Posho na Mishahara ya wabunge...

Imekuwa ni porojo tu ndani ya bunge juu ya posho za wabunge na viongozi wa serikali na idara zake. Nauliza swali moja : hawa wabunge wanapoomba kura za watu wanakuwa wamelenga kuwatumikia au wapo kwa ajili ya masilahi yao? Kama kweli wanawatumikia wananchi basi wakubali kutolipwa posho ili zisaidie shughuli nyingine zaidi za maendeleo. Jamani pendeni nchi yenu
 
Jamani wana JF- kuna haja ya watumishi wa kada mbalimbali kama Madaktari, Waalimu, Wahasibu, Maainjinia na wengine wote kuanza kudai Posho kama inavyotokea kwa Wabunge wa nchi hii, Daktari akishamaliza kuwahudumia wagonjwa wodini akitoka asaini posho, Mwalimu naye akitoka darasani asaini posho,na makundi mengine yote iwe hivyo, nadhani hapa uwiano utakuwepo maana kitendo cha wabunge kulipwa posho na wakati wanamishahara ni kichefuchefu, harafu wanasema posho haziepukiki eti maisha ni magumu kama kwao maisha ni magumu mwalimu aseme nini? Acheni utahila huyo nyie wakubwa sasa,
 
Huo ndo upeo wa wabunge wetu. Ni aibu kwa kweli. Hivi wewe umegombea ubunge ili ukagawe hela? Uchizi. Well done Zito lakini pia nimefurahi limefanywa na mtu (si chama) ili kutoa fursa kwa wengine kuiga (bila ya kujali chama chake).
 
Ukitaka kujua nani ni mbunge/ waziri/mkuu wa mkoa/wilaya n.k. wa ki-ukweli na nani siye wewe kongoloa posho zote na uwape mishahara tu kulingana na kiwango cha ilimu yao, hapo watabaki akina Mwl. J K Nyerere tu, labda, na wale waliopo kwa ajili ya maslahi ya biashara zao.
Waliowengi wapo kwa posho tu na wachache sana kwa maslahi ya nchi na wananchi!
 
Ukitaka kujua nani ni mbunge/ waziri/mkuu wa mkoa/wilaya n.k. wa ki-ukweli na nani siye wewe kongoloa posho zote na uwape mishahara tu kulingana na kiwango cha ilimu yao, hapo watabaki akina Mwl. J K Nyerere tu, labda, na wale waliopo kwa ajili ya maslahi ya biashara zao.
Waliowengi wapo kwa posho tu na wachache sana kwa maslahi ya nchi na wananchi!

Una maana tutegemee kina Prof. Maghembe, Prof. Mwandosya, Dr Mwakyembe, Prof, Mwakyusa kurudi kuimarisha taaluma katika vyuo vyetu vikuu? Mimi nafikiri hivyo....
 
Hivi lile wazo la kila mtu akiingia bungeni aingie na mshahara wa uraiani limeishia wapi? Yaani kama wewe ni mwalimu by proffession, bungeni unapewa mshahara wa mwalimu, bwana shamba, daktari hivyo hivyo. Kuna haja ya kuliweka hili kwenye katiba.
 
Jamani wana JF- kuna haja ya watumishi wa kada mbalimbali kama Madaktari, Waalimu, Wahasibu, Maainjinia na wengine wote kuanza kudai Posho kama inavyotokea kwa Wabunge wa nchi hii, Daktari akishamaliza kuwahudumia wagonjwa wodini akitoka asaini posho, Mwalimu naye akitoka darasani asaini posho,na makundi mengine yote iwe hivyo, nadhani hapa uwiano utakuwepo maana kitendo cha wabunge kulipwa posho na wakati wanamishahara ni kichefuchefu, harafu wanasema posho haziepukiki eti maisha ni magumu kama kwao maisha ni magumu mwalimu aseme nini? Acheni utahila huyo nyie wakubwa sasa,

Tuombe mishahara iboreshwe tu. Na sio posho.
 
Tuesday, 14 June 2011 21:43


Neville Meena, Dodoma

HOJA ya kutaka kufutwa kwa posho za vikao za wabunge na watumishi wengine wa umma wa imechukua sura mpya baada ya jana Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba kuliambia Bunge mjini hapa kuwa suala la kufutwa kwa posho ni la kitaifa na ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano uliowasilishwa na serikali.

Kauli hiyo yab Makamba ambaye pia ni Katibu wa Mambo ya Nje wa Sekretarieti ya CCM imekuja huku kukiwa na malumbano makali baina ya Spika wa Bunge, Anne Makinda na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kuhusu suala hilo la posho za vikao vya wabunge.

