Posho na Mishahara ya wabunge...

Nyie watanzania wenzangu ukweli nisawa na jua haufichwi ukafichika. Hoja ya CHADEMA niyamsingi sana kwa maslahi ya taifa letu, najua kunawatanzania wanaweza kulipwa au kuwalipa watu ili kupotosha msingi wa hoja hii ya posho. Mimi nawashauri kabla ya kuifanya kaz hiyo wafirie juu ya hatma ya taifa letu na vizaz vijavyo, kurundika pesa kwa wanasiasa, watawala na kuwanyima civil servant, kutumia vyombo vya dola kuwatishia na kuwajeruhi. JE UMMA UTAVUMILIA MPAKA LINI HALI HII? Tunaumia jamani.
 
kujiuzulu sio suluhisho.suluhisho ni bunge kukaa na kufuta sheria hiyo inayoruhusu kupokea posho.waziri mkuu kazi yake anasimamia sheria zilizopo na zitto ndio kazi yake pia.hivyo wakwanza kujiuzulu inabidi awe ni zitto kwa kutosimamia sheria zilizotungwa na bunge.au auambie umma wa watanzania kuwa alikuwa anatafuta umaarufu wa kijinga.
 
CHADEMA Kama kweli wana dhamira ya kweli wakatae kusaini ili wafukuzwe na Watanzania tutaliona hilo lakini hili la matamko yasiyofuatana na matendo mimi naona ni ulaghai mtupu. !

Exactly...!!

Ni jambo la ajabu sana kuilalamikia posho unayoendelea kuichukua, huu ni unafiki ulioifikisha nchii hii hapa ilipo na ndio maana akina Pinda wanapata mlango wa kulipuuza hili kwa sababu hii move inaonekana kujaa blah blah pasi umoja wenye nia ya dhati ya kubeba gharama zake, ni vyema sasa wanasiasa waanze kuongea yale wanayoweza kuyatenda au la wakae kimya...
 
huyo pinda nae si ndo wale wale si alisema hajui kwa nini watanzania ni maskini kwa kuwa yeye anapokea posho nyingi,akiwa kama waziri mkuu hajui tutegemeee nini?hii nchi inaelekea ukingoni very soon kitanuka
 

Nadhani hujaelewa somo! Hoja ni kwamba, kama ulifuatilia vizuri bunge wakati J.makamba anachangia hotuba juu ya mpango wa serikali wa miaka mitano, alisema hivi, hoja ya posho sio hoja ya chadema, ni sera ya serikali, ambayo imo kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ambao umepitishwa na mawaziri na kusainiwa na rais, na mpango huo unaeleza wazi kwamba, posho zitaangaliwa upya ama kuondondolewa kabisa kwa kuwa ni mzigo kwa serikali.
Pinda kama waziri mkuu ndiye msimamizi wa mambo haya, leo anageuka sera za serikali na kusema posho haziwezi ondolewa! Hapa ndipo zitto anahoji, huyu waziri mkuu kama haamini anayosimamia aachie kiti hicho, kwani anapigana na sera anazozisimamia
 
Tatizo viongozi wengi Tanzania wamejilimbikiza mali kiasi kwamba hawatambui kuwa Tzania ni masikini. Kama wanakula Tsh.12m kwa mwezi, watatambua vipi kuwa kuna watu wanaishi kwa Tsh. 50,000 kwa mwezi. Mpaka hapo viongozi wetu watakapo tambua kuwa nchi yetu ni masikini, watu wengi wataumia sana
 
Jambo moja ni kwamba Pinda hajawahi kuwa msafi na hana record ya kutenda . Kama kuna ubuishi niwekeni sawa hapa . Ndiyo maana sishangai matamshi yake na kejeli kwamba hizo ni pesa ndogo . Huyu ni mtoto wa Mkulima . Ni aibu kwamba ni mkatoliki mwenzangu na mseminary mwenzangu pia .Aibu mno .
 
Gezeti la Daily News linatumika kueneza cheap propaganda! Point si wabunge walipokea na walitumia kukopa benki, point ni je wapo taayari kuachana na hii dhuluma na kujilimbikia maslahi huku walimu hawana hata kipato kinachowahakikishia mlo waa siku? Nimeisoma habari hii daily news nimeona inalengo la kutaka kuwaaminisha CCM sio wao pekee ambao ni mafisadi? Mhariri anatoa hoja zisizo na msaada wowote kuhusu suala zima la posho!
 
Wako wapi wale Pro-Chadema walikuwa wanapinga eti hakuna benki inayoweza kutoa mikopo kupitia posho, LAT na wenzako mpooo???
 
Nyie Pro-Chadema msiwe kama makinda ya bata yanamfata mama yao ata popote anapokwenda kama anavuka barabara. Hawo viongozi wenu wameishachukuwa mikopo benki kupitia hizo posho wanazozisema tena wa kwanza kuchukuwa ni Mbowe 200 milioni Zitto 150 milioni, mdhamini wao ni ofisi ya katibu wa bunge
 
Ayaah..!!sasa huo mkopo wanaulipaje hawa jamaa..jesus christ on a bicycle..!!hii mijianasiasa ni mijizi yote .
 
Kwa taarifa yako hakuna mbunge yeyote wa cdm aliyechukua posho tangu bunge hili linza wiki jana!!
Mwongo mkubwa.

Yeye mwenyewe Mnyika kasema "...Posho ya Kikao (Sitting Allowance) ambayo inalipwa hivi sasa kwa kuwekwa kwenye akaunti za wabunge moja kwa moja... " Hela wanaingiziwa moja kwa moja kwenye akaunti, hakuna aliyeirudisha!

You see, uzuri wa John Mnyika hasemi semi uongo most of the time. Mnyika kafananisha posho na nyama tamu, na kuacha posho kasema ni kama kumsusia fisi bucha yako ya nyama.

"Kabla ya kubadilishwa kwa mfumo mzima wa posho si jambo lenye maslahi ya umma kuziachia posho hizo zikatumiwa kiubadhirifu na serikali inayoongozwa na CCM badala yake ni lazima kuweka mazingira ya kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwenye masuala ya kimaendeleo kinyume na hapo itakuwa ni sawa sawa na ‘kumsusia fisi bucha.'' Chanzo

Kwa hiyo Mnyika hakatai kwamba huwa anakula posho, mikopo, mishahara, hela za mashangingi, wewe taja. Simtengenezi haya mambo, namnukuu:

"Nilichukua pia msimamo kama huo kwenye suala la mikopo ya magari ya wabunge, wakati wa kampeni nilipinga kiwango cha mikopo kinachotolewa cha milioni 90 kwa ajili ya gari kuwa ni kikubwa; na baada ya kuchaguliwa nilipewa mkopo huo na kuupokea." Chanzo

Hahahahahahaha....... Siasa za Tanzania na viongozi wetu zinatia udhia na machungu kupindukia lakini kwa sababu watu wazima haturuhusiwi kulia unaishia kucheka. John Mnyika, among the best and the brightest in the annals of our political leadership anakwambia ana msimamo mkali wa kupinga mikopo ya mashangingi lakini ukimpa atakula!
 

Sioni sababu ya kuwashinikiza wabunge wa Chadema wasichukue posho hiyo kabla haijaondolewa, kinachopiganiwa posho hiyo iondolewe si kwa wabunge tu ila watumishi wote wa umma, kwa nini mnakomalia tu wabunge wa chadema wasichukue? Hamna uchungu na nji hii, duh!
 

Mkuu naomba nikurekebishe kidogo,

Sheria ya benki ya mwaka 1961, 1991, na duniani kote duty of confidentiality ends if the information inquiry is of the matter of national interest, judicial inquiry or tax purposes (with authorisation from the commissioner). Hivyo basi Daily News hawajafanya kosa lolote. Ila mie najiuliza kama mshahara wako ni kidogo kwanini ukope hela nyingi hivyo milioni 200 kwa mshahara wa 2.5 na posho ya milioni 5???? Kweli Tanzania hakuna mkombozi wala mzalendo wamejaa walafi na watu wenye njaa tu.
 
<“So, the claim by the opposition MPs that they want the sitting allowances slashed is purely a publicity stunt,” said an impeccable source. >
1. Kama ni 'publicity stunt' inayoweza kuokoa mabilioni na yakawanunulia watoto wetu madawati ya kusomea, basi ni bora hiyo 'publicity stunt' mara kumi kuliko 'ndiyo mzee' inayoangamiza kizazi kizima.

2. Tumwamini yupi: mhariri wa Daily News au Mtoto wa Mkulima? Mtoto wa Mkulima amesema hizi posho ndio zinawawezesha Wahishiwa kuwamegea wapiga kura wao ndogo ndogo pindi wanapokumbana nao katika geti la Jengo la Bunge wakiomba nauli, karo za watoto, nk. Wakati huo huo Mhariri wa DN anatamka bila kutafuna maneno kuwa hizo posho ndio nguzo ya Wahishiwa kukopesheka!!

3. Ukishangaa ya Musa, basi subiri uyaone ya Bongo!!!!!
 
Nilishapata taarifa hapa hapa JF kuwa kulikuwa na habari iliyosambazwa kwa vyombo vya habari kutokea Ikulu kuhusu hili sakata la posho. Nadhani hii ni fotokopi ya habari hizo zilizotayarishwa na ikulu (ya walaji)
 
Sioni tatizo, sasa wafanye nini? Wakae nazo tu hizo hela huku zina depreciate? Huo utakuwa uzembe wa hali ya juu, you have to make your money work for you.
Pia Benki imevunja sheria kutoa data za watu kiholela, liangaliwe hili.
 

Kama habari ndio hiyo nani wa kumfunga paka kengele?
 
Kwa hiyo??? Unatetea posho za wabunge kwakuwa Mbowe na Zitto wamekopa?? Kweli wewe akili zako kama za Kiwete Mkwer.e
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…