Rais Samia ni jasiri mpambanaji

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,740
Ndugu zangu Watanzania,

Wakati wenzetu Wakenya kwa sasa wanakabiliwa na Tatizo la Bei kubwa ya Nishati ya mafuta kuwahi kutokea na kushuhudiwa katika Taifa lao, wakati kukiwa na Tishio la mfumuko wa bei ya bidhaa nchini Kenya, wakati Nauli zikipanda nchini kenya,wakati wakenya wakikabiliwa na hali mbaya ya upatikanaji wa chakula na kwa bei kubwa hasa unga, wakati uchumi wa Kenya ukitetereka na manung'uniko yakisikika na kuongezeka kila kona ya kenya juu ya ugumu wa maisha na kupanda kwa bei ya maisha nchini Kenya yanayopelekea kufanyika kwa maandamano ya mara kwa mara. Hali ni tofauti kwa Tanzania.

Hali kwa Tanzania ni njema, ni yenye kuleta matumaini,ni yenye kuonyesha kesho iliyo njema na bora zaidi ya leo na jana. Ni yenye kuvutia na kuibua fursa kila iitwayo leo. Hii yote ni kutokana na ujasiri na upambanaji wa Rais samia anao ufanya kila leo usiku na mchana ili watanzania Tuishi kwa amani na utulivu. Hii ndio maana tunaona kwa upambanaji wake imepelekea bei ya nishati ya mafuta kuwa ni ile isiyo muumiza mwananchi ukilinganisha na Nchi kama kenya.Hii ndio maana tunaona hatuna mfumuko wa Bei za bidhaa muhimu kama vile vyakula hususani Unga,mchele na maharage, hii ndio maana tunaona leo hii miundombinu ikijengwa na kupangwa kujengwa kila mahali kama ilivyo mipango ya kujengwa kwa km 237.9 za barabara za njia nne kutoka igawa Mbeya hadi Tunduma mkoani Songwe.

Ndugu zangu Watanzania kama tungeona maisha wanayoishi majirani zetu au kusikiliza katika vyombo vya habari hali ya kiuchumi wanayopitia majirani zetu, kwa hakika tungepigaa magoti kwa unyenyekevu kumshukuru, kumpongeza, kumpa faraja na kumtia moyo Rais wetu kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa letu. Wengine husema kuwa kwanini tumpongeze wakati anatumia kodi zetu?

Jibu ni kuwa kama angekosa mipango na kuwa na uchungu na maisha ya watanzania angeweza kutapanya kila kitu na kila senti iliyokusanywa kwa mambo yasiyo na tija kwa mtanzania na yasiyo Gusa maisha yake moja kwa moja wala kumsaidia katika kupata milo mitatu iliyo bora au kupata matibabu bora au ajira kwa watoto wake.

Lakini Hii ndio maana ya wenye akili kuanzisha hata kwa Tuzo katika kuwapongeza watu wanaofanya vizuri katika maeneo yao ya kazi katika kuleta matokeo chanya katika maisha ya watu wengi.Ndio maana kuna Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia japo hachezi peke yake uwanjani na Tuzo zingine nyingi tu.

Hivyo Watanzania hatuna budi kumpongeza Rais wetu,kumtia moyo na kumpa faraja kwa kazi ngumu aifanyayo katika kututumikia Watanzania. Embu angalia katika ziara yake ya mikoa ya kusini huko namna alivyo fanya kazi kubwa yakiuwekezaji katika kuwafikishia huduma wananchi,ikiwepo kuwajengea hospitali kubwa ya Rufaa kanda ya kusini Mtwara, miradi ya Maji, kuwapelekea pembejeo wakulima kwa wakati, miundombinu ya barabara,uboreshaji wa bandari unaorahisisha usafirishaji wa mazao ya mkulima hasa korosho katika kufika haraka sokoni.

Kila Eneo utakalo angalia na kutupia jicho lako lazima uone kazi za mh Rais, lazima ukute alama zake,lazima ukutane na mikono yake,lazima ukutane na uwekezaji wa serikali yake,lazima uguswe na serikali yake na kufikiwa kihuduma. Zote na yote hayo ni kutokana na ujasiri wake pamoja na upambanaji wake katika kuhakikisha kuwa watanzania tunapata huduma bora,kuhakikisha ya kuwa serikali inamsaidia kila mwananchi mwenye kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa kuweza kupiga hatua za kimaendeleo, kuhakisha kuwa serikali haimkwamishi mtu katika kutimiza ndoto zake.

Ndio maana serikali inatoa Elimu bure ili kila kijana afikie ndoto zake,inatoa Ruzuku ya mbolea ili kila mkulima alime kulingana na ndoto zake, inatoa maelfu ya ajira ili vijana walitumikie Taifa lao,inaboresha miundombinu ili watu wasafiri na kusafirisha bidhaa bila shida, inatoa maji safi na salama ili watu wasidamke usiku usiku kutafuta maji na kuhatarisha maisha yao,inapeleka umeme kila mahali ili kuibua fursa mpya za ajira kwa vijana na kukuza na kuongeza miji midogo itakayo kuwa kichocheo cha biashara.

Inalipa mishahara kwa wakati kwa watumishi wa umma na kuwaongeza nyongeza kila mwaka ili wafanye kazi kwa amani na wakijitoa na kujitolea katika kutoa huduma bora kwa watanzania wafikao katika ofisi zao.

Pamoja na upambanaji wote huu wa Mh Rais wetu mpendwa wapo watanzania wachache wenye upofu wa akili na wenye kukosa adabu ,heshima na staha unakuta bado wanakashifu na kusema hakuna kilichofanyika na kinachofanywa na mh Rais wetu na serikali yake,kwamba hatusongi mbele kwa lolote.

Yote hii wanafanya ni kwa chuki tu binafsi kwa mh Rais ni kukosa tu shukurani na kutambua mchango wa mtu pale awapo madarakani,ni aina tu ya watu ambao wao ni wa kupinga kila kitu na kila jambo ilimradi tu linafanywa na serikali.wapo wengine bila kupinga na kuishambulia serikali hawawezi kupata misaada kutoka kwa wafadhili wao ,hivyo kula yao ni kuporomosha matusi na kejeri kwa serikali,ni kuitukana na kuisema vibaya serikali wakati wote,ni kuichonganisha serikali na wananchi wake muda wote.

Hivyo watanzania tuendelee kumuunga mkono mh Rais katika kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwa taifa letu, Tuