Pongezi kwa Zakazakazi kuufafanua mgogoro wa Israel na Palestina kwa facts na kuweka udini pembeni

Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.

Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

View attachment 2779426

Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.

Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.

Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.

Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.

Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.

Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.

Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.

Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.

Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.

Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.

Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.

Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.

Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.

Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.

Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.

Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.

Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.

Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.

Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.

Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.

Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.

Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Ramani inahusika.

View attachment 2778309

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

Itaendelea...
Hapo kwenye "itaendelea" ndio Kuna mtego wafuasi wa munyaazi nawajua vizuri
 
Just to be clear:

Before Israel, there was a British mandate, not a Palestinian state.
-Before the British Mandate, there was the Ottoman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Ottoman Empire, there was the Islamic state of the Mamluks of Egypt, not a Palestinian state.
-Before the Islamic state of the Mamluks of Egypt, there was the Ayubid Empire, not a Palestinian state. Godfrey IV of Boulogne, known as Godfrey de Bouillon, conqueror of Jerusalem in 1099
-Before the Ayubid Empire, there was the Frankish and Christian Kingdom of Jerusalem, not a Palestinian state.
-Before the Kingdom of Jerusalem, there was the Umayyad and Fatimid empires, not a Palestinian state.
-Before the Umayyad and Fatimid empires, there was the Byzantine empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there were the Sassanids, not a Palestinian state.
-Before the Sassanid Empire, there was the Byzantine Empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there was the Roman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Roman Empire, there was the Hasmonean state, not a Palestinian state.
-Before the Hasmonean state, there was the Seleucid, not a Palestinian state.
-Before the Seleucid empire, there was the empire of Alexander the Great, not a Palestinian state.
-Before the empire of Alexander the Great, there was the Persian empire, not a Palestinian state.
-Before the Persian Empire, there was the Babylonian Empire, not a Palestinian state.
-Before the Babylonian Empire, there were the Kingdoms of Israel and Judah, not a Palestinian state.
-Before the Kingdoms of Israel and Judah, there was the Kingdom of Israel, not a Palestinian state.
-Before the kingdom of Israel, there was the theocracy of the twelve tribes of Israel, not a Palestinian state.
-Before the theocracy of the twelve tribes of Israel, there was an agglomeration of independent Canaanite city-kingdoms, not a Palestinian statehood.
Actually, in this piece of land there has been everything, EXCEPT A PALESTINIAN STATE!
 
Watu wanapotosha sana.
Wafilisti walikuwepo enzi na enzi zaidi ya miaka 500 kabla ya Yesu kuzaliwa.

Enzi za Ibrahimu,
MImi ni Mkristo.
Ukweli ni kwamba Wafilisti ndio
Wakaazi wa kwanza pale Kanaan/Israel.

Ona
na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti na Wakaftori.

Mwanzo 10:14
Basi wakafanya mapatano huko Beer-sheba. Abimeleki, na Fikoli mkuu wa jeshi lake, wakaondoka wakarudi hata nchi ya Wafilisti.

Mwanzo 21:32
Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Mwanzo 21:34
origin ya ibrahim ni wapi mpaka akafika hapo ugenini?
 
Hiyo ardhi awali ilikaliwa (kwanza) na Wafilisti kaka, kabla Joshua hajaamuriwa awasngamize wenyeji wote ili Israel akae.

Tukiongea uongo hata haisaidii ukristo wetu
israel alitokea wapi mpaka kufika kwenye nchi ya watu, na Mungu kumtaka joshua asiwaangamize wenye nchi wote.
 
Siyo 165,Ni 70AD destruction of the second temple and start of diaspora
Kiufupi wote hao ni wavamizi tu na best solution ni 2 state solution ambayo wapalestina hawataki.
kama wote ni wavamizi, wenyeji wa hyo nchi walikuwa nani? au nchi ilikuwa tupu?
 
Just to be clear:

Before Israel, there was a British mandate, not a Palestinian state.
-Before the British Mandate, there was the Ottoman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Ottoman Empire, there was the Islamic state of the Mamluks of Egypt, not a Palestinian state.
-Before the Islamic state of the Mamluks of Egypt, there was the Ayubid Empire, not a Palestinian state. Godfrey IV of Boulogne, known as Godfrey de Bouillon, conqueror of Jerusalem in 1099
-Before the Ayubid Empire, there was the Frankish and Christian Kingdom of Jerusalem, not a Palestinian state.
-Before the Kingdom of Jerusalem, there was the Umayyad and Fatimid empires, not a Palestinian state.
-Before the Umayyad and Fatimid empires, there was the Byzantine empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there were the Sassanids, not a Palestinian state.
-Before the Sassanid Empire, there was the Byzantine Empire, not a Palestinian state.
-Before the Byzantine Empire, there was the Roman Empire, not a Palestinian state.
-Before the Roman Empire, there was the Hasmonean state, not a Palestinian state.
-Before the Hasmonean state, there was the Seleucid, not a Palestinian state.
-Before the Seleucid empire, there was the empire of Alexander the Great, not a Palestinian state.
-Before the empire of Alexander the Great, there was the Persian empire, not a Palestinian state.
-Before the Persian Empire, there was the Babylonian Empire, not a Palestinian state.
-Before the Babylonian Empire, there were the Kingdoms of Israel and Judah, not a Palestinian state.
-Before the Kingdoms of Israel and Judah, there was the Kingdom of Israel, not a Palestinian state.
-Before the kingdom of Israel, there was the theocracy of the twelve tribes of Israel, not a Palestinian state.
-Before the theocracy of the twelve tribes of Israel, there was an agglomeration of independent Canaanite city-kingdoms, not a Palestinian statehood.
Actually, in this piece of land there has been everything, EXCEPT A PALESTINIAN STATE!
Mm nadhan Palestin ni ukanda.

Mfano tuseme ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kuna nchi kama TZ, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na S. Sudan

Au nmekosea mkuu 😎
 
Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.

Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?

Hao Wapalestina walitokea Arabia.
Halafu hao waliokua wanaitwa Wafilisti walishakua extinct, yaani walitawanyika na kuwa assimilated kwenye jamii zingine.
 
Mawazo yako ni kama yangu niliochangia sehemu flan kuhusu chanzo cha mgogoro. Watu wengi hawaanzii mwanzo wa mgogoro. Wao wanaanzia Israeli kashaingia Kanaani na kuvamiwa na warumi kisha wapalestina wakachukua ardhi yao. Sijui ni maksudi au wanasahau.

Kingine ambacho sijui, hawa wapalestina ndo wale wafilisti wa mwanzo au hawa ni wengine? Na kama sio, wafilisti wa kale masalia yao ni akina nani wa sasa?
embu tuelezeni hawa wayahudi/waisrael walitoka wapi wakaja kuvamia nchi ya watu, we want to know their origin
 
Wakatoliki wa Peramiho ni Watanzania, Wayahudi sio Wapalestina au Waarabu.
Nchi ya Israel imekuwepo karne na karne katika Historia.
Hivi wakatoliki wa peramiho leo hii wakisema wanaanzisha nchi yao hapo peramiho kwa kuwa wapo 100% wakatoliki na eneo hilo walipewa na Wajerumani walipokuwa wanatawala kimabavu basi ndiyo imeshakuwa sawa hivyo?
 
Miaka 1800+ hawakuingiliana na jamii zingine huko walikokua?.

Je Judea ile ndiyo hii nchi yote inayozozaniwa!?

Kama yesu alikua na rangi ya shaba kwanini netanyahu ni mweupe pee!?
Fujo zote za middle east ni hawa wazungu fake wanaojiita wayahudi .myahudi halisi muonekano wake upo kama mwarabu

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu taifa la Israel rasmi lilianzishwa mwaka 1948 kwa msaada wa Serikali ya Uingereza na Marekani ndio walichukua jukumu la kuwasafirisha Jews kutoka nchi mbalimbali za Ulaya kwenda Israel na hata Raman ya Nchi ya Israel rasmi imeingia ktk uso wa Dunia mnamo mwaka huo kabla ya hapo hakukuwa na taifa la Israeli duniani
Na baadae kidogo wakawachukuwa wayahudi wa nchi za Kiarabu na Persia, mwisho kabisa wakawachukuwa wayahudi wa Kiafrika, kutokea Ethiopia. Wayahudi wa Somalia walikataa kuwachukuwa, wengine wakaenda kujichomeka na Wayahudi wa Ethiopia, wengi wao wakaondoka baada ya kupata hati za kusafiria wakaingia USA na Canada.
 
Watu wengi huzihusisha dini kwenye mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Israel ni nchi moja inayokaliwa na watu ambao hawajakubaliana kuishi pamoja, wayahudi na waarabu.

Waarabu ndiyo wapalestina ambao eneo lao ni hilo lenye vidoti doti vya kijani, na sehemu iliyobaki yenye rangi ya bluu ni ya wayahudi.

View attachment 2779426

Kuna sehemu mbili za waarabu.

1. Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ambako kunatawaliwa na chama cha Fatah.

2. Ukanda wa Gaza ambako kunatawaliwa na kikundi cha Hamas.

Sehemu hizi mbili ndizo zinazounda mamlaka ya Palestina ambayo Rais wake ni Mahmoud Abbas, mwenyekiti wa chama cha Fatah.

Sehemu yenye machafuko yanayoendelea sasa ni ukanda wa Gaza.

Hili ni eneo dogo la kilomita za mraba 365, yaani ni karibu sawa na wilaya ya Ilala yenye kilomita za mraba 364.9.

Lakini licha ya udogo wake, eneo hili la lina watu zaidi ya milioni mbili waliobanana vibaya.

Asilimia kubwa ya watu hawa ni vijana wasio na ajira ambao maisha yao yote wamekuwa wakishuhudia machafuko ya umwagaji damu.

Watu hawa hawaogopi chochote kuhusu vita, huku ndiko inakotoka Hamas, yaani kikundi cha harakati za ukombozi cha kiislamu (Ḥarakah al-Muqāwamah al-ʾIslāmiyyah).

Hamas ni kikundi ambacho kimechagua vita kama njia yao ya kutafuta ukombozi kutoka Israel.

Hii ni tofauti na vikundi vingine kama Fatah, PLO na PLMA ambavyo viko tayari kwa mazungumzo na Israel kupata muafaka wa kudumu.

ASILI YA MGOGORO
Watu wengi huuhusisha na udini mgogoro huu. Yawezekana kuna udini ndani yake lakini siyo asili ya mgogoro wa Palestina na Israel.

Kujua asili ya mgogoro huu inabidi kurudi nyuma miaka zaidi ya 3000.

Picha inaanzia mwaka 63 kabla ya kuzaliwa Kristu pale dola ya warumi ilipoivamia nchi ya wayahudi na kuitawala kama wakoloni.

Wakamtoa mfalme wa wayahudi, Hasmonean na kumuweka Herod madarakani.

Wayahudi hawakukubali kutawaliwa hivyo wakapigana vita kadhaa za kutafuta uhuru.

Mwaka 165 baada ya kuzaliwa Kristu, vita kali ilizuka lakini wayahudi wakashindwa tena.

Baada ya vita hii warumi wakaamua kuwafukuza wayahudi kutoka nchi yao.

Wakaibadilisha jina nchi hiyo na kuiita Palestina.

Hili ni neno la kigiriki ambalo maana yake ni 'vunja kabisa uhusiano kati ya wayahudi na ardhi yao'.

Wayahudi wakasambaa Ulaya yote ambayo ilikuwa chini ya Warumi, na hawakutakiwa tena kurudi.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho ukristu ulikuwa unaanza kushamiri lakini warumi waliupiga vita.

Kuwa mkristu ilikuwa kosa kubwa sana ndani ya himaya ya warumi hadi karne ya nne pale mtawala wa warumi, Constantine alipoupokea.

Akausambaza katika himaya yote aliyoitawala na kuufanya ukristu kuwa dini rasmi ya warumi.

Hii ilimaanisha kwamba sasa wazungu wataanza kujifunza ukristu na katika kujifunza wakagundua kwamba kumbe wayahudi ndiyo walimuua Yesu.

Wakawachukia na kuanza kuwaua kila walipokuwepo.

Karne kadhaa baadaye himaya ya warumi ikaanguka na nchi ya Palestina pamoja na eneo lote la Mashariki ya Kati likaangukia chini ya tawala kadhaa za kiislamu za waarabu. Hapo ndipo Palestina ikakaliwa na waarabu.

Utawala wa mwisho wa kiislamu ukawa wa himaya ya Ottoman, ambayo ilianguka baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia.

Ottoman ilipigana vita ya dunia upande wa Ujerumani, baada ya kushindwa, ikanyang'anywa makoloni yake yote kama adhabu, kama ilivyokuwa kwa Ujerumani ambayo ilinyang'anywa hadi nchi yetu.

Hapo ndipo Palestina ikaangukia kwa wakoloni wapya, waingereza.

Mauaji ya wayahudi Ulaya yakasababisha kuzaliwa kwa harakati za kuwarudisha kwao na kuanzisha taifa lao, zilioitwa Zionism.

Harakati hizi zikaitikiwa vizuri na wayahudi wote duniani, wakanza kurudi Palestina.

Hii ikasababisha vurugu kati ya waarabu waliokuwa wakiishi pale na wayahudi waliokuwa wakirudi.

Vurugu hizi zikawafanya wakoloni waingereza kusimamishela harakati za wayahudi kurudi.

Nchini Ujerumani ikiwa inaongozwa na Hittler, Wayahudi milioni 6 waliuwawa kinyama (Holocaust), Kama Vita vya Pili vya Dunia havingeisha ama Mjerumani angeshinda na kuitawala ulaya basi wayahudi wote wangeuliwa Ulaya, Mauaji haya ya kutisha ya Ujerumani dhidi ya wayahudi yakarudisha tena harakati zile.

Kadri wayahudi walivyokuwa wakirudi ndivyo vurugu baina yao na waarabu zikaongezeka.

Mwaka 1947 umoja wa mataifa ukaandaa mpango wa kugawa ardhi ya Palestina ili kuwe na mataifa mawili, la waarabu ambalo litaitwa Palestina na la wayahudi ambalo litaitwa Israel.

Mji wa Jerusalem ukaachwa kama ukanda huru kutokana na umuhimu wake katika dini zote tatu za eneo lile.

Ramani inahusika.

View attachment 2778309

Waarabu wakaukataa mpango huu lakini wayahudi wakaupokea na kuanzisha taifa lao, na waarabu kujikuta ndani ya taifa hilo.

Itaendelea...
Shida ni kwamba Hamas alianzishwa na kuwa supported na Israeli ili kupambana na PLO ya Arafat. So wanavuna walichopanda or mipango Yao bado Inaendelea kuwatumia ili wavamie GAZA strip kiescelate mambo.
But nachoona ni mpango tu WA WW3. coz siamini kuwa intelejensia ya Israeli haikuona hii (???????) "ingawa Kuna taarifa kuwa misri walijua na wakawaambia but makamanda WA Israeli wakauchukuna hawakumwambia Netanyau.
MI naona plan ya WW3 iko tayari kitufe kimebonyezwa.
Arabs and Hao fake Israeli wapigane mpk wawe hoi. And waulize upepo Wa propaganda za kidini so nchi nyingine zaidi ziingie vitani kila mtu akichagua upande ili iwe rahisi Kuleta Dunia Yao MOJA.
SO tutegemee mtu atapigwa nuclear soon ili kuliamsha mazima. Kama sio Ukraine basi hapo Middle Eeast.
Naomba tu nchi zangu za kiafrika zisiingie kwenye huu mgogoro maana hautuhusu. Tusipeleke kaka zetu wakafa kama walivyopigana vita ya 1 Na 2 ya dunia. Ingawa Najua puppets wengi Africa so nako tutapelekwa kama mapazia.
 
Bora hata na wewe umeongea ukweli.
Muingereza anapaswa kulaumiwa kwa hili. Aliwapatia ardhi watu wasio takiwa kwenye ardhi hiyo.

Bora wangepewa Uganda
Sehemu ya Palestina ilikuwa ni ardhi ya Wa-Israeli ya muda mrefu tu.
 
Abraham/Ibrahim aliishi wapi
Watoto WA Abraham/Ibrahim ni Akina Nani.
Makabila yaliokuwepo huko ni yapi.
Kuna makabila 12 ya wayahudi ni yapi.

Wayahudi walivyokwenda utumwani Misri , nchi Yao ilikaliwa na Nani.

Walivyo Rudi toka utumwani waliishia wapi , na nchi ya ahadi ilikuwa ipi.

Hii itakuwa agano la kale .

Na baada ya agano Jipya kuondoka Kwa wayahudi ilikuwaje na nchi Yao ilitwaliwa na Nani.
maswali mujarabu kabisa, watu wanaelezea kana kwamba kuna watu walikuwa na makazi angani makakulia huko na baada ya kuwa watu wazima ndo wakashushwa ardhini
 
Back
Top Bottom