THINKINGBEING
JF-Expert Member
- Aug 9, 2010
- 2,779
- 1,304
I swear u will never give any valid argument until when u start to use in THINKING a special organ that is indowed in ur head for that task.Hamna aliye serious hapo, hiyo ni domo tu la kisiasa, tulimsikia Dr.Slaa mwaka jana na akapata sana publicity ya kisiasa lakini leo hii hana tena ujasiri wa kuliongelea hilo kwa kuyaramba matapishi yake na hivyo kuonyesha uhalisia wa mtazamo wake halisi aliokuwa ametuficha juu ya hilo.
Sintamuamini mtu yeyote juu ya hizi porojo za kujitafutia cheap popularity,kama mtu yuko serious aanze sasa kwa kuonyesha mfano wa kuzikataa hizo posho na sio vinginevyo.
Cheap and populist poitics.
We need to push for the overall public policy as far as the issue of allowances is concerned. Populism won't do anything neither can it help much, dear Zitto.:majani7:
Hakuna mbunge hata mmoja wa CDM anataka posho ipunguzwe, wote wako pale kwa maslahi yao na si ya wananchi, hizo ni daganya toto tu za kisiasa mkuu
Naibu Spika Job Ndugai, amewaambiwa wabunge wa kambi ya upinzani wanaosema posho za wabunge ziondelewe waonyeshe mfano kwa kuiandikia ofisi ya bunge (Spika) kuomba kuondolewa posho zao na wao wataziondoa haraka>
Amesema kitendo cha wabunge hao kuongea kwenye majukwaa ya kisiasa kuhusu kuondolewa kwa posho hizo hakina tija na wanapaswa kuongoza kwa mfano kwa kuandika barua kwa spika ili posho zao zianze kuondolewa kwanza.
Source: TBC 1 asubuhi hii, kipindi cha Jambo Tanzania.
I swear u will never give any valid argument until when u start to use in THINKING a special organ that is indowed in ur head for that task.
Nafikiri wewe ni mmoja wa watu ambao hudandia mada bila ya kuzisoma kisawasawa. Alichosema Mhe Zitto ktk bajeti ya kambi ya upinzani ni kuwa wabunge hulipwa posho za aina mbili kwa siku, ya kwanza inayitwa Sitting Allowance ya SHS 80,000/= kwa ajili ya kukaa katika vikao vya bunge; na ya pili ni posho ya kujikimu kwa lugha ya kigeni huitwa "Subsistence Allowance" ya Shs 70,000/= kwa ajili ya chakula, malazi n.k kwa kuwa viako vya bunge hufanyika nje ya vituo vyao vya kazi kwa maana ya maimbo yao ya uchaguzi. Ndipo akahoji uhalali wa mbunge kulipwa posho ya kukaa katika vaikao vya bunge ilihali kazi aliyoomba ni kuwawakilisha wananchi katika bunge na tayari analipwa mshahara kwa kazi hiyo hiyo.
Hivyo bajeti ya upinzani inapendekeza posho ya kujikumu iendelee na posho ya kukaa katika vikao vya bunge iondolewe. Vivyo hivyo kwa kwa watumishi wa serikalini hususan wakubwa wakikaa katika vikao mwisho hupitishwa bahasha zenye posho ilihali waliomba wenyewe kazi za kutumia akili katika vikao ndio maana hawafanyi kazi za shuruba kama vile kilimo, vibarua n.k. Kiutendo cha watumishi wa serikali tena wa kada ya juu tu, kulipwa posho ya kutimiza wajibu wao ambao tayari wanalipwa mishahara kuutimiza ni ufujaji mkubwa wa fedha za walipa kodi. Ndio maana vikao serikalini haviishi. Kinachotokea wanapanga vikao kufanyika katika mikoa nje ya vituo vya kazi na kupata posho mbili kama wabunge yaani posho ya vikao na posho ya kujikimu.
Je hiyo ndio siasa kwako?
M nafikiri ni wakati mzuri kwa wabunge wa UPINZANI wa kweli kuuthibitishia uma kwamba wapo pamoja nao kwa kuzikataa hizo posho kwa nguvu nzote. Asilimia 99 ya wananchi wote wanaunga mkono hoja hiyo isije ikawa walikuwa wanatafuta umaarufu bila kujitoa mhanga. Kwa mfano idadi ya wabunge wote wa upinzani au watakaokubaliana na hoja hiyo hela zao zikajumulishwa na kufanya kitu cha maana kama kujenga vyoo au kununua madawati tutaona wamefanya la maaana sana ili hata watakapokuwa wankuja kwetu kututambishia waseme tuliokoa kiasi fulani cha hela zikafanya kazi fulani:smiling: Cha kushangaza unaweza kuona hoja hiyo imeishia mdomoni mwa Zitto.
Its time for action, Mh Waziri Zitto umetoa hoja, kama wabunge hawataki waacheni, lakini kama hili liko ndani ya uwezo wenu CDM litekelezeni ili ukweli wake uonekane.
Kwanini waachwe na sisi wananchi ndio tumewaajiri? Mimi nashindwa kuelewa hii mantiki. Hili ni suala la kupunguza spending hata makazini utasema tupunguze marupurupu ya matarishi alafu madereva tuwaache? Sisi wananchi tuna-demand wafanye hivyo, sisi ndio tumewaajiri na sisi ndio tunawalipa. Hivi bosi akija kazini akasema sasa tunaondoa overtime pay inakuaje. Ni either unakubali au unaacha kazi; huwezi kujadili eti ondoa kwa fulani lakini mimi hivi na hivi.
This is the push we are talking about, not just words; refusing the allowance will send a very strong message as to how serious we are in confronting corruption disguised as allowance. If you are one of those who like to talk without action, go ahead and attack Zito, but he has set a very good example to all MPs.
We must walk the talk. I have written to the Clerk of Bunge that all sitting allowances I am entittled to should be directed to a charity in my constituency up to when the law is changed and sitting allowances scrapped.
I will advise my fellow CHADEMA MPs to take similar measure.
Kwa kuwa hao nguruwe wa kijani wanaiba mihogo ya wananchi, ni bora na sisi tuibe pia??? Mh! Jamani!"Hatuwezi kuwaachia nguruwe wale mihogo shamani peke yao"___Hamad Rashid Mohamed (Mp)