POSHO: Bunge lamjibu Zitto Kabwe; atoa msimamo wake

What does this mean? Au alifikiri watu wanabeep walipokuwa wanataka posho ziondolewe?
Posho-Za-Vikao-Majibu-Ya-Bunge.jpg
Posho-Za-Vikao-Mhe-Zitto-Kabwe-II.jpg
it's ok kukataa posho.Ila kukataa na kuelekeza zipelekwe wapi ni kuzikataa nusu nusu.why?kwa sababu kuelekeza ziende wapi indicates you are exercising a certain right over hizo posho whilst umezikataa kwa maana ya HUZISTAHILI!Swali.Kama hustahili una haki?Naona WAZIKATAE JUMLA!
 
zitto simameni kwa pamoja kutetea hilo janga la kitaifa, coz mijitu ya magamba kama vile hawana roho.
 
Unafahamu suala linalogusa masilahi binafsi ni gumu kulitekeleza kichama, lakini ni gumu kuacha kulitekeleza kama kutofanya hivyo unakizana na dhana ya kisiasa unayoihubiri. Wachache watamwangalia na kumchambua Zito wengine wataangalia dhana hii na msimamo wa chama. Hata mimi ningependa na nataka uwe ni uamuzi wa kitaasisi kwa maana ya CDM lakini kama chama hakina kauli moja sitazuia uamuzi wa mtu mmoja moja kukataa sitting allowance.


Ndugu wana Jamii forum hivi unapokuwa kwenye nchi yako ya Tanzania ambayo bajeti yake ni kubwa kuliko mapato yake kwa asilimia zaidi ya 50, na mapato yake ni asilimia 75 ya mahitaji ya matumizi yake ya kawaida kwa mwaka, halafu kunakuwa na hela ambazo zinamlipa mtu kwa kukaa kwa muda mrefu, unategemea nini? Serikali yeti ni ya uwema wa kulipa watu kwa kukaa? Chonde sana sana wabunge walipwe DSAs na si sitting allowance. Hayo ni matumizi mabaya ya fedha za umma na Mbunge anayesimamia kidete kupinga sitting allowance yupo na wapiga kura wake. Kama tutapambana kuokoa kiasi hiki cha hela tutakua tumeokoa watanzania wangapi. Nataka kuona Rais anatofautiana na Wabunge wa Chama chake, nataka kuona waziri mkuu anakaa upande wa umma, nataka kuona tunaanza kupunguza utegemezi wa bajeti kwa kuanza na Wabunge na viongozi wa Serikali Billioni mia saba kwa kulipa watanzania wenzetu kwa kukaa ni dhambi isiyosameheka


Wenye uchungu na nchi hii tumekataa vitu hivi huko nyuma, tunakataa leo na tutaendelea kukataa, hoja si nani anaisimamia, au wangapi wanaikataa hoja hii bungeni hoja hapa ni kwa masilahi ya nani na kwa mantiki ipi?


Nakubaliana na mwenyekiti alivyosema jana kuwa hii ni hoja ya chama basi na iwe hivyo tunapenda kuona akiwaongoza wabunge wake waitekeleze mara moja.


Hiyo ni ndowano ya Chadema kwa CCM itumieni, lazima watakuja upande wenu tu hawana jinsi, wanalazimika kuingia wazimawazima kwenye chambo hicho, hiyo ndiyo tiba na usalama wao wakiikwepa wataingia kwenye chambo isiyo na huruma ambayo imeshikiliwa na isikariot na wataadhibiwa ipasavyo.
 
Hiyo hoja waliyomjibu zito haina mshiko/ Lets say Mbunge kapata safari ya kimasomo au kiafya muda mrefu nje ya nchi. Je akiandika kuomba bunge stahili za malipo yake alipwe mkewe au mumewe watagoma kwa hoja zao hizo hizo? Je sasa hivi hawafanyi haya mambo????

Majibu waliyotoa bunge ni ya Kisiasa
 
Hiyo barua haikuandikwa na wabunge wa CDM,mbona aliposusia walkout hakurepresent chama?

Aliposusia walkout walimpigia kura ya kutokuwa na imani nae ...so labda nae kaamua kufanya kivyake vyake tu.
 
We can not under estimate the importance one pillar by the presence of 3 pillars..... of course 4 pillars in totally are very crucial since they complement each other ( distribution of forces in eng.). However, we need to concur at this juncture that majority are not always right!!!!! Zitto go go on and don't bow down for the eyes can not see what the brain doesn't now..... show them for one day they gona c. PAMOJAH sana truly u have my support.
 
Hii ni changamoto ya ukweli kwa wabunge na bunge kwa ujumla! Namshauri na mbunge wa Arusha azielekeze posho zake kwenye maendeleo ya jimbo letu!
 
Nina hisi damu kuchemuka kwa jinsi hawa CCM walivyo na kiburi na wasio na huruma kwa sisi wanyonge wa Tanzania. Ingawa wazungu wanasema religion is a defense of indefensable, lakini mimi ninamulilia Mungu awaadhibu hawa CCM kwa njia yeyote ile atakayoona inafaa.

Eeeh Mungu tusikilize sisi Watanzania tunaoteseka kwasababu ya utawala dhalimu wa CCM ambao kwa ujinga wetu ndio tuliouweka madarakani. Pia tuondolee huu ujinga ili 2015 tufanye maaumzi sahihi kwaajili yetu na vizazi vijavyo.
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?
Kama ilikuwa move ya chama na yeye amekuwa wa kwanza kuitekeleza anastahili kupongezwa na sio lawama kama zako... Au ni mambo ya chuki binafsi nini? Kama sio chuki binafsi ni wivu wa kike
 
Kabla hamjaenda mbali na mjadala hii hapa chini ndiyo barua ya zitto sasa cha muhimu kwa sasa ni ku-assess kama hayo majibu ya bunge yanakidhi maombi ya Zitto. Kwa maoni yangu bunge limeplay politics at its best, maana wao kama waajiri hawampi zitto hizo posho mikonomi sasa kuna ugumu gani kuzideposit huko KDI anakotaka. After all hii haitainvolve any bunge official to do it manually. Kwamba et labda spika itabidi akapange foleni benki....... inasikitisha kuona bunge linashindwa kuaddress hata ishu ndogo kama hizi.

o5v0i0.jpg


Mheshimiwa ugumu hapa ni sheria. Bado bunge halijaweka utaratibu wa kudeposit moja kwa moja posho za wabunge( watakao penda hivyo) kwenye akaunti za watu binafsi au taasisi nyingine kwa maelekezo tu ya mbunge husika,ndio maana ameshauriwa kuchukua fedha hizo yeye mwenyewe azipeleke kwenye taasisi hiyo ya Kigoma.
 
majibu mazuri sana kwa mh.zitto.pokea stahiki zako kisheria then wewe amua pa kuzipeleka

Acha ubazazi, Mwl. Nyerere enzi zake alikwisha sema sehemu ya mshahara wake ukatwe ukajenge nchi ukakatwa-hawakuleta siasa, nchi zingine tumeshuhudia Rais ana agiza vivyo hivyo na inatendeka. Sasa hapa Tanzania kulazimishana ufisadi kwa nini?
 
Wana JF itakumbukwa majuzi Mh. Kabwe Zitto aliandika barua bunge kukataa malipo ya vikao vya posho yaani Sitting Allowance akiamini analipwa pesa asiyostahili. Hapa chini ni barua yake.
barua.jpg

Natumaini barua yake inajieleza. Bunge nalo limemjibu barua yake kama inavyoonekana hapa chini.


REPY ZITTO.jpg

Ok sasa baada ya kusoma barua Zotte unaweza kuona jinsi Mh. Zitto hoja yake ilivyotupwa kapuni indirect. Swali langu je Mh. Zitto atazipeleka posho mwenyewe hizo kama alivyokusudia?
Je majibu ya spika yamekidhi kwa mtazamo wako?
 
Kuna Barua nyingine ambayo mh zitto amekataa kulipwa hiyo posho baada ya bunge kumjibu.
 
Wana JF itakumbukwa majuzi Mh. Kabwe Zitto aliandika barua bunge kukataa malipo ya vikao vya posho yaani Sitting Allowance akiamini analipwa pesa asiyostahili. Hapa chini ni barua yake.
View attachment 31811

Natumaini barua yake inajieleza. Bunge nalo limemjibu barua yake kama inavyoonekana hapa chini.


View attachment 31812

Ok sasa baada ya kusoma barua Zotte unaweza kuona jinsi Mh. Zitto hoja yake ilivyotupwa kapuni indirect. Swali langu je Mh. Zitto atazipeleka posho mwenyewe hizo kama alivyokusudia?
Wacha tuone yetu macho, kama ana nia kweli wala asichelewe baada ya kudaka huo mkwanja wahaisha CRDB straight to KDI. Hiyo haina taabu bali ushahidi tunautaka!!!!!!
 
Zitto alifanya move mzuri. Tatizo tu ni ubinafsi. Suala hili liko kwenye mpangowa chama. Wamelihubiri kwenye mikutano yao mingi, na kama mnakumbuka vizuri alilianza Dk. Slaa akiwa mbunge. Pia limo kwenye bajeti yao mbadala ya fedha. Alikuwa na haraka gani kuandika barua peke yake, hata kabla hiyo bajeti hajaisoma (mwenyewe) wiki ijayo? Na atueleza hiyo taasisi ya KDI ni ya nani kama si yake mwwnyewe?

I like your comments. Kwa kukataa tu posho hii, huenda akawa ametoa mwanya wa posho yenyewe kutumiwa kifisadi na hao hao. Alternatively, angefuata tu ushauri wa kuichukua lakini awe na malengo ya kuiwekeza yote kwa maendeleo ya wananchi, vinginevyo itaenda kulipa posho nyingine za chama cha magamba.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom