Pongezi kwa Walimu wote wa Kibaha High School

Pongezi kwa Walimu wote wa Kibaha High School

Pest

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2014
Posts
216
Reaction score
144
Ukweli hawa jamaa wapo vizuri, wanaajiriwa kwa kutumia njia nzuri tofauti na njia wanayotumia wizara ya elimu. Huweza kuajiriwa kwenda kufundisha shule hii bila kusailiwa na sekretarieti ya ajira na miongoni mwa shule ambazo za shirika la umma ambalo lipo chini ya ofisi ya waziri mkuu.

Naomba wizara ya elimu iige mfumo wa kuajiri walimu kutoka shule hìi, mnapeleka walimu wengine wabovu kabisa.

Hongereni walimu wa Kibaha kazi zenu zinaonekana kwenye matokeo.
 
Mishahara inatofautiana mkuu pakubwa sana,mwalimu wa diploma wa pale anamzidi wa degree tamisemi
 
Ukweli hawa jamaa wapo vizuri,wanaajiriwa kwa kutumia njia nzuri tofauti na njia wanayotumia wizara ya elimu.huweza kuajiriwa kwenda kufundisha shule hii bila kusailiwa na sekretarieti ya ajira.na miongoni mwa shule ambazo za shirika la umma ,ambalo lipo chini ya ofisi ya waziri mkuu.naomba wizara ya elimu iige mfumo wa kuajiri walimu kutoka shule hìi,mnapeleka walimu wengine wabovu kabisa,ongereni walimu wa kibaha kaz zenu zinaonekana kwenye matokeo

Hamna cha maana sikuhizi pale kibaha sec zamani ndio walikuwa wanalipwa vizuri na hata wafanyakazi wa TUMBI HOSPITAL walikuwa wanalipwa vizuri siku hizi hamna kitu mishahara ni ileile ya kawaida! SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA Linaelekea kufilisika ufisadi, miradi mingi imekufa hamna cha maana pale
 
Mishahara inatofautiana mkuu pakubwa sana,mwalimu wa diploma wa pale anamzidi wa degree tamisemi

Muongo wewe iyo ilikuwa ni zamani! sikuhizi KIBAHA EDUCATION CENTRE(1970) mishahara ni ileile nina ndugu yangu pale ni DAKTARI wa tumbi hospital
 
Walimu wa degree wanaanza na ptss11 ambayo sh.milion moja na laki 2,diploma wanaanza na laki 64OOO0,acha kubisha vitu huzivyo vijua ,
 
Wafundishe sasa waache utani maana bongo elimu mziki mwingine, hasa sayansi, wako shallow vby..
Ila kibaha hiyo unayoisema siku hizi mbona ina tokeo la kawaida sana tu, shule special naona iliyobaki Mzumbe tu, yenyewe ndio inaongozea shule za serikali kila mwaka kwenye hii miaka ya hivi karibuni... japo na yenyewe imechakaaaa, majengo, walimu..
 
Pale kuna madaktari wa aina mbili,wa shirika na halmashauri,huyu ndugu yako yupo halmashaur ,daktar wa shirika yuko,juu.kama walimu wa degree wanaanza na 1milion na lak 2,je daktari? Acha ubish,tunawatu wapo pale wanafanya kazi.
 
Muongo wewe iyo ilikuwa ni zamani! sikuhizi KIBAHA EDUCATION CENTRE(1970) mishahara ni ileile nina ndugu yangu pale ni DAKTARI wa tumbi hospital
pale kuna madaktari wa aina mbili halmashauri ambao mishahara yao midogo kama ndugu yako na wanaajiriwa na shirika ambao wako juu,siku ukienda pale kuna magari yenye no.sm ambayo ya halmashaur na su.ambayo ni shirika.watu wanakula pesa kubwa wewe chechemea na vijisent vyako na mikopo iliyokidhiri.kiufupi na nenda kaulize kote huwezi kulinganisha mtumishi wa halmshaur na shirika au taasis,halmashaur wana vijimishahara,thanx
 
Shule yangu ya zamani hii...

Sijui kama waalimu wote wa wakati huo kina Abacha, Kashinde, Majala, Festo Urio, Mgina, Zuberi n.k kama wapo hapo

watu8 kumbe vijana wa Kibaha tupo jeshi Kubwa! mie nilikuwepo enzi zile mkuu wa shule akiitwa Msaki,baadaye Adel Mwampaja naimiss Kibaha shule yangu.
 
Shule yangu ya zamani hii...

Sijui kama waalimu wote wa wakati huo kina Abacha, Kashinde, Majala, Festo Urio, Mgina, Zuberi n.k kama wapo hapo

Wengine wamestaafu mkuu ila Majala na Festo Urio wapo na festo Urio amekua Mkuu wa shule ya sekondary Tumbi...

Daah mkuu umenikumbusha mbali enzi za hisabati za urio...

Hivi kayenga ulimwacha?
 
watu8 kumbe vijana wa Kibaha tupo jeshi Kubwa! mie nilikuwepo enzi zile mkuu wa shule akiitwa Msaki,baadaye Adel Mwampaja naimiss Kibaha shule yangu.

Mwampaja alipanda cheo akawa meneja hiduma za elimu wa shirika na sasa amestaafu...

Dah mkuu ulimaliza mwaka gani?
 
Naam Kayenga alikuwepo mkuu na baadaye akaukwaa Ukuu wa Shule na makamu wake akawa Kachingwe Kaselenge.

Wengine wamestaafu mkuu ila Majala na Festo Urio wapo na festo Urio amekua Mkuu wa shule ya sekondary Tumbi...

Daah mkuu umenikumbusha mbali enzi za hisabati za urio...

Hivi kayenga ulimwacha?
 
Nilikuwepo hapo nyakati za Mr. Mwampaja lakini baadaye akapandishwa cheo na kupelekwa kwenye Idara ya Elimu ya Shirika.

watu8 kumbe vijana wa Kibaha tupo jeshi Kubwa! mie nilikuwepo enzi zile mkuu wa shule akiitwa Msaki,baadaye Adel Mwampaja naimiss Kibaha shule yangu.
 
Mwampaja alipanda cheo akawa meneja hiduma za elimu wa shirika na sasa amestaafu...

Dah mkuu ulimaliza mwaka gani?

Mkuu huyu mkuu wa Shule alikuwa mzuri sana tulikula kuku sana,maziwa kwa sanaa, walimu wa kumwaga nilikuwa nasoma kama nimetumwa na kijiji.
 
Naam Kayenga alikuwepo mkuu na baadaye akaukwaa Ukuu wa Shule na makamu wake akawa Kachingwe Kaselenge.

Kaselenge kashushwa cheo na kuwa mwalimu wa kawaida pale Tumbi Secondary
 
Back
Top Bottom