MWENYEKITI wa Chama cha UPDP, Faham Dovutwa, anajiandaa kupinga alichokiita ubadhirifu na ufisadi wa kitaasisi, unaofanywa na Bunge kwa kulipa posho za kujikimu kwa wabunge wanapokuwa katika vikao vyao mjini Dodoma.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake jana, Dovutwa alisema utaratibu wa kuwalipa posho za kujikimu wabunge wanapokuwa mjini Dodoma, ni makosa na ubadhirifu wa fedha za walipa kodi.Alisema wabunge hawastahili kulipwa fedha hizo kwa sababu wanalipwa mishara yao kwa kazi hiyo.
"Wabunge wanalipwa mishahara ya kila mwezi kama watumishi wa eneo lolote na miongoni mwa kazi zao ni wanazifanyia mjini Dodoma, sasa inashangaza wanapolipwa posho za siku huku wakiwa wanalipwa mishahara yao," alisema Dovutwa.
Dovutwa alisema kwa kawaida posho ya kujikimu inalipwa kwa mtumishi anapokwenda nje ya kituo chake cha kazi na kwamba kitendo cha kuwalipa posho wabunge wanapokuwa mjini Dodoma ni cha ubadhirifu.
Alisema Dodoma ndiyo kituo cha kazi za wabunge na kwa hiyo hakuna sababu ya kuwalipa posho ya kujikimu.
Alisema anakusudia kutafuta usahihi wa jambo hilo kabla ya kuamua kuchukua hatua za kisheria."Hoja yangu ni viongozi wetu tuliowapa dhamana ya kuongoza taasisi na idara za umma, kuhusika katika hujuma za ubadhirifu na ufisadi huo, maana wakati mwingine inakuwa vigumu kuhoji kutokana na kuwa tuhuma zenyewe zinafanyika baada ya kubarikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni," alisisitiza. [/COLOR]
Kumbe hapo ndipo ilipotoka????