Mishahara, posho na mafao ya wabunge yanapangwa na chombo gani?

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Wadau Nawasalimu.

Naomba kufahamishwa yafuatao kwa mwenye Uelewa Mpana juu ya BUNGE

1.Ni Chombo Gani KISHERIA kinachopanga Mishahara Posho na Mafao ya WABUNGE?

2.Kwanini Mishahara Posho na Mafao ya Wabunge ni Makubwa kuliko ya Mihimili Mingine?

3.Kwanini MIHIMILI 3 itofautiane Mishahara Posho na Mafao wakati Mihimili yote inatumia KODI na Mihimili yote inawatumikia Wananchi?

4.Kwanini Wabunge Mafao yao ni Makubwa licha ya kutumikia Bunge kwa Miaka 5 tofauti na Watumishi wa Mihimili mingine waliokaa kazini kwa Miaka zaidi ya 20?
 
Wadau Nawasalimu.Naomba kufahamishwa yafuatao kwa mwenye Uelewa Mpana juu ya BUNGE
1.Ni Chombo Gani KISHERIA kinachopanga Mishahara Posho na Mafao ya WABUNGE
2.Kwanini Mishahara Posho na Mafao ya Wabunge ni Makubwa kuliko ya Mihimili Mingine?
3.Kwanini MIHIMILI 3 itofautiane Mishahara Posho na Mafao wakati Mihimili yote inatumia KODI na Mihimili yote inawatumikia Wananchi?
4.Kwanini Wabunge Mafao yao ni Makubwa licha ya kutumikia Bunge kwa Miaka 5 tofauti na Watumishi wa Mihimili mingine waliokaa kazini kwa Miaka zaidi ya 20?
Hawa wanajipangia kupitia kamati zao za budget na Rais kazi yake kubwa ni kubariki tu maamuzi yao ili naye akipeleka miswada mibovu bungeni bunge kazi yake ni kupiga mhuri tu
 
Wanaokula nchi ni wabunge na mawaziri wenyewe wanajipangia mishahara yaani nchi inaliwa na watu 400 huku watu milioni 70 wakihangaika kulipa Kodi wafanyakazi gomeni haraka iwezekanavyo
 
1.Ni Chombo Gani KISHERIA kinachopanga Mishahara Posho na Mafao ya WABUNGE
Bunge
2.Kwanini Mishahara Posho na Mafao ya Wabunge ni Makubwa kuliko ya Mihimili Mingine?
Sio mikubwa kuliko mihimili mingine. Unachokosea ni kudhani kwamba mbunge ni sawa na mwalimu au nesi kwenye serikali kuu. Mbunge ni kiongozi. Kwenye mihimili mingine nako viongozi wanalipwa pesa nyingi na wana marupurupu mengi wengine kuliko hata wabunge.
3.Kwanini MIHIMILI 3 itofautiane Mishahara Posho na Mafao wakati Mihimili yote inatumia KODI na Mihimili yote inawatumikia Wananchi?
Rejea jibu namba 2.
4.Kwanini Wabunge Mafao yao ni Makubwa licha ya kutumikia Bunge kwa Miaka 5 tofauti na Watumishi wa Mihimili mingine waliokaa kazini kwa Miaka zaidi ya 20?
Wabunge ni viongozi, sio watumishi. Wabunge sio waajiriwa. Watumishi ni waajiriwa.
 
Bunge

Sio mikubwa kuliko mihimili mingine. Unachokosea ni kudhani kwamba mbunge ni sawa na mwalimu au nesi kwenye serikali kuu. Mbunge ni kiongozi. Kwenye mihimili mingine nako viongozi wanalipwa pesa nyingi na wana marupurupu mengi wengine kuliko hata wabunge.

Rejea jibu namba 2.

Wabunge ni viongozi, sio watumishi. Wabunge sio waajiriwa. Watumishi ni waajiriwa.
Namba 3 hujajibu mkuu
 
Sasahivi watalipwa perdiem 250,000 + 350,000 posho ya kikao kwa siku = 600,000 x 60 = 36,000,000 bunge la budget nje na mishahara miwili 2 = 24,000,000 bado rushwa 60,000,000 then vijana mnaambiwa mjiajiri
 
1. Kwa mujibu wa sheria No 2 ya 1999 bunge lazima liongeze pensheni ya rais mstaafu kila baada ya miaka 5.

Maana yake ni kwamba;

2. Kwa mujibu wa ibara ya 73 ya Katiba ya JMT 1977 wabunge hujiongzea mishahara wenyewe kupitia sheria wanayotunga kinapowadia kipindi husika. Ambacho kinatajwa ktk sheria no 2 hapo juu, yaani lini na vipi mshahara wa mbunge utaongezwa.

3. Kwakuwa pansheni ya rais mstaafu kwa mujibu wa sheria No 2 ni 80% ya mshahara wa rais aliyepo madarakani.

4. Kwa mujibu wa sheria No 2 lazima bunge liongeze pensheni ya rais mstaafu kila baada ya miaka 5, na ili pensheni ya pensioner president iongezeke; salary ya sitting president lazima kwanza iongezeke!

4. Kwa mujibu wa Katiba ya JMT 1977, rais ni sehemu ya bunge.

5. Kwakuwa bunge na rais ni kitu kimoja mshahara wa rais ukiongezwa na mishahara ya spika, naibu wake, W. Mkuu, mawaziri na wabunge inaongezwa.

6. Kwahiyo ni Rais J K Nyerere aliyetunga ibara ya 73 ya Katiba ya JMT 1977 kuruhusu wabunge hujiongzea mishahara. Hlafu

7. Kupitia ibara ya 73 ya Katiba Bunge la Mkapa ndilo lilitunga muswada wa sheria No 2 ya 1999, Mkapa akausaini kuwa sheria! Huo ndiyo mrija unaotumiwa na bunge au (system) kufyonza kodi za wananchi!
 
Namba 3 hujajibu mkuu
Swali lako lina matatizo maana linapandikiza dhana ya kwamba mishahara ni lazima iwe sawa.

Sasa sijui hiyo dhana umeitoa wapi? Kusema kwamba zote ni pesa za kodi ndo mishahara iwe sawa hiyo sio kweli.

Unachoweza kuhoji kwa mfano ni je mishahara ya Spika, Rais na Jaji Kiongozi iko sawa? Maana hawa ndo watu pekee ambao wako sawa na wako katika mihimili tofauti.

Kuhusu usawa wa watu walio chini yao huo huwezi kuupima.
 
Bunge

Sio mikubwa kuliko mihimili mingine. Unachokosea ni kudhani kwamba mbunge ni sawa na mwalimu au nesi kwenye serikali kuu. Mbunge ni kiongozi. Kwenye mihimili mingine nako viongozi wanalipwa pesa nyingi na wana marupurupu mengi wengine kuliko hata wabunge.

Rejea jibu namba 2.

Wabunge ni viongozi, sio watumishi. Wabunge sio waajiriwa. Watumishi ni waajiriwa.

Hayo majizi ya kura ndio unatoa hizi sifa kuhalalisha wao kulipwa fedha nyingi?
 
Back
Top Bottom