Pongezi kwa Walimu wote wa Kibaha High School

Pongezi kwa Walimu wote wa Kibaha High School

Hamna cha maana sikuhizi pale kibaha sec zamani ndio walikuwa wanalipwa vizuri na hata wafanyakazi wa TUMBI HOSPITAL walikuwa wanalipwa vizuri siku hizi hamna kitu mishahara ni ileile ya kawaida! SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA Linaelekea kufilisika ufisadi, miradi mingi imekufa hamna cha maana pale

Weka data kamili Wewe kijana spesho skuli tangu O'level na ukapiga One kali saaana
 
Muongo wewe iyo ilikuwa ni zamani! sikuhizi KIBAHA EDUCATION CENTRE(1970) mishahara ni ileile nina ndugu yangu pale ni DAKTARI wa tumbi hospital

Wewe hauaminiki tena,labda wakusafishe kwa Semen.
 
Weka data kamili Wewe kijana spesho skuli tangu O'level na ukapiga One kali saaana

Mkuu bado tu unamkomalia dogo mbona kashakua mpole muda? Nasikia na yale mapicha kule fb kayang'oa yote?
 
Jaman Kibaha boyz tupo wengi,nilikuwepo enz ya headmaster mwampaja,mama luhaga,luhaga,festo urio,mama kisanga,kaselenge,rizik majala,kashindye,mwl wa GS alikuwa kipofu. Ila ukweli Kibaha imeshuka sana hadhi yake kwa matokeo mabovu. Ila kuhusu walimu wanawalipa vizuri sana. Kuhusu madaktari wanalipwa vizur,kwa kifupi mfanyakazi wa shirika la elimu Kibaha mambo safi.
 
Mwaka jana kama mwezi wa 10 hivi,kuna kipindi kilikuwa kinazungumzia Shirika la Elimu Kibaha
 
Mwaka jana kama mwezi wa 10 hivi,kuna kipindi kilikuwa kinazungumzia Shirika la Elimu Kibaha

Basi itakua kilichukuliwa long time kuna skendo flan hv ilimwondoa pale now anafundisha English Tumbi
 
Shule yangu ya zamani hii...

Sijui kama waalimu wote wa wakati huo kina Abacha, Kashinde, Majala, Festo Urio, Mgina, Zuberi n.k kama wapo hapo


Umenikumbusha huyo ndugu Kashinde Kaselenge....lol!!

Hivi na mama Mbalawa bado yupo?? Maskini mwalimu Mbalawa alifariki akingali kijana...RIP!
 
Hamna cha maana sikuhizi pale kibaha sec zamani ndio walikuwa wanalipwa vizuri na hata wafanyakazi wa TUMBI HOSPITAL walikuwa wanalipwa vizuri siku hizi hamna kitu mishahara ni ileile ya kawaida! SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA Linaelekea kufilisika ufisadi, miradi mingi imekufa hamna cha maana pale

Wee umesema kweli, Mishahara ya shirika la elimu siku hizi ni sawa na serikalini, hapo palianza kuharibika kiutawala na kiuchumi toka pale Mkurugenzi mpya alipoingia akiitwa Mr Swai..pakawa na umbeambea wa kumwaga kama ----- na ndipo wafanyakazi wengi wakaanza kuondoka au kupachukia wakati huo huo Swai mwenyewe akiwa hajali nini kinatokea bali kazi yake kubwa ilikuwa ni kukusanya vyake harakaharaka ili atayarishe nyumba ya kwake kule porini njia ya Mlandizi, leo hii yupo bwana mmoja (Dr Mpemba?) nafikiri yeye ndio kaletwa pale KEC kuja kusoma hitima ya mwisho kwani kapangua pangua watendaji makini na kuweka watu wake ambao hawajui lolote na si wabunifu, angalia mwalimu makini aliyeiletea sifa Secondary (Mathematics) ya Kibaha yupo frustrated na anataka kuacha kazi sababu ni kupewa visharti vya kijinga jinga na bwana huyu achilia mbali kapelekwa kwenye ile shule ya Day pale pembezoni, ukienda Hospitali ndio kabisaa imekuwa sawa na haina tofauti na Mwananyamala Hospital, sio ile Tumbi Hospital ya Dr Mtei tena,

Ukweli KEC inakufa taratibu, Wapi maziwa tuliyokuwa tunaletewa mpaka mlangoni? wapi wale kuku tuliokuwa tunauziwa kwa bei nafuu kila week end? Wapi miradi ya ng'ombe waliokuwa wametapakaa pale tumbi mpaka kule Sofu? Wapi miradi ya Nguruwe?, Wapi mitambo ya kutengeneza chakula cha kuku? Kibaha ilikuwa inauza na inapeleka vifaranga mpaka Zambia leo hata Dar haileti vifaranga vyake tena kule Vigunguti...

JE SHIRIKA HAPO BADO LIPO AU KILICHOBAKI NI ULAJI TU?
 
nashindwa hata nichangie nini. tuliopo sasa hivi ni masitiko, kibaha si ile nliyokuwa naisikia nikiwa o'level. hakuna kuku, maziwa, mayai wala vifaranga. ufundishaji dah! hata shule yangu benjamin inawazidi pakubwa. juzi juzi dawasco walikata maji, shirika lilikuwa linadaiwa. wazabuni wa chakula walikataa kuleta chakula akabaki 1 tu aliyejitolea. kifupi ni hali ni mbaya.
 
Back
Top Bottom