Juzi, Spika Makinda alisema Zitto ambaye ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anaweza kufukuzwa ubunge kwa kutosaini karatasi za mahudhurio, hatua ambayo Zitto alisema ataichukua ili asilipwe posho za vikao.

Spika alisema Zitto anaweza kukumbwa na adhabu hiyo iwapo hatasaini karatasi za mahudhurio ambazo ndizo zinathibitsha uwepo wa mbunge katika mikutano na vikao vya bunge na kwamba kanuni zinamwadhibu mbunge kwa kumfukuza asipohudhuria mikutano mitatu. Hata hivyo, Zitto amepuuza kauli hiyo ya Spika kwa kusema kwamba kama ni kwa ajili ya kukataa posho, yuko tayari kufukuzwa bungeni.

"Nitafanya hivyo tuone, Kanuni inasema mikutano mitatu mfululizo na siyo vikao vitatu mfululizo. Nitatumia uzoefu wangu wa siasa za wanafunzi kukwepa mtego wake. Lakini kama anadhani ni sawa kunifukuza ubunge kwa kukataa posho, nipo tayari," alisema.

Kauli ya jana ya Makamba pia inaonekana kutofautina na mawazo ya wabunge wengi wa CCM akiwamo Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo ambaye amesema wanashabikia suala hilo wanajitafutia umaarufu.

Akichangia huo wa maendeleo wa miaka mitano jana, Makamba alionekana kupigia chapuo suala la kufutwa au kuangaliwa upya kwa posho za vikao huku akisema kwamba ni la kitaifa na ni sehemu ya mpango huo.

Makamba alisema kuwa suala la nidhamu na usimamizi wa matumizi ya fedha za umma ni muhimu na kwamba mpango huo umeliona katika ukurasa wa 17 wa kitabu kilichochapishwa kwa Kiingereza na kutoa mapendekezo ya kufutwa kwa posho za vikao na zile za usafiri.

"Mpango unabainisha kwamba kuna umuhimu wa kufutwa kwa posho za vikao na usafiri hivyo iwapo wabunge mtalisikia likiwasilishwa hapa kwa mbwembwe kesho (leo), basi msije mkashangaa kwani ni sehemu ya mpango huu," alisema Makamba.


Kujadiliwa bungeni leo

Mjadala kuhusu malipo ya posho ambao umekuwa ukiendelea kwa wiki moja sasa hasa zaidi nje ya Bunge, leo unatarajiwa kuingizwa rasmi bungeni wakati Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa na Mkulo Jumatano iliyopita itakapoanza kujadiliwa.

Suala hilo ni dhahiri litajitokeza katika bajeti mbadala itakayowasilishwa na kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe ambaye amekuwa katika mvutano usio rasmi na Spika kutokana na kukataa kulipwa posho za kikao.

Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema jana kuwa kambi yake inatarajiwa kutoa ushauri mgumu ambao haujazoeleka kwa watendaji wa serikali na kwamba suala la kufutwa kwa posho ni sehemu ya mapendekezo hayo.

Alisema kufutwa kwa posho hizo kunaweza kuokoa zaidi ya Sh900 bilioni ambazo zinaweza kuelekezwa katika maeneo mengine ya huduma kwa wananchi.

Uhalisia posho za wabunge

Mmoja wa wabunge wa CCM ambaye hakutaka kutaandikwa jina lake alisema anasikia kuhukumiwa katika nafsi yake kutokana na kupokea posho za vikao ambazo kimsingi ni sawa na "kuwaibia wananchi".

"Ujue bwana sisi ndani ya CCM mambo hayaendi kama kwa wenzetu (Chadema), wale wanaweza kukaa leo na kuamua, sisi ni tofauti lazima kuwepo na mchakato lakini ukweli ni kwamba hoja yao ni nzuri," alisema mbunge huyo.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa malipo ya wabunge yamegawanyika katika sehemu nne ambazo ni pamoja na mshahara ambao ni Sh2,300,000 kwa mwezi, posho ya ubunge kila mwezi ambayo ni Sh5 milioni, posho ya kujikimu (per-diem) Sh80,000 wawapo nje ya majimbo yao kikazi na posho ya vikao (sitting allowance) ambayo huwa ni Sh70,000 kwa kila mbunge.

Kwa maana hiyo, kwa kawaida mbunge hulipwa Sh7.3 milioni kila mwezi kabla ya kukatwa kodi na wawapo Dodoma na Dar es Salaam kwa ajili ya vikao vya kamati na bunge au mikoani kwa ajili ya kukagua shughuli zilizopo chini ya kamati zao. Hulipwa kiasi cha Sh150,000 kila mmoja kwa siku ambazo ni Sh70,000 kwa ajili ya vikao na Sh80,000 kwa ajili ya kujikimu.

Kwa maana hiyo bunge linatarajiwa kutumia kiasi cha Sh1.788 bilioni kwa ajili ya kugharamia vikao 73 vya Bunge la Bajeti iwapo wabunge wote 350 waliopo watahudhuria vikao hivyo.

Kwa hesabu hizo, kila mbunge katika mkutano wa Bunge la Bajeti anatarajiwa kuondoka na kikita cha Sh5.1 milioni mbali na Sh 5.58 milioni ambazo ni malipo kwa ajili ya kujikimu, fedha ambazo ni mbali na mshahara wake kwa mwezi na posho ya ubunge.

CCM yakataa posho
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeanza machakato wa kufuta posho hizo ikiwa ni hatua ya kupunguza matumizi yasiyo ya lazima. Habari kutoka ndani ya CCM, Dodoma na Dar es Salaam zinasema kuwa mkakati wa kufutwa kwa posho ulianzishwa takriban mwezi mmoja uliopita na sekretarieti mpya inayoongozwa na Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, baadhi ya wajumbe wa sekretarieti walihoji uhalali wa posho wanazolipwa hata pale vikao vinapofanyika katika sehemu ambako ni makazi yao na kwamba hoja hizo ndizo zilizozaa wazo la kufutwa kwa posho katika vikao.

"Hoja ilikuwa kwamba kama chama hakina fedha na tunataka kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, basi posho za vikao zifutwe kwa sababu hakuna ulazima wa posho hizo hasa kwa wajumbe wa sekretarieti ambao kazi zao ni za kila siku," kilieleza chanzo chetu na kuongeza:

"Hivi sasa mpango huo uko kwenye mchakato wa kuwekewa mwongozo na nadhani baada ya kupitia katika vikao vyetu utaanza kutekelezwa. Lakini kimsingi ni kama utekelezaji wake umeshaanza kwa sababu baadhi ya wajunbe wamekataa kabisa kusaini posho hizo."

Habari zaidi zinadai kuwa waraka wa mapendekezo ya kupunguza matumizi ndani ya CCM unakwenda mbali zaidi hadi katika matumizi ya magari na kwamba pale usafiri unapohitaji wa kuelekea kwenye mkutano mmoja, basi viongozi watumie magari machache kwa maana ya usafiri wa pamoja badala ya utaratibu wa sasa ambao unamruhusu kila kiongozi kutumia usafiri wake.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu sekretarieti kufuta posho katika vikao vyake, hakukanusha wala kuthibitisha, badala yake akadai kuwa hayo ni mambo ya ndani ya chama ambayo hayana faida yoyote kwa umma.

"Hivi ninyi waandishi wa habari, haya mambo mnayapata kwa nani! Haya ni mambo ya ndani ya chama sidhani kama yana tija yoyote kwa umma, maana haiwezi kusaidia chochote," alisema Nape kwa kwa simu.

Alipoelezwa kwamba suala hilo lina uhusiano na sakata linaloendelea bungeni, Nape alisema: "Bunge ni bunge na chama ni chama. Kila taasisi inajitegemea na ina uamuzi wake, lakini pia sisi kama chama tulishatoa kauli mara nyingi kwamba suala la posho kwa wabunge na watumishi wengine wa serikali linazungumzika, ni la kisera na wanaohusika wapo waulizeni hao."

Mwishoni mwa wiki iliyopita Nape akizungumzia malumbano miongoni mwa wabunge kuhusu suala la posho alisema suala hilo linajadilika na kwamba si vyema kulipinga kwa sababu tu linatokea kambi ya upinzani.

Kwa upande wake, Makamba alipulizwa kuhusu kufutwa kwa posho katika vikao vya Sekretarieti ya CCM naye kama ilivyokuwa kwa Nape, hakukanusha wala kuthibitisha.

"Wewe si unamfahamu msemaji wa chama ni nani? Mwulizeni Nape tena nadhani anakuja Dodoma. Akija mwulizeni, mimi siwezi kulizungumzia.... lakini ninyi waandishi haya mambo ya ndani ya chama huwa mnayapata wapi? Anyway, mwulizeni mwenezi atawaambia," alisema Makamba.



 
mbona ccm inageuka na kuwa kama kidumu cha CHADEMA? kila kitu wasubiri wabunge wa CHADEMA wamesema nini ndiyo wajifanye kutoka na sera!!! aghh
 
Makazi yangu jijini Dar yako chini ya jimbo linaloongozwa na mbunge wa CCM na ofisi zangu ziko katika jimbo linaloongozwa na mbunge wa CHADEMA, toka sakata la posho lichukue sura mpya nimejaribu kuwasiliana nao ili kujua msimamo wao, wote wawili wamesema hawakubaliani na wafanyakazi wa serikali na wabunge kupokea posho, wa CDM amedai kuwa mbali ya yeye kupinga posho hata chama chao kina msimamo huohuo wa kupinga posho, wa CCM amedai anapinga posho kwa asilimia mia moja na si yeye peke yake basi wabunge wengi wa CCM wanapinga posho pia lakini anahofu ya kujitokeza hadharani na kutoa msimamo wake kwa kuwa bado hajajua msimamo wa chama chake, lakini akadai muda simrefu yeye pamoja na wabunge wenzake wataitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma na kutoa msimamo wao juu ya kupinga posho, kwa kuwa fedha hizo zinahitajika katika ujenzi wa taifa letu changa,

Je mbunge wako anamsimamo gani, wasiliana naye na tujulishe msimamo wake.
 
Mkuu kama haya ya kweli nimefurahi sana kwa hatua na ujasiri ulochukua kutaka kujua Mbunge wako amesimama wapi ktk swala hili la Posho. nawaomba Watanzania wazalendo wengine wafanye hivyo hivyo tupate kujua ni wabunge gani wanaopendekeza/kupinga hoja hii ya posho..
 
..sasa kama mpango wa maendeleo wa miaka 5 uliowasilishwa na JK unaelekeza kusitishwa kwa posho, kwanini Spika,Nape,na wabunge wa CCM, wanapinga suala hilohilo pale liliporudiwa na Zitto Kabwe?!!!

..kinachobainika hapa ni kwamba, CCM na serikali yake wamekosa umakini, hawana-coordination, na wamechanganyikiwa. wa-Tanzania we r stuck na uongozi usiojua ufanye nini na dhamana tuliyowakabidhi ya kuongoza taifa hili.
 
Mkuu kama haya ya kweli nimefurahi sana kwa hatua na ujasiri ulochukua kutaka kujua Mbunge wako amesimama wapi ktk swala hili la Posho. nawaomba Watanzania wazalendo wengine wafanye hivyo hivyo tupate kujua ni wabunge gani wanaopendekeza/kupinga hoja hii ya posho..
Mkuu Mkandara heshima mbele sana mkuu.Hili swala ni kubwa kuliko vyama vya siasa na misimamo yake, hili ni jambo la kitaifa kimaslahi na mustakabali wake, haiitaji ujasili kujua msimamo wa mbunge wako, no matter where you at, wasiliana naye kujua msimamo wake, ili tujue kama wako ki maslahi binafsi au ya taifa letu.
 
Mzee wa Gamba,

Hongera kwa kazi nzuri, naona taratibu mnavua magamba na kurudi kundini.

Niko mbali kidogo lakini ninampigia mbunge wangu ambaye ni wa chama gamba sasa hivi kupata msimamo wake.
 

Mkuu Kimbunga...Mshahara kwa mawazo yangu madogo ni given na unatumika kama security, hivyo mwajiri anaweza kumkopesha mwajiriwa alafu akamkata kwa mshahara wake...Ila inategemea na makubariano yenu...Mwaka 2007 nilikuwa nafanya kazi kampuni moja na nikafiwa na mama yangu mzazi hapa Dar na tulitakiwa kuusafirisha mwili wake kwa maziko huko Musoma. Nilienda kwa mwajili wangu na kukopa mshahara wangu wa miezi miwili hivyo katika makubariano yetu ni kuwa nitalipa deni hilo kupitia mishara yangu itakayofuata. So kwa muda wa miezi miwili sikupata mashahara coz pesa yote iliishia kulipa mkopo...Ila si unajua mambo ya mjini, niliishi hivyo na hatimaye nikamaliza deni...Unajua wakati mwingine ukiwa na shida kama ugonjwa na msiba, unawezajikuta unakubali tu mashart ya namna hiyo hata kama yanaumiza...Yangu ni hayo mkuu...

Ahsante mkuu kwa ilimu yako. Kumbe mkuu na wewe kuna wakati unaishi kimjini mjini!!
 
Wewe acha porojo mnataka tu kugawana pesa zetu (Ruzuku) maandamano sababu ya posho tu mbona wabunge wenu wamechukuwa milioni 90 juzi mbona mlikuwa kimya sisi wananchi tunawashangaa sana
Hivi na wewe unajihesabu kama mwananchi?
 
Back
Top Bottom