Ndugu wana JF,
Nianze kwa kumpongeza Mh. Zitto kwa hatua alizochukua za kukataa wabunge wasilipwe posho ya Tshs 70,000/=. Niwapongeze pia CHADEMA na NCCR-Mageuzi kwa kupigia kelele jambo hili.
Hebu tujiulize, Kuna wabunge 357 kwa siku wanalipwa jumla ya Tshs 24,990,000/=. Ukijaribu kukokotoa zaidi unapata hesabu hizi:
Kwa wiki (5 days) = 24,990,000 x 5 = 124,950,000/=
Kwa Mwezi (4 weeks)= 124,950,000 X 4 = 499,800,000/=
Kwa miezi 2 (Budget session)= 499,800,000 X 2 = 999,600,000 Almost One Billion
Hesabu hii ni makadirio ya chini ya Bunge la Budget ambalo linachukua takribani miezi 2. Hapo zijakokotoa posho za vikao vya kamati za Bunge na posho za watumishi wa Bunge.
Hebu fikirieni, vikao vya kawaida vya Bunge ambavyo huketi takribani wiki 2 (10 days) na kama sikosei ni kama vikao vitatu hivi ambapo jumla ya siku wanazokaa ni kama siku 30 (30 days) kwa vikao vitatu.
Hesabu za posho zao kwa vikao hivyo vitatu ni kama ifuatavyo;
30 days X 24,990,000 = 749,700,000/=
Hivyo basi, wastani wa posho za wabunge kwa mwaka ni;
Budget session (999,600,000) + Other Three sessions (749,700,000) = 1,749,300,000 (~ 1.75 Billion).
Kwa Miaka mitano: 1.75 Bil X 5 = 8.75 Billion
Kama nilivyosema hizi ni posho ambazo hazihusishi posho za vikao vya kamati za Bunge wakati wa Bunge session na baada ya Bunge sesssion (Kuzungukia miradi au kukagua n.k) na hazihusishi watumishi wengine wa Bunge.
Swali:
1. Watu wanaodai hoja ya Zitto na CHADEMA/NCCR-Mageuzi haina mashiko ni kweli , kwa takwimu hizi????
2. Pesa hizi zinaweza kujenga madarasa managapi ya shule za msingi?
2. Zinaweza kutengeneza madawati mangapi ya watoto wetu wa shule ya msingi?
3. Inaweza kulipa walimu wangapi wa shule za kata? n.k
Naomba kutoa hoja.
Tujiulize, Vikao vyote ambavyo wabunge wanakaa kwa Mwaka na kulipwa posho hiyo ni