Posho na Mishahara ya wabunge...

Posho na Mishahara ya wabunge...

Haya Maandamano tunataka yawe tofauti na malengo ni Kuwaaibisha kikwete, Mkullo, Ndullu, Makinda na wabunge wa ccm. Umaskini wa Tanzania ndio huu nothing else ....

Kama una Ujumbe kwa Wabunge wa ccm na serikali yao ya kizembe, jiandae kwenda Dodoma na Miji mingine. Hakikisha Ujumbe Wako Unafika Bungeni na Ikulu. We need creativity here ....to send message to the world.

Usiishie kwa Wabunge wa CCM tu bali pia na wale wa CHADEMA, CUF, TLP na UDP ambao bado wanachukua hiyo posho, so far waliokataa posho ni Zitto wa CHADEMA na vijana wa Kigoma wa NCCR, kwa kifupi NI WABUNGE WA UPINZANI WA MKOA WA KIGOMA NDIO WALIOKATAA POSHO YA VIKAO , hivyo usiwape credit ambayo hawana Wabunge wengine 44 wa CHADEMA, kuanzia Mbowe+Mnyika+Tindu Lisu+Lema to infinit wanaendelea kuitandika hiyo posho kama Wabunge wenzao wa CCM, no change na hawajaonyesha uongozi wowote katika hilo.

Hongera Zitto Kabwe, hongera David Kafulila, hongea Felix Mkosamali, hongera Moses Machali, Hongera Zeitun Boyogela, Hongea kubwa kwa Wananchi wa mkoa wa Kigoma kwa kuwachagua Wabunge makini, na shame kwa Wabunge wengine wote wa CHADEMA wakiongozwa na Mbowe...

Kama kutakuwa na maandamano yoyote basi yawe ni ya kuwaunga mkono Wabunge hawa wa walioonesha mfano kwa vitendo na kuwashutumu Wabunge wengine woote bila kujali vyama vyao wanaoendelea kupokea posho hiyo.
 
Hiyo ndio kazi yenyewe! Kudai haki na uwajibikaji.
Kwanza fateni haki ya mwajiri wenu. Na mwaka huu mtafukuzwa wengi makazini, Ofisi za chadema ndio zitakua makao makuu ya wakabaji.
 
Haya maigizo, mbona mbowe hakatai posho km Zitto. andamaneni kwa wabunge wa chadema kutom support zitto, mkimaliza hilo tutaandamana.
 
Kuna haja ya kuangalia posho zote, yaaaani zoooooooooooooote!, kwanzai za vikao mpaka ile mihela ambayo wabunge huwa wanagawanaga baada ya miaka mitano. Nipesa nyingi sana zinapotea sasa sijui kama hilo nalo mnalizungumzia au ndo hivo vi sitting allowance??

Na ile mishangingi mnayokopeshwa wabunge na mnaikubali pia angalieni kwani sidhani kama mnatozwa kodi, pili mikopo ya hiyo midude sidhani kama ina riba, alafu kwani ni lazima kukopeshwa ile migari, Piga kitu ya Rav 4 hapo tuliza makalio!
 
Great thinker msijibizane na wapinga mageuzi kama Omr,ritz,Tumain,Ms na wengine! Kufanya hivyo kunaondoa umakini ktk kujadili mstakabali wa taifa letu wa kupinga ufisadi wa ccm!!
 
Haya maigizo, mbona mbowe hakatai posho km Zitto. andamaneni kwa wabunge wa chadema kutom support zitto, mkimaliza hilo tutaandamana.

Hapa kuna upotoshaji wa makusudi. Suala la kukataa posho sidhani kama ni la Mhe. Zitto binafsi, bali liko katika bajeti kivuli ya Kambi ya Upinzani ambayo msingi wake si Waziri Kivuli wa Fedha na Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Huu ni msimamo wa chama (CDM), utekelezaji wake uko kwenye bajeti. Sidhani kama limewekwa kwenye bajeti bila utaratibu wa kulitekeleza. Mhe. Mbowe amewahi kulitolea maelezo kwamba Zitto amefanya vile kwa sababu ya kujibu hoja za wapotoshaji lkn hapa kuna utekelezaji wa pamoja na si mbunge mmoja.

Tunasubiri bajeti isomwe tuone utekelezaji wake na mahali hizo posho zinapopaswa kuelekezwa si kutuambia habari za Kigoma Dev. Innititive (KDI) wakati ni pesa za walipa kodi wote wakiwemo wa Mwanza. Wabunge wa NCCR wamefanya vema kuonyesha nafasi yao kwenye kambi ya upinzani. UDP, TLP na CUF tunahitaji kusikia kutoka kwao..!
 
Hapa kuna upotoshaji wa makusudi. Suala la kukataa posho sidhani kama ni la Mhe. Zitto binafsi, bali liko katika bajeti kivuli ya Kambi ya Upinzani ambayo msingi wake si Waziri Kivuli wa Fedha na Kaimu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Huu ni msimamo wa chama (CDM), utekelezaji wake uko kwenye bajeti. Sidhani kama limewekwa kwenye bajeti bila utaratibu wa kulitekeleza. Mhe. Mbowe amewahi kulitolea maelezo kwamba Zitto amefanya vile kwa sababu ya kujibu hoja za wapotoshaji lkn hapa kuna utekelezaji wa pamoja na si mbunge mmoja. Tunasubiri bajeti isomwe tuone utekelezaji wake na mahali hizo posho zinapopaswa kuelekezwa si kutuambia habari za Kigoma Dev. Innititive (KDI) wakati ni pesa za walipa kodi wote wakiwemo wa Mwanza. Wabunge wa NCCR wamefanya vema kuonyesha nafasi yao kwenye kambi ya upinzani. UDP, TLP na CUF tunahitaji kusikia kutoka kwao..!
ila kuna kila dalili ya Makinda kukataa kuwasupport na hilo swala kwa kutishia kuwafukuza, wakat upande wa pili mkulo anasema ata waandalia form, je wakikataa hayo mapendekezo ya kambi ya upinzan?!! Next step itakuwa n nn? Hapa kna maswali meng yasiyo na jibu ,ebu tusubirie hiyo kesho mkuu.
 
Maandamano hayo yashirikishe vyama vyote, hata ccm ambao,wanapigika na maisha sawa na watanzania wote. Mwana 'magamba' ambaye haguswi na ukali wa maisha kupitia mambo kadhaa ikiwemo kodi kubwa katika mafuta, madeni makubwa yanayodaiwa na tanesco kwa serikali ya Zanzibar,ufisadi wa watendaji wa ngazi zote wa serikali ya ccm asi shiriki. Lakini ajue ukoo wake wote wamepigika. Vimbwenelehi wa nape wao wakae pembeni.
 
Shule yetu nzuri.jpg


Wana Jf hivi huyu mbunge wa eneo hili anathubutu kula Posho (sitting allowance) na mambo kwake yako hivi.....huenda yeye ni mmoja wa wale wazomeaji maarufu bungeni, I wish ningejua hapa ni wapi.

Picha kwa hisani ya Profesa...
 
nchi yetu ina wazalendo wachache na mamluki Lukuki, naipenda tanzania nawachukia mamluki wanafiki wanaojifanya hawajui hali duni zinavyowasotesha watanzania..wanavuja jasho , halafu wachache wenye ulafi na wasiotosheka wanajineemesha...mi niko pamoja na mtu yeyote yule anayepigania maslahi ya taifa mbele..go ahead guys.
 
Mkulo asema ni kazi ya Baraza la Mawaziri
Makinda: Mshahara wa mbunge ni 2.5m/- tu
Saini milioni moja kukusanywa nchi nzima


Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo


Posho za wabunge sasa ni zogo kubwa. Waziri wa Fedha, Spika wa Bunge, wabunge na wanaharakati wanakamatana koo juu ya uhalali wa kuendelea kulipwa huku wananchi wakitaabika kwa umaskini wa kutupwa.
Moto mpya wa kupinga posho wanazolipwa wabunge jana ulizidi kusambaa kwa kasi, baada ya wana harakati kuingilia kati kutaka zifutwe na kutangaza kampeni ya kuzipinga.
Kampeni maalum ni ya kukusanya na kupokea maoni ya watu milioni moja kote nchini, kwa lengo la kushinikiza kufutwa posho zisizo na tija za wabunge na watumishi wa serikali, inaanza rasmi leo.
Kampeni hiyo inaendeshwa na Taasisi ya Muungano wa Maendeleo (ADO) na inataka posho hizo zisaidie katika shughuli za kijamii. Mkurugenzi Mtendaji wa ADO, Ntamilyango Buberwa, aliwaambia waandishi wa habari kuwa ukusanyaji na upokeaji wa maoni utafanyika kabla ya kusomwa bajeti ya Wizara ya Fedha na Uchumi kisha watayawasilisha kwa Rais Jakaya Kikwete wakiamini ni kiongozi makini mwenye kujua umuhimu wa maendeleo nchini.
Alisema wanaamini baadhi ya malipo wanayolipwa wabunge na watumishi wa serikali, ni kinyume cha taratibu kwani zinalenga kulipia kazi ambazo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku ambayo inalipwa kupitia ujira wa mishahara yao ya mwezi.
Alisema vitendo vya wabunge na viongozi wa serikali kutaka kuendelea kupatiwa posho za vikao na misimamo tofauti inayotolewa na viongozi wa Bunge, akiwamo Spika, vinawapa shaka na utayari wa uzalendo wao katika kusimamia maslahi ya umma. Buberwa alisema viongozi hao wanawapa Watanzania wasiwasi wanapotoa misimamo inayosigana na kwamba, dhana ya namna hiyo, ni kukosa dhamira ya kweli katika uwakilishi wao kwa maendeleo ya wananchi.
Alisema katika nchi kama Tanzania, ambako kima chini cha chini cha mshahara wa mfanyakazi hakizidi Sh. 160,000 kwa mwezi, ni aibu ya aina yake kwa mbunge kukubali kulipwa pesa za walipakodi maskini Sh. 150,000 kila siku kwa vikao, ambazo ni sawa na Sh. 1,050,000 kwa wiki, nje ya mishahara yao.

TGNP: NI KOSA KULIPA POSHO HIZO
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) umesema ni kosa kwa serikali kuendelea kutoa posho kwa wabunge na viongozi wengine wa ngazi za juu serikalini huku wafanyakazi wa ngazi ya chini wakipata mshahara usioweza kukidhi mahitaji yao.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya, alipokuwa akitoa tathmini ya bajeti ya mwaka huu.
Mallya alisema sehemu yoyote duniani kipimo cha kupanga kima cha chini cha mshahara kwa wafanyakazi huwa ni gharama ya mahitaji muhimu ya mfanyakazi wa ngazi ya chini kuyapata kwa kutumia mshahara wake.
" Hii ndiyo inayofanyika duniani kote. Sasa sisi kama wanamtandao, tunapinga kwa nguvu zote kutoa posho ya aina yoyote kwa wabunge kama ilivyo kwa maofisa wengine wakubwa wa serikali, kwa kuwa wana hali nzuri kimapato ukilinganisha na wafanyakazi wa ngazi ya chini na hasa walio pembezoni, wanawake wakiwemo," alisema.

MKULO AWABEZA WANAOZIPINGA
Wakati wanaharakati wakipinga, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, amesema hana uwezo wa kuondoa posho za Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, na wenzake wa NCCR- Mageuzi wanaotaka ziondolewe.
Akizungumza na NIPASHE mjini Dodoma jana, Mkulo alisema Baraza la Mawaziri pekee ndilo lenye uwezo wa kutengua sheria hiyo na si yeye hivyo wanaomtaka azihamishe hawajui wanachosema.
" Mimi Mkulo sina uwezo wa kubadilisha maamuzi ya baraza la mawaziri hata siku moja, suala likishaamriwa kule mtu binafsi huna uwezo wa kulitengua, labda niende kwenye baraza hilo nijenge hoja wakubali," alisema.
Katika hatua nyingine, Mkulo alishangaa hatua ya wabunge wanaokataa posho hizo zipelekwe kwenye majimbo yao badala ya kuiachia serikali uamuzi.
" Kama wanataka zifutwe waseme, lakini kusema ziende sehemu fulani haina maana, kama kweli wanataka kubana matumizi waseme posho hizi zifutwe na wafuate taratibu maana ziko kwa mujibu wa sheria za nchi,"alisisitiza Mkulo.
" Zitto ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge kama kweli hataki hizi posho angesema kule zikatwe sasa mbona alishiriki kuzipitisha? "alihoji.
Wabunge wa Chadema na wengine wanne wa NCCR-Mageuzi wote kutoka majimbo ya Mkoa wa Kigoma, wanataka posho hizo zifutwe.
Akizungumzia posho hizo za vikao, Mbunge wa Vunjo (TLP), Agustine Mrema, alisema kwa kuwa serikali ilishatangaza katika bajeti yake kuwa itapunguza posho zisizo za lazima, basi itaangalia kama posho za wabunge nazo hazina ulazima.
" Mimi naunga mkono posho zisizo za lazima ziondolewe, kama serikali itaona posho za wabunge si za lazima na ikaziondoa mimi sina neno, wakiona mbunge anaweza kuja hapa Dodoma na akafanya kazi zake bila kuhitaji hiyo posho sawa mimi nasubiri uamuzi wa serikali," alisema.
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid, alisema kuwa: " Katiba inatamka wazi kwamba mtu akifanya shughuli hii malipo yake ni haya sasa tatizo ni nini."
Alisema kama wanaopokea posho hizo wanaona hawana haja nazo waandike hundi na kuzirejesha zilikotoka badala ya kupiga kelele kwenye vyombo vya habari.
" Hizo ni cheap politics (siasa uchara) ambazo mimi binafsi sizitaki na kamwe sitazishabikia, mbona wanapokwenda kwenye halmashauri kule wanasaini posho iweje wakija huku ndipo waseme hawazitaki, maoni yangu ni kwamba tukiamua kubadili sheria na kuziondoa sawa sitakuwa na tatizo, lakini kwa kuwa sasa hivi ziko kisheria tatizo linatokea wapi, " alisema Rashid.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema kuna watu wanapotosha kuwa mshahara wa mbunge ni zaidi ya milioni saba wakati mshahara halisi ni Sh. milioni 2.5 na wanakatwa Sh. 900,000 kila mwezi kwa ajili ya mikopo ya magari waliyochukua.
Imeandikwa na Sharon Sauwa na Joseph Mwendapole, Dodoma; Muhibu Said na Raphael Kibiriti, Dar.



CHANZO: NIPASHE

MAONI YANGU

Huyu Mustafa Mkulo (Kwanza tunaomba utuachie nchi yetu Mmalawi) sijui anatupeleka wapi. Jamani for the sack of the record wiki iliyopita Mkulo alitwambia kwamba kwa wale wabunge wote wasiotaka kuchukua posho (IN BOLD SITTING ALLOWANCE) atawaandalia form za ku sign ili kuzikataa posho hizo.

Jamani huyu Mmalawi kwa kutuona sisi ni wadanganyika ni mazezeta, hata kabla ya wiki haijapita anakuja na statement nyingine tata kwamba baraza la mawaziri tu ndilo lenye uwezo wa kubadilisha hizo posho (MSISITIZO SITTING ALLOWANCE, MAANA CCM WAMEANZA KUPOTOSHA KWAMBA NI POSHO ZOTE). Sasa kutokana hii kauli mkanganyikao nani hajui alisemalo? Mkulo au wabunge wa upinzani waliokataa kuendelea kununuliwaa na CCM kwa hizo SITTING ALLOWANCE! BTW, Hivi anayejiita MTOTO WA MKULIMA YUKO WAPI KUHUSU hili?

Hivi huyu Mkulo ametuona kwamba sisi watanzania wote ni mbumbumbu hatujui kinachoendelea huko bungeni na kwenye kamati za Bunge. Lakini sio makosa yako Mkulo, kama watanzania wote hatuwezi kumpata waziri wa fedha hadi tufikie ku-import kutoka Malawi una haki ya kutona mabwege.

Ni wazi kuwa huko bungeni na kwenye kamati za bunge majority ni CCM. Na tunafahamu CCM ni wachumia tumbo. Zitto hata akipeleka kwenye kamati hoja ya SITTING ALLOWANCE itapingwa kwa nguvu zote na CCM kama mnavyofanya sasa hivi mbele ya kadamunasi ya watanzania, hadi kufikia hatua ya Anne Makinda eti kutishia kumfukuza ubunge Zitto simply amekataa posho (SITTING ALLOWANCE, SIC!) Kweli CCM mnatia aibu hii sio tena dunia ile ya mwaka 47. You're days are numbered mimi sitawasamehe kamwe, nimeshaanza kwenye familia yangu kuonesha dhuluma yenu, sasa hivi niko ngazi ya mtaa. Mungu anijalie afya njema niendelee na elimu ya uraia hadi 2015 matokeo yake mtayaona!
 
Kweli kuendelea kumlipa mhe kama huyu Sitting allowance bado kuna watu wanaona sawa tuu. Mshahara anakula kama kawaida kisha akifanyacho hapo nacho tukilipie? Utakuwa ujinga.View attachment 31951
 
Hivi nyie hamna kazi?
SISI TUNA KAZI MDOGO, NA KAZI YETU NI KUIFUNDISHA NA KUILEKEBISHA GOVT KWA USTAWI WA NCHI YETU. Kupitia kazi hii tunayoifanya tz itasonga mbele na wewe mjinga utaanza kujivunia mafanikio ambayo hukuyapigania. Acha ujinga wewe kazi yetu ndio hiyo na usiweza kukemea nyamaza tutakusaidia kukemea.via Mobile
 
Kila lenye mwanzo halikosi mwisho. Kwa kuwa SISIEM ilianza lazima itafikia mwisho. Na mwisho wa hili GAMBA ni sasa. Maandaamano ndiyo mwisho wake. Big up CDM!
 
Back
Top Bottom