POSHO: Bunge lamjibu Zitto Kabwe; atoa msimamo wake

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
8,316
7,734
What does this mean? Au alifikiri watu wanabeep walipokuwa wanataka posho ziondolewe?

Posho-Za-Vikao-Majibu-Ya-Bunge.jpg

Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg
 
Attachments

  • 1-2ade5936cd.jpg
    1-2ade5936cd.jpg
    58.6 KB · Views: 907
Hii kali! jamaaaaaaaaaaa kawasitua sana; lakini wamekimbia kivuli chake.
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?
 
Mimi naona Bunge linajichanganya kwa sababu Jumanne Asubuhi wiki hii kupitia vipindi vya asubuhi vya TBC1 nilimsikia Naibu Spika Ndugai akisema kuwa kama kweli kambi ya upinzani iko serious kutokutaka posho basi waliandikie barua bunge nalo litawakata hizo posho mara moja. Sasa, nashangaa majibu haya kwa Zitto.
 
attachment.php

Alivyojibiwa sawa sawa, sasa tunamngoja Zitto atangaze aseme mimi sizitaki na kuanzia leo nisilipwe, hapo ndio tutajuwa kweli.
 
Mi naona ubinafsi wa Zitto umeharibu lengo la CDM la kususia posho! Badala ya kusia yeye anataka ziende jimboni kwake !
 
Naunga mkono hoja ya hoyce. Mpango huu ungekuwa na maana na uzito wa kipekee kama kwa mfano wabunge wote wa upinzani au hata CHADEMA peke yao wangeandika barua ya pamoja kukataa posho hizo na kutoa maelekezo ya wapi zipelekwe. Hata hivyo, bado hawachelewa. Ni opportunity nyingine kwa kambi ya upinzani kuwin support ya umma kwa kweli wapo serious.
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?

Kabla hamjaenda mbali na mjadala hii hapa chini ndiyo barua ya zitto sasa cha muhimu kwa sasa ni ku-assess kama hayo majibu ya bunge yanakidhi maombi ya Zitto. Kwa maoni yangu bunge limeplay politics at its best, maana wao kama waajiri hawampi zitto hizo posho mikonomi sasa kuna ugumu gani kuzideposit huko KDI anakotaka. After all hii haitainvolve any bunge official to do it manually. Kwamba et labda spika itabidi akapange foleni benki....... inasikitisha kuona bunge linashindwa kuaddress hata ishu ndogo kama hizi.

o5v0i0.jpg
 
Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi majibu ya dharau na kiburi aliyoyatoa Mustafa Mkulo. Mkulo kasema anangoja hoja ya posho itinge bungeni halafu baada ya kupitishwa budget yake ataandaa fomu maalumu kwa wabunge wa CDM na asiyetaka posho asign hiyo fomu halafu posho zao zipelekwe kwenye "vituo vya kuleo Yatima" Nashangaa katribu wa bunge naye anajibu utumbo, kwani alichosema Kabwe hapo kwenye barua yake ni kuwa badala ya kupeleka kwenye account yake binafsi aweke kwenye account ya KDA.

Ulevi wa madaraka ni kitu kibaya sana hivi Mkulo alikuwa na haja gani ya kusema hivyo, eti kulea yatima? Tena ana uhakika hakuna mbunge hata mmoja wa CDM atasign hizo fomu, hivyo anasema Kabwe ni mnafiki, kwa kuwa alihusika katika kupitisha hizo posho

Wabunge wa CDM huu ni mtaji mkubwa sana wa kisiasa, mkicheza vizuri hii karata mtashangaa ccm nao wataopt out kimya kimya. Unganeni katika hili, sikupenda kauli za Mbowe kuwa hata wakichukua haina maana wanakubali huo mfumo. Shilingi elfu sabini kwa siku wanazokaa dodoma sio nyingi kuzidi mtaji wa nguvu wa kisiasa watakaoupata wakizikacha hizo posho
 
Zitto ana nia njema lakini sidhani kama mtu unaweza kukataa sehemu ya stahili yako kama muajiriwa. Yeye angeweza kuiambia benki yake ipeleke hiyo posho kila ikiingia kule anakotaka wakati akiungana na wenzake kupigana ili hiyo posho iondolewe kwenye stahili ya nafasi ya ubunge.

Amandla......
 
Mimi naona Bunge linajichanganya kwa sababu Jumanne Asubuhi wiki hii kupitia vipindi vya asubuhi vya TBC1 nilimsikia Naibu Spika Ndugai akisema kuwa kama kweli kambi ya upinzani iko serious kutokutaka posho basi waliandikie barua bunge nalo litawakata hizo posho mara moja. Sasa, nashangaa majibu haya kwa Zitto.
ninawasiwasi kuhusu baadhi ya wabunge wa chadema,as far as suala zima la teamwork linavyohusika. kama tunavyowasikia wenyewe kuhusu suala kufutwa posho inaonekana ni suala la kichama na kambi yao nzima ya upinzani. sasa iweje mtu mmoja aanze ku execute mpango mzima wa chama peke yake? ndo maana zinajengeka hisia za ubinafsi ndani ya chama na hata uzito wa issue yenyewe unapungua inapapelekwa hoja na mtu mmoja mmoja tofauti na ambavyo ingepelekwa na kambi ya upinzani kama hoja ya pamoja. 2. tukiangalia majibu ya ofisi ya bunge, kwamba utaratibu uliopo sasa ni" kumlipa mbunge moja kwa moja" hatuoni kwamba kuna umuhimu wa kupeleka hoja kwanza bungeni au popote panapohusika ili kuubadili kwanza utaratibu huo ili hoja ya kuzifuta iweze kupata nguvu?
 
Zitto ana nia njema lakini sidhani kama mtu unaweza kukataa sehemu ya stahili yako kama muajiriwa. Yeye angeweza kuiambia benki yake ipeleke hiyo posho kila ikiingia kule anakotaka wakati akiungana na wenzake kupigana ili hiyo posho iondolewe kwenye stahili ya nafasi ya ubunge.

Amandla......

Mkuu u are right, lakinik nadhani zitto amefanya hivyo akiamini is a right move na angeungwa mkono na wabunge wengine.
 
Hongera sana Mheshimiwa Zitto, this is the time to put your words in action. Natamani wabunge wote wa CDM wafuate mfano wako.
 
attachment.php
Alivyojibiwa sawa sawa, sasa tunamngoja Zitto atangaze aseme mimi sizitaki na kuanzia leo nisilipwe, hapo ndio tutajuwa kweli.
ishu si kusema sizitaki. Ni kuelekeza zitumike kufanya nini, na seikali/bunge ikubali kufanya hivyo, vinginevyo utamwachia fisi bucha.
 
Mhh...nadhani dhamira za kifisadi ni kubwa kuliko tunavyofikiri.Hapa ndipo utakapotofautisha kati ya wazalendo wa kweli wenye nia ya mabadiliko na wabinafsi.Zitto endelea kuonyesha njia,usitarajie kuungwa mkono na wengi.Siku zote ukweli husimama hata kama una sapoti ya mtu mmoja.Kasi ya kutaka mabadiliko inabidi iendane na vitendo dhahiri kama hivi.Bado tunahitaji kuongeza spidi,tuonyeshe dhamira yetu ya dhati katika yale tunayoyaamini
 
Mimi naona Bunge linajichanganya kwa sababu Jumanne Asubuhi wiki hii kupitia vipindi vya asubuhi vya TBC1 nilimsikia Naibu Spika Ndugai akisema kuwa kama kweli kambi ya upinzani iko serious kutokutaka posho basi waliandikie barua bunge nalo litawakata hizo posho mara moja. Sasa, nashangaa majibu haya kwa Zitto.

Kwa kauli sio za bunge tu bali kwa viongozi wengi wa chama tawala CCM serikali yake na JK kauli zao nyingi ni kauli ambazo ni za kinafiki bora lipite,zimelenga kudanganya jamii na kuipoza na hivyo ndivyo walivyo zoea na hazikua zinahojiwa matakeo yake ni matamko na kauli zinazopingana.Kwa sasa kwa umakini wa wabunge wa CHADEMA na mwaamko wa wananchi, kauli zao zinawatia matatani kama ilivyotokea kwa kauli ya JK kujivua gamba. Ilikua ni porojo za jukwaani lakini wananchi walipoivalia njuga ikabidi waitekeleze kwa shingo upande na sasa inawasumbua kwani hawakuwa wamejiandaa.Kauli ya waziri Wa fedha na mipango kutofautiana na kilichoandikwa katika bajeti yenyewe ni mfano mwingine,tofauti katika kauli za Nape na Mukama katika muda wa watuhumiwa kujivua magamba n.k.Hii inaonyesha ni kwa kiwango gani hawako makini au wanafanya makusudi ili tudanganya au wamezoea kutudanganya na mtindo wao wa kua na majibu mepesi kwa mawali mazito.HATUDANGANYIKI MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Back
Top Bottom