Jasho la Damu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 956
- 120
Bado sijamwona swahiba wa MS, Faiza Foxy sijui nae ataendeleza utaifa unaoanza kumwingia MS au ataendelea kushikilia magamba yake yasidondoke.
Sasa si alihogwa na mijinga ulitaka afanyeje!me naungana na ww kaka huyu zitto ni mnafiki wa cdm mbona kuna pesa gari na kiwanja cha ufukweni alihongwa na thithiem ameshindwa kusema vipelekwe jimboni?wajinga wenzie wa cdm ndo ataendelea kuwa fitini lkn sisi wengine tunaojua data zake tunamwangalia.in short anatafuta umaarufu kupitia hizo posho km kawaida yake.
Let us be realistic,Wanachama wengi ikija kwenye kuchangia vyama vyao wanakuwa wagumu.Kapite mapato na matumizi ya chadema wakati wa uchaguzi uangalie ni kiasi gani wanachi walichangia pamoja na kufanya kampeni kubwa ya kuwaamasisha wananchi kuchangia.Wanasiasa wanawageuza wananchi kuwa wajinga, na bahati mbaya tunaponzwa na ushabiki wa vyama. Akishasema kiongozi wangu wa chama ni sahihi hakuna kuquestion.
Ukisoma Habari Leo, ya leo Mbowe anasema Shangingi lake (V8) hawezi kuacha kulitumia sababu tayari kashapewa, anasahau katibu wake (Dr.Slaa) alivomshambulia W/Mkuu kuwa anatumia gari la kifahari.
Na kwa nini ruzuku za vyama zisivutwe, wanachama ndio wachangie vyama vyao? Tunapoteza pesa nyingi kwa vyama ambavyo mi naona wengi ni kunufaisha viongozi wa vyama vya siasa. Hili hawataki kabisa.
Ukiangalia kwa undani unaona kuwa hatujawa na viongozi wenye nia ya dhati. Wengi ni makelele ya kutafuta umaarufu na kuchumia matumbo yao.
KDI ni ya nani? Nani mwanzilishi wa KDI?Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana. Namshangaa mtoa mada anamwita Zitto mnafiki. Ningekuona wa maana kama ungempongeza kwanza then ungeshauri njia bora za matumizi ya hizi pesa, sio kumkejeli. Lazima tukubali kwamba this is a step in the right direction. Inaonekana kwako unaona ni sawa tu, tena kuna wabunge wengine useless hata michango huwa hawatoi, kazi wanayofanya ni kula posho tu.
nashawishika unafikiria kwa kutumia makalio badala ya ubongo."kwa mfano, mimi ni mjumbe wa kamati ya uongozi (ya bunge), nasaini 'sitting allowance' katika kikao cha bunge, nikiitwa katika kikao cha kamati ya uongozi nasaini tena sitting allowance na hata kama kutakuwa na kikao kingine jioni naweza kulipwa, sasa kama huo siyo wizi ni nini?"
alisema pamoja na kwamba wabunge wa chadema akiwamo yeye wanachukua posho hizo, kamwe hawataacha kusema kwani tatizo si wao kuchukua, bali sera inayoruhusu ufujaji huo wa mali ya umma.
maneno ya rangi nyekundu hapo juu yamesemwa na chairman mbowe.
Huyu mangi hayuko serious. Anaping posho huku anadai yeye na wenzake wataendelea kuichukua.
Bunge letu ni la kupewa pole kwa kuwa na kiongozi wa upinzani kama mbowe....what a disgrace to tz!
Kama mmegundua kuwa mnaibia watz si muache kuendelea kuchukua kama zitto?
Acheni unafiki.
KDI ni ya nani? Nani mwanzilishi wa KDI?
Kwani mwizi akikiri kosa katika famili, anaambiwa ni mnafiki au assibe tena. Watu wangine tumekosa uzalendo kabisa kiasi cha kua vipofu. Walimu watu wanaolipwa 200,000 wanapata teaching allowance kwa kufundisha kwanye mazingira magumu. Zile seat za bunge letu ni too comfotable to get an allowance. Wako wafanyakazi wanaofanya kazi za hatari sana na hawapewi allowance. Trilioni moja, hela ya kujikimu, mshahara millioni 12. yote hayo unamwambia nini mkulima wa Tanzania. Eti unafiki. Rafiki!