Posho na Mishahara ya wabunge...

Mmmh! ama kweli kuna kazi kwa CCM kujivua Gamba. Nilikuwa nasikiliza Clouds Radio sasa hivi na nikasikia mahojiano kati ya Mtangazaji wa Clouds na Naibu Katibu Mkuu wa CCM JOhn (Tukokati) Chiligati kuhusiana na Kauli ya Zitto Kabwe juu ya kuondoa posho mbalimbali zikiwemo za vikao vya wabunge wanapokuwa Bungeni.

Sikuamini masikio yangu Chiligati aliposema kuwa anakubaliana na Zitto juu ya kauli hiyo, ila anashauri utekelezaji wake usianze mara moja kwa wabunge wote.

Anapendekeza kuwa utekelezaji wake uanze kwa wabunge wa CHADEMA, mpango huo ukifanikiwa ndipo na wabunge wengine watafuata.

Alipohojiwa kwanini wasianze wabunge wote kama kweli anakubaliana na Zitto, jibu lake likawa ni kwa sababu shida za wabunge zinatofautiana, na kwa wabunge wengi kama yeye wanatumia pesa hizo kuwasaidia wapiga kura wao kila wanapotembelea majimbo yao.

My take: JE PESA ZILIZOTENGWA ZA MFUKO WA JIMBO ZINAFANYA KAZI GANI NDUGU CHILIGATI??????:
 
shida walizonazo si kulipa madeni za pesa walizokopa ili kununua ubunge, so ni wazi wanajua kuwa wabunge wa CDM hawajununua ubunge so pesa ya kulipa madeni hawaihitaji. Jamani posho za wabunge ndo za kusaidia wananchi kweli na hela za mfuko wa jimbo wanafanyia nini? au wanahonga mademu zao
 
Ni kweli shida zinatoutiana sana, ni kama kufikiria masuala na maslahi ya umma wa kitanzania na taifa kwa kutumuia tumbo na kichwa, kina Chiligati wanafikiria maslahi ya umma wa tz kwa kutumia matumbo yao ilhali kina Zitto wanatumia vichwa vyao kuhakikisha umma unafaidika na rasilimali zilizopo:glasses-nerdy:
 
Nani kamwambia wananchi tunataka kusaidiwa na fedha za wabunge ?!!
Tunachohitaji ni kuona tunajisaidia kwa kutumia kodi zetu.kwa hiyo kazi ya mbunge sio uwakilishi tena,badala yake ni kuwa wahisani!!poor chiligaati.

Jk tunaomba semina elekezi kwa mps!
 
Na mimi nilikuwa nawasikiliza Clouds muda huo pia, na nimeshangaa sana what I heard. Kuna kipindi nilimsikia Mh Mdee wa Kawe kwenye redio ya East Africa na ilikua mida ya saa nne hv asb ila sikumbuki kipindi kilikua kinaitwaje, but alielezea vizuri sana jinsi wananchi wanavyosaidiwa na mfuko wa jimbo na alieleza mengi sana.

Sasa huyo gamba, aliposema eti hela za posho ndizo anazotumia kuwasaidia wananchi, kweli hapa kazi ipo, na kama mlivyosema, za jimbo wanazopewa anafanyia kazi gani?
 
Mhhh ama kweli kuna kazi kwa CCM kulivua Gamba. NIlikuwa nasikiliza Clouds Radio sasa hivi na nikasikia mahojiano kati ya Mtangazaji wa Clouds na Naibu Katibu Mkuu wa CCM JOhn (Tukokati) Chiligati kuhusiana na Kauli ya Zitto Kabwe juu ya kuondoa posho mbalimbali zikiwemo za vikao vya wabunge wanapokuwa bungeni. Sikuamini masikio yangu Chiligati aliposema kuwa anakubaliana na Zitto juu ya kauli hiyo, ila anashauri utekelezaji wake usianze mara moja kwa wabunge wote. Anapendekeza kuwa utekelezaji wake uanze kwa wabunge wa CHADEMA, mpango huo ukifanikiwa ndipo na wabunge wengine watafuata.

Alipohojiwa kwanini wasianze wabunge wote kama kweli anakubaliana na Zitto??
Jibu lake likawa ni kwa sababu shida za wabunge zinatofautiana, na kwa wabunge wengi kama yeye wanatumia pesa hizo kuwasaidia wapiga kura wao kila wanapotembelea majimbo yao.

My take: JE PESA ZILIZOTENGWA ZA MFUKO WA JIMBO ZINAFANYA KAZI GANI NDUGU CHILIGATI??????:

Katika mazingira haya haupaswi kuumiza kichwa kuwa anayoyasema Nape kuwa ccm inarudia misingi yake ya kujari wanyonge ni uzushi mtupu,zingatia kauli ya Chiligati na nafac yake katika Chama.
 
Mhhh ama kweli kuna kazi kwa CCM kulivua Gamba. NIlikuwa nasikiliza Clouds Radio sasa hivi na nikasikia mahojiano kati ya Mtangazaji wa Clouds na Naibu Katibu Mkuu wa CCM JOhn (Tukokati) Chiligati kuhusiana na Kauli ya Zitto Kabwe juu ya kuondoa posho mbalimbali zikiwemo za vikao vya wabunge wanapokuwa bungeni. Sikuamini masikio yangu Chiligati aliposema kuwa anakubaliana na Zitto juu ya kauli hiyo, ila anashauri utekelezaji wake usianze mara moja kwa wabunge wote. Anapendekeza kuwa utekelezaji wake uanze kwa wabunge wa CHADEMA, mpango huo ukifanikiwa ndipo na wabunge wengine watafuata.

Alipohojiwa kwanini wasianze wabunge wote kama kweli anakubaliana na Zitto??
Jibu lake likawa ni kwa sababu shida za wabunge zinatofautiana, na kwa wabunge wengi kama yeye wanatumia pesa hizo kuwasaidia wapiga kura wao kila wanapotembelea majimbo yao.

My take: JE PESA ZILIZOTENGWA ZA MFUKO WA JIMBO ZINAFANYA KAZI GANI NDUGU CHILIGATI??????:

Dah!pumba nyingine hii kutoka big potato!jamani hii nchi imekosa heshima kabisa!Chiligati kama huwezi kuongea na media bora ungetumia neno lenu lile la "no comment" ili kutokuonesha namna gani usivyojali maneno yatokayo kinywani mwako!In short umeniboa kama kweli umetamka hayo.Na kama ndivyo wewe ni gamba pia!
 
uzoefu wangu katika hiyo fedha ni kwamba:-
Huko vijini wabunge wa CCM hutoa madebe ya pombe kwa vijiji. debe moja la pombe za kienyeji ni shilingi elfu mbili. hilo debe wanakunywa watu wasiopungua sitini na kulewa kwa hivo kanunua madebe matano kijiji kizima wanakunywa na kulewa chakali. hali hiyo inampa ummarufu maana katumia shilingi 8000/= kutoa burudani kwa kijiji kizima. Kama Jimbo lina vijiji mbili maana yake atahitaji shilingi milioni moja na laki sita kuburudisha jimbo zima.
Tell me GUYZ why should Chiligati and others from similar constituents deny that mighty CASH to help them become visible GODS?
 
Mbona sababu aliyoisema haija kaa vizuri,
kama posho anaitumia kuwapa wapiga kura wake sisi hatujui na hatuna uhakika katika hilo pia sioni kama ni mbaya kama posho hizo zitasitishwa kwa sababu bado zitatumika kuwasaidia wapiga kura wakati yeye akiendelea kutumia mfuko wa jimbo kuwasaidia wapiga kura.
hakuna lolote Fisadi tuuu
 
Ni bora kunyamaza kuliko kuongea,mtu mzima na ndevu zake anaweza kuheshimika kwa muonekano wake lakini akifumbua kinywa anajulikana true Coluors..
Japo sijasikia hayo mahojiano lakini ni aibu kwa kiongozi mkubwa katika chama kuongea hayo.Je ni wapi tunaenda kama hawa wazee wanaongea hizi tamaa zao hadharani?
Je uongozi ni posho za vikao Ama ni chanzo cha mapato binafsi? Kwa nini mfano usianze kwa baba(ccm waliopo madarakani) na kuigwa na wengine?..na hawa jamaa wa Clouds naona wamechukua nafasi ya Radio uhuru,no entertainments any more!
 
Kazi ya bunge sio kugawa pesa za posho kwenye majimbo yao. Wabunge are LEGISLATURES, meaning wanatunga sheria na kusimamia utendeji wa serikali, full stop. Siku hizi kumeibuka kasumba ya wabunge kuomba omba, kila kukicha wako kwenye balozi za nchi za nje hapa Tanzania pamoja na mashirika ya kimataifa wakiomba vitu vidogo vidogo. Yes, ni vizuri kwa wabunge kutafuta misaada lakini ni kweli serikali haiwezi kutatua haya matatizo bila omba omba ya wabunge?

Tuchukulie kwa mfano, kama wabunge bila kujali chama wangesimama imara na wakaiwajibisha serikali leo tusingekuwa na EPA, Richmond, IPTL, TICS etc. Wabunge wanaomba msaada wa USD 10 million (kwa mfano) wakati EPA ni USD 90 na ushee!!!! ndio maana wafadhali wanatudharau maan wanaona kabisa tunaacha hela zinaenda mifukoni mwa wachache lakini tunawasumbua na vibakuli kila kukicha.

Sasa kisingizio cha Chilligati kuwa wabunge wa CCM wanatumia posho kuwasaidia wananchi, hiyo siyo primary role yao wao wabunge. Kusaidia wananchi sio kutuleta pombe, kanga, mipira na t-shirt. ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi na serikali inatimiza wajibu wake. Maadam hilo wameshindwa sasa tunataka posho zikome. kabisa. Chilligati na wenzake watafute vianzo vingine vya kuwahonga wanachi pombe na t-shirt. Nasema posho mwisho.
 
Chiligati hana ubongo wa Mbele jamani anatumia utumbo na tumbo kufikiri, msishangae hayo majibu yanatoka tumboni kwake na sio kichwani.wazee hawa wa CCM wanazeeka vibaya sana hata 1 + 1 = 11 tunaelekea wapi na hawa magamba?
 
Ama kweli kazi ipo kama ndo kiongozi mkuu wa chama anafikiri kwa kutumia tumbo na nyuchi za mademu zao then gamba haliwezi kutoka labda ngozi kabisa. Sidhani kama ametumia hata 1/10 ya ubongo wake kuwa jambo hlo likipitishwa litakuwa na madhara yepi kwa chama chake anachokiongoza.
 
Wanatumiaga kuwahonga mademu wao
Kwa hili, there is a disconnect, to be sure, and a dysfunctional situation kwenye strategy ya kuvua magamba. Sijui kama kweli Chiligati anajua wapi tuendapo miaka kumi ijayo zaidi ya kutaka kushiba na ku-puke yeye na chama chake cha magamba!
 
WTF.................mupuuzi mwingine unanifanya nitake kufnya kitu kibaya sana!!!
Nina hasira asee!!
 
Back
Top Bottom