Pongezi kwa Rais Samia. Hadi sasa ametoa ajira nyingi sana japo hitaji ni kubwa

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,664
18,039
Kwa kweli hatuna budi kumshukuru sana Mungu kwa ajiri ya Rais wetu kuweka mkazo katika kutoa ajira kwa vijana wetu waliomaliza vyuo.

Japo hitaji bado ni kubwa sana lakini hatuna budi kumpongeza kwa wingi wa ajira ambazo keshatoa hadi sasa. Si mnakumbuka tangu 2015 ajira zilikata kabisa.

Kilikuwa ni kipindi cha kufunga mikanda ili mambo mengine pia yaliyokuwa yamekwama kwa muda mrefu yaweze kutekelezeka kama vile kuhamishia makao makuu Dodoma, reli standard gauge, bwawa la mwalimu Nyerere nk.

Tutabaki tunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya JPM kwa kukwamua mambo hayo kwa kipindi chake!! Mungu alikuwa mwema kwetu kipindi na anaendelea kuwa mwema sasa, Jina la Bwana libarikiwe!!

Nakumbushia tu kuwa zitamwagwa ajira zaidi ya 43,000 mwaka wa fedha ujao wa 2023/2024!!
 
Bado Kuna kundi kubwa linahitaji ukombozi wa fikra katika taifa hili

"Idi ni j,mosi mwaliko
Enzi za mzee Ruksa, sikukuu ikiangukia weekend (jumamosi au jumapili) lazima ifidiwe jumatatu!! Mzee Ruksa alitupa raha na vionjo fulani ambavyo tunavimiss sana!!
 
Back
Top Bottom