Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Mimi nilidhani watu wanaandamana kuunga mkono kitu fulani si kwa sababu wanalipwa. Je zikiondolewa posho za maandamano watu wataendelea kuandamana au idadi itapungua?
Yawezekana wakati mwingine tunaona watu wa kampuni fulani wanapita mbele ya mgeni wa heshima kwa furaha si kwa sababu wanafurahia kilichowaleta hapo bali wanapigia mahesabu 'posho ya bajeti'?
Hivi si watu wanalipwa kwa mwezi, sasa na hiyo siku ya maandamano si imo ndani ya mwezi huo? Ni sawa na posho ya kikao, ambapo kikao cha ndani ya kujadili mikakati mipya watu wanalipwa posho...
...ndivyo mlivyo!Hii poa tu...haina noma wala nini...
...ndivyo mlivyo!
Leo ni Mei Dei... baadhi ya mashirika na idara za serikali ambazo zinashiriki maandamano zinalipa wafanyakazi wake posho ya kuja kuandamana na mabango. Mojawapo ya mashirika yanayofanya hivyo ni la ATC ambapo leo wale wote walioshiriki maandamano walikusanyika Mnazi mmoja na kujiandikisha (kwa ajili ya posh) na kuelekea uwanja wa Taifa.
Hivi, kweli kuna ulazima wa kulipa watu kuandamana au ndiyo namna nyingine kumegeana kula. Wenyewe wakitoka uwanja wa Taifa basi wanarudi Terminal One kulipokea dege lao kubwa linalokuja na nusu ya viti vichakavu...
kazi ipo...
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni; wenzetu Bongo wanatoa posho ili watu waandamane; lakini katika baadhi ya mataifa ya Africa mf. Ethiopia, askari hupita nyumba hadi nyumba siku hiyo na wanahakikisha watu wote wanashikriki.Jana kuna mahali(mada ya Mwanahaki kuhusu kero ya usafiri Dar) niliandika kwamba mifumo ya uendeshaji hapa Tz ni mibovu; na inaachwa katika hali hiyo kwa sababu inakuwa ni mifereji ya kutiririsha kipato haramu cha lazima kufidia kipato halali kidogo ikilinganishwa na gharama za kuishi.
Hili la kuwalipa watu ili waende kwenye maandamano ni mfano halisi. Kwa habari nilizonazo wengine hulipwa elfu 20+ kwa tukio kama hili. Zinasaidia kusukuma siku. Mabosi wanaiba. Wafanyakazi wa chini hugawiwa kidogo, au kuachiwa mianya ya kujitengenezea chochote.
Katika hili: Serikali ya CCM inajijengea mazingira ya "kupendwa" miongoni mwa watumishi wa serikali na umma.
Ndio maana mojawapo ya majaribu yanayozunguka kichwani mwangu ni lile la kukubali yaishe. Hii vita ni kubwa mno kiasi kwamba ushindi tunaweza tusiuone katika maisha yetu..
Nyani, kutokuwa katika denial siyo justification ya hii malady... tunaweza kuwa tunasutwa na hali hii kwa sababu ya inevitability ya kuwa tunaishi pamoja na ma-propagator katika jamii, lakini si kwa makusudio wala matendo yetu. Inseparability ya belonging na acceptance yake ndicho chaonekana chanzo cha kujisuta hapa.At least hatuko kwenye denial...
Mlioko kwenye denial hali halisi inawasuta...Lol