Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,922
- 30,271
Ndugu zangu,
Lini Tanzania ilibadili msimamo wake?
Zitto Kabwe Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ni kijana hodari mwenye kujua kuchagua maneno yake vyema.
Hapo chini ameandika masikitiko yake kuhusu Tanzania kukataa kupiga kura kulaani mauaji ya Waislam Myanmar.
Katika maandishi yake neno, ''Waislam,'' halipo.
Lakini dunia nzima inajua kuwa wanaouliwa Myanmar ni Waislam si suala la kuuliwa ''wananchi.''
Iwe itakavyokuwa Zitto Kabwe kaeleza masikitiko yake ili Watanzania wajue nini kimetokea.
Kwa sera ya Tanzania kuhusu msimamo wake wa kusimamia haki duniani kote kitendo hiki ni mabadiliko makubwa sana katika msimamo huo uliowafikisha Watanzania kupigana Msumbiji bega kwa bega na Frelimo na kutoa misaada kote kulikokuwa na dhulma sawa na kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere aliposema, ''Tunataka kuwasha mwenge uangaze kote na kuleta matumaini kule watu walikokata tamaa.''
Hii sera mpya ya kushindwa kulaani mauaji ya Waislam wanaouliwa Myanmar huenda ikawa ni sera mpya ambayo kwa sasa ndiyo inaongoza Tanzania na uhusiano wake na mataifa mengine.
Ndiyo kusema kuwa sasa Tanzania haijali tena dhulma bali inaongozwa na maslahi yake mengine ambayo kwa bahati mbaya kwa sasa hayajakuwa bayana.
Tanzania ilianza na kurejesha uhusiano na Israel uliovunjwa na Baba wa Taifa mwenyewe nusu karne iliyopita.
Leo Tanzania imeridhia kutopiga kura kwenye mauaji ya kimbari ya Waislam wa Mynmar.
Wachunguzi wa siasa wanasubiri kutazama nini lingine litafuatia.
Labda hilo litatoa mwanga zaidi kuonyesha nchi yetu imesimama upande gani na kwa nini.
Ingekuwa ni kura ya East Timor na wanaouliwa ni Wakatoliki Tanzania ingekaa pembeni ikaacha kupiga kura?
Jibu unalo wewe ndugu msomaji wangu.
Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yamezuiwa yasifanyike na kiongozi wake Sheikh Issa Ponda, Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania amekamatwa.
Ndugu zangu iwe iwavyo.
Kweli Tanzania ni ya kuwazuia wananchi kufanya maandamano ya amani kuwaunga mkono Wapalestina?
Nitaweka hapa historia ya Wapalestina na Tanganyika kuanzia miaka ya 1940 hadi uhuru unapatikana na msimamo wa Nyerere katika kuwaunga mkono Wapalestina.
Umma unasubiri.