Leo Palestina imepigiwa kura 143 za kuwa mwanachama wa umoja wa mataifa

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,314
3,443
Leo Palestina imepigiwa kura 143 za kuwa mwanachama wa umoja wa mataifa

Kura 9 ikiwemo ya Marekani na Israeli zimekanusha, na wanachama 30 hawajapiga kura. Hii ni harakati ya kuifanya Palestina kuwa nchi kamili na mji wa Yerusalem kuwa mji huru naam mji mkuu wa dini kuu tatu (Uyahudi, Ukristo na Uislamu).

Israeli itaenda kupoteza sehemu ya maeneo kwajili ya taifa la Palestina. Sasa ni ngumu kueleweka sababu ya sera ya Marekani inayopinga taifa la Palestina kupitia ushawishi wa Waevangalical. Lakini Vatican na Umoja wa Ulaya wapo upande wa taifa la Palestina na wakiwa na mlengo wa kuifanya Yerusalemu mji mkuu wa kimataifa chini ya Vatican. Na hilo ni moja ya agano kati ya Vatican na Waislamu.

Kamwe huwezi sikia Vatican inaunga mkono mji wa Yerusalemu kuwa upande wa Wayahudi. Umoja wa mataifa unatambua kuwa mlinzi wa Yerusalemu ni Vatican na Ufaransa (makruseda) ambao daima wameugombania mji huo kwa mamia ya miaka.

Huwezi elewa hili jambo kwa sasa, ila unaweza pitia makala mbili ambazo nimezishare hapa, nitaziweka kwenye comment. Moja nimeiandika 2019 na nyingine 2023. Katika makala hizo mbili nimegusia machache yaliyo nyuma ya mchakato mzima ambao leo katika UN sura yake imeanza kuwa wazi. Hakuna matukio ya ajali duniani, kila kitu kinamatokeo yake. Vita vya Gaza goal lake ni kuvuruga akili za walimwengu ili waweke huruma kwa Wapalestina waliotolewa kafara pamoja na Wayahudi.

End justifies the means.

Na kama utakuwa na swali katika hili au baada ya kusoma makala hizo utauliza.

Na Jeff Massawe.
FB_IMG_1715453428015.jpg
 
Post yangu ya siku za nyuma

Kuhusiana na mpinga Kristo

Yerusalemu au Roma?

Kwa mujibu wa imani ya Kiprotestant (akiwemo Martin Luther, Huss na Kelvin nk) "mpinga Kristo" anatokea Roma na yupo tayari, Ila kwa mujibu wa Wajesuits Francisco Ribera na Bellmine ni kwamba mpinga kristo atatokea Yerusalemu huko mbele ya nyakati (Futurism doctrine) akitawala ndani ya Hekalu la Kiyahudi. John Darby msaliti wa imani ya Kiprotestant aliinuka na kunakshi somo la mpinga kristo atokeaye baadae huko Yerusalemu na kuongeza habari za unyakuo wa siri. Somo lake linajulikana kama "Ugawaji" yaani Dispensationalism. Theolojia ya Ugawaji inaiweka Israeli juu ya Kanisa la Mungu. Theolojia hii sasa linaaminiwa sana na Waevangalical wa Marekani na sehemu kubwa ya Wapentekoste na sehemu ya Waprotestant ingawa sasa baadhi ya wahubiri wa maeneo hayo wameanza kulitilia shaka. Dispensationalism ndio inaunda Wakristo wa Kizayuni (Zionism Christian) kundi lenye nguvu sana. Biden rais wa Marekani, alisema si lazima uwe Yahudi ili uwe Mzionisti. Hawa Wazayuni ndio wanasukuma juu ya ujenzi wa Hekalu la tatu na wametoa pesa nyingi sana juu ya ujenzi huo. Na NetanYahu amechaguliwa kusimamia ujenzi. Ukitaka ushahidi nitakupa.

Mimi nakubaliana na msimamo wa wanamatengenezo kuhusiana na "mpinga kristo". Hivyo basi hiki kinachofanyika hapo Yerusalem ama juu mgogoro wa Israeli na Palestina ni moja ya ajenda ya kusukuma injili ya Francisco Ribera na John Darby. Haikihusiani na unabii wa Daniel ama Ufunuo. Dunia nzima imetazamishwa Yerusalemu badala ya Roma.

Je wewe upo na Wanamatengenezo ama upo na Wajesuits kuhusiana na mpinga kristo?

Pichani ni Kiongozi wa mamlaka ya Palestina (PLO) bwana Yesse Arafat akiwa na Papa Yohana Paulo 2 mnamo August, 2001 kule Vatican. Wakiongea juu ya mgogoro wa Palestina na Israeli. Askofu wa Roma alimuambia yeye anasimama na msimamo wa kuunda mataifa mawili (Palestina na Israeli) na Yerusalemu ibakie kuwa jiji la kimataifa (mamlaka huru) ambayo itahudumu dini kuu tatu na si taifa la Kiyahudi pekee.

Na Jeff Massawe
The Watchman
0757-722557
 
Hii niliandika mwaka 2019

JE WAJUA?

Wayahudi waliteseka sana na kuuawa sana katika nchi za Wakristo kuliko katika nchi za Waislam. Kuna kipindi walifukuzwa kabisa Ulaya na kukimbiia Afrika ya Kaskazini na mashariki ya kati ambako kulikuwa na utawala wa Kislam. Na kuna kipindi walishirikiana na Waislam kupambana na jeshi la msalaba lililokuwa linaongozwa na Papa Urban kwajili ya kuiteka Yerusalemu, tendo hilo lilifanya Wayahudi kuteswa na kuuawa kinyama kama wapinga Kristo.

Point ni kwamba; Wakristo wasijenge chuki sana na Waislam sababu ya kupingana na Wayahudi kwa mtazamo wa dini na nchi ile ya Ahadi, Yesu hakufundisha chuki bali UPENDO ambayo ndio sheria mpya ya kanisa. Kihistoria Wayahudi walitengwa sana na Wakristo kuanzia zama za Kostantino; leo Wayahudi wamekuwa vipenzi vya Wakristo mpaka na wao(Wayahudi) wanashangaa ingawa bado wengi hawana imani na Wakristo. Na Wakristo nao wameenda mbali zaidi kwa kutafuta baraka kwa njia ya kuwabariki Wayahudi, tendo ambalo Yesu na Mitume wake hawakulifundisha wala kuliamuru.

Kuna chuki ambayo imepandikizwa baina ya dini tatu, Dini ya Kiyahudi, Kikristo na Kislam na kiini cha chuki hii ni mji wa Yerusalem. Na hitimisho la chuki hii, ni Yerusalem kuchaguliwa kama mji wa dini tatu kuu, na mpatanishi atakuwa ni Papa. Israeli itakuja kuwa CORPORATION STATE, mpango huo ulianza kwa Ignatius Loyola, na Napoleon Bornapatre akaanzisha hatua, na Serikali ya Uingereza ikafanikisha mchakato, na Papa atahitimisha mpango mzima. Dunia nzima itakuwa na amani ya mda mfupi.

Wakati Trump anatangaza kuitambua Yerusalem kama mji mkuu wa Israel. Papa Francis aliungana na umoja wa Waarabu, na umoja wa Ulaya na umoja wa mataifa kupinga mpango wa Trump. Papa alisema.....

"Yerusalemu ni jiji la pekee, takatifu kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu, wanaoheshimu maeneo yao matakatifu ya dini zao huko, na mji huo una hisia maalum ya amani," Papa alisema.

"Ninamwomba Bwana kwamba utambulisho huu uweze kuhifadhiwa na kuimarishwa kwa manufaa ya Mashariki ya Kati na ulimwengu wote," akasema, "na kwamba hekima na busara vinashinda, ili kuepuka kuongeza mambo mapya ya mvutano "

Katika picha ya kushoto mwa post, ni Papa na Iman mkuu wa Palestina Ahmad Al-Tayyib wakiwa Yerusalem katika eneo la Dome of the Rock. Papa alimwahidi Imam kwamba atapambana kuhakikisha kutakuwa na suluhisho la nchi mbili. Papa Francis alizidi kujizolea umaarufu na wapenzi huko Palestina na katika nchi za Waislam na Waarabu, sasa anaonekana ni mtu mwenye kutaka maslahi mapana ya wengi na amani ya dunia.

Na picha ya kulia mwa post ni Papa Francis na Rabi Abraham Skorka na Iman Omar Abboub, wakiwa katika ukuta wa kulia machaozi Yerusalem. Hao watatu ni marafiki wa utotoni, na sasa ni viongozi wakubwa duniani, na wamepatana kuleta umoja wa dini tatu kuu.

Umejifunza nini?
 
Sasa ndio naamini roma catholic ilianzisha uisilamu ili kupunguza nguvu ya ukrsto
 
Back
Top Bottom