katika mazingira ya kupokea rushwa ili wapindishe usimamizi na utekelezaji wa sheria?

  Mzee hapa labda kama una ajenda nyingine,lakini kama ni suala la ugumu wa maisha,hili ni janga la kitaifa. Hakuna cadre iliyo exceptional.
   
 19. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Taja hayo Magazeti au ni yote?

  Halafu ndugu yangu hoja si posho hoja ni mfumuko wa bei na ukali wa maisha kutokana na uchumi kuyumba sasa tukijadili Mbunge kulipwa zaidi vipi kuhusu Mwananchi anayemwakilisha?

  Jambo lingine kama kuna uwezekano embu Kaka jaribu kupunguza matumizi ya 'I mean zinanipa tabu kusoma post zako.

  Nakupongeza pia kwa kujaribu kugombea.
   
 20. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  hebu tupe idadi ya wananchi wanaowafuata wabunge dodoma....kila mbunge anafuatwa na wananchi wangapi kwa siku?
  Maana wabunge wengine huwa wanawalipia wanachama waonauli na hoteli wakienda dodoma kwa 'shughuli'za chama, kwa hiyo sidhani kama wananchi wanawafuata dodoma bila ridhaa ya mbunge.........

  Au unataka kutuaminisha kuwa mwananchi anayeishi huku tandahimba, ambako shilingi 100 ya kununua panadol anakosa, ila anapata shilingi 50,000 za nauli ya kwenda dodoma kumfuata mbunge? (hii hoja haina mashiko wabunge wzjipange upya)

  pia ukiona wananchi wamekufuata bungeni ujue kuwa hufai kuwa mbunge, hufai kuwa kiongozi......ungekua kiongozi bora na si bora kiongozi ungeonana na wananchi wako jimboni na kumaliza matatizo, bungeni ungeenda kuwasilisha hoja tu........................ Ila kwavile wabunge wengi wamepatikana kwa mshahara wa tshirt na kofia hawaonekani majimboni hadi msimu wa bunge.....
   
Loading...