Wako wapi wale Pro-Chadema walikuwa wanapinga eti hakuna benki inayoweza kutoa mikopo kupitia posho, LAT na wenzako mpooo???
[ mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.]
.
Sioni sababu ya kuwashinikiza wabunge wa Chadema wasichukue posho hiyo kabla haijaondolewa, kinachopiganiwa posho hiyo iondolewe si kwa wabunge tu ila watumishi wote wa umma, kwa nini mnakomalia tu wabunge wa chadema wasichukue? Hamna uchungu na nji hii, duh!
Siasa za kipuuzi kabisa. Hakuna mikopo kwa kutegemea posho za vikao maana mbunge hulipwa posho baada ya kuhudhuria kikao. Mkopo unatokana na mshahara na posho ya Ubunge ambayo inafikia tshs 5m kwa ajili ya mafuta 2m, kuendesha ofisi nk. Pia mshahara 2.3m! Hakuna mbunge anayeruhusiwa kukopa kwa kutumia posho za kujikimu au za vikao. Hizi ni propaganda za kitoto na zisizo na maana yeyote ambazo wala haziwezi kuzuia uzito wa hoja ya kufuta allowances za vikao.
CRDB nao ni wajinga tu kutoa taarifa kwa serikali au dailynews. Hata hivyo sishangai hata kidogo kwani crdb ndio benki iliyotumika kupitisha fedha za epa zaidi ya benki yeyote. Pia ndio benki inayoongoza kwenye wizi wa fedha za stimulus package.
Mwongo mkubwa.
Yeye mwenyewe Mnyika kasema "...Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja... " Hela wanaingiziwa moja kwa moja kwenye akaunti, hakuna aliyeirudisha!
You see, uzuri wa John Mnyika hasemi semi uongo most of the time. Mnyika kafananisha posho na nyama tamu, na kuacha posho kasema ni kama kumsusia fisi bucha yako ya nyama.
"Kabla ya kubadilishwa kwa mfumo mzima wa posho si jambo lenye maslahi ya umma kuziachia posho hizo zikatumiwa kiubadhirifu na serikali inayoongozwa na CCM badala yake ni lazima kuweka mazingira ya kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwenye masuala ya kimaendeleo kinyume na hapo itakuwa ni sawa sawa na ‘kumsusia fisi bucha.'' Chanzo
Kwa hiyo Mnyika hakatai kwamba huwa anakula posho, mikopo, mishahara, hela za mashangingi, wewe taja. Simtengenezi haya mambo, namnukuu:
"Nilichukua pia msimamo kama huo kwenye suala la mikopo ya magari ya wabunge, wakati wa kampeni nilipinga kiwango cha mikopo kinachotolewa cha milioni 90 kwa ajili ya gari kuwa ni kikubwa; na baada ya kuchaguliwa nilipewa mkopo huo na kuupokea." Chanzo
Hahahahahahaha....... Siasa za Tanzania na viongozi wetu zinatia udhia na machungu kupindukia lakini kwa sababu watu wazima haturuhusiwi kulia unaishia kucheka. John Mnyika, among the best and the brightest in the annals of our political leadership anakwambia ana msimamo mkali wa kupinga mikopo ya mashangingi lakini ukimpa atakula!
Siasa za kipuuzi kabisa. Hakuna mikopo kwa kutegemea posho za vikao maana mbunge hulipwa posho baada ya kuhudhuria kikao. Mkopo unatokana na mshahara na posho ya Ubunge ambayo inafikia tshs 5m kwa ajili ya mafuta 2m, kuendesha ofisi nk. Pia mshahara 2.3m! Hakuna mbunge anayeruhusiwa kukopa kwa kutumia posho za kujikimu au za vikao. Hizi ni propaganda za kitoto na zisizo na maana yeyote ambazo wala haziwezi kuzuia uzito wa hoja ya kufuta allowances za vikao.
CRDB nao ni wajinga tu kutoa taarifa kwa serikali au dailynews. Hata hivyo sishangai hata kidogo kwani crdb ndio benki iliyotumika kupitisha fedha za epa zaidi ya benki yeyote. Pia ndio benki inayoongoza kwenye wizi wa fedha za stimulus package.
Hatupingi posho kwa sbbu cdm wanapinga na hatutaunga mkono posho kwa sbbu cdm wanaziunga, POSHO ZIONDOLEWEEEEEE! Hata ccm wakiamua kusimamia hilo tutawaunga mkono.Nyie Pro-Chadema msiwe kama makinda ya bata yanamfata mama yao ata popote anapokwenda kama anavuka barabara. Hawo viongozi wenu wameishachukuwa mikopo benki kupitia hizo posho wanazozisema tena wa kwanza kuchukuwa ni Mbowe 200 milioni Zitto 150 milioni, mdhamini wao ni ofisi ya katibu wa bunge
Suala si kuteka hoja bali ni uhalali wa hizo posho. posho za vikao (sitting allowance) ni wizi, narudia tena ni wizi. hata kama zimeainishwa kwenye sheria... aidha naomba niambiwe ni sheria gani imehalalisha sitting allowance. narudia tena, tunaomba tufahamishwe sheria gani inahalalisha sitting allowance. kipengele cha katiba (No. 73) alichotumia Pinda kujibu hoja kipo general kinataja posho, hakitaji sitting allowance. kwa hiyo wahusika waepuke majibu rahisi, watuambie WAPI WAMEANDIKA SITTING ALLOWANCE KWENYE SHERIA. hata kama ipo ni wizi kwa sababu wahusika wanalipwa mshahara kwa ajili ya kazi hiyo.Wanabodi,
Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.
Zitto, Wewe kweli umechukuwa mkopo benki na ofisi ya katibu wa bunge ndio mdhamini wako? Tunaomba utuweke sawa kwenye hili swalaSiasa za kipuuzi kabisa. Hakuna mikopo kwa kutegemea posho za vikao maana mbunge hulipwa posho baada ya kuhudhuria kikao. Mkopo unatokana na mshahara na posho ya Ubunge ambayo inafikia tshs 5m kwa ajili ya mafuta 2m, kuendesha ofisi nk. Pia mshahara 2.3m! Hakuna mbunge anayeruhusiwa kukopa kwa kutumia posho za kujikimu au za vikao. Hizi ni propaganda za kitoto na zisizo na maana yeyote ambazo wala haziwezi kuzuia uzito wa hoja ya kufuta allowances za vikao.CRDB nao ni wajinga tu kutoa taarifa kwa serikali au dailynews. Hata hivyo sishangai hata kidogo kwani crdb ndio benki iliyotumika kupitisha fedha za epa zaidi ya benki yeyote. Pia ndio benki inayoongoza kwenye wizi wa fedha za stimulus package.
Kama kweli CDM wameiba hii hoja toka ccm basi nawapongeza sana, tena sana na ningeshauri wapitie kwa umakini viji-kabrasha vya ccm na watakapobaini hoja nzuri zenye maslahi mazito kwa taifa basi wazibe - zoooote kabisa. Siku zote ccm wamekuwa wanatundanganya kwa speeches zenye maneno kama 'serikali ina mpango kabambe' mara serikali imedhamiria kuondoa kero' n.k baada ya speech hakuna chochote, makaratasi yanaishia kabatini. Only now, for the first time in the history of this country tunapata wanasiasa wanaosimamia kile wanachosema. Kwa nini basi tusiwaunge mkono wanachama wa aina hiyo? ccm your time is up- mmefilisi hili taifa kwa nidhamu ya woga na mufilisi wa maadili.
Wanabodi,
Mjadala wa Posho za Wabunge, umerindima kwenye kipindi cha Baragumu ambacho kiko live Channel Ten wakati huu ninapoandika post hii. Mgeni mwalika ni Katibu Uenezi wa CCM, Nape Mnauye na mchokoza mada ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyechokoza mada kwa njia ya simu.
Mtoa hoja ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amefafanua vizuri sana msimamo wa Chadema na kujielekeza suala la posho za Wabunge, ni suala mtambuka zaidi ya posho za wabunge pekee bali ni posho za watumishi wote wa umma kwa ujumla wao, zikikatwa zitaokoa zaidi ya Shilingi Bilioni 900. Mhe. Mbowe, amekwenda mbali zaidi na kufafanua kwa nini Chadema inapigania kufutwa kwa posho hizo na sio kila posho lazima ifutwe, posho kama za kujikimu ni posho muhimu hivyo Mbowe amesema hana tatizo nazo.
Pia Mheshimiwa Mbowe ameweka bayana suala la posho lisionekana ni la Wabunge wa Chadema tuu, linapaswa kuwa ni suala la bunge lote kwa sababu linahusu maslahi ya taifa. Mbowe akasisitiza ukiweka maslahi ya taifa mbele badala ya maslahi binafsi.
Ilipofika zamu ya Nape, aliunga mkono hoja ya Mbowe kuwa kuna posho za lazima na zile ambazo sio za lazima. Amekubaliana na Mbowe kuwa posho ya kujikimu ni posho ya lazima, hivyo iendelee kuwepo. Mhe. Nape, amekwenda mbali zaidi kwa kueleza dhamira yake ya dhati kupunguza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho. Amekiri wafaidika wa posho ndio wale wale wenye mishahara minono na marupurupu kibao. Amesisitiza hoja siyo ya Chadema, hoja iko kwenye ule mpango wa miaka 5. Amesema unaungana na hoja za kufutwa kwa posho ambazo sio za lazima, ila kwa vile posho hizo zipo kisheria, basi kuondolewa kwa posho hizo kufuate utaratibu.
Miongoni mwa wachangiaji kwa simu ni Mhe. Zarina Madabida, aliiweka wazi kuwa suala la posho liko kwenye hotuba ya bajeti. Naye alitetea msimamo wa kuwepo kwa posho muhimu na kutolea mfano posho za madakitari na uwepo wa per diem. Huyu mbunge Mama Madabida, aliwashutumu wabunge wa upinzani kwa kuuiba hoja ya posho baada ya kuikuta kwenye kamati, hivyo kuiteka hoja.
MY TAKE.
Mbowe amejieleza vizuri sana kwenye hili suala la posho. Nape pia is good, anasimamia maslahi ya taifa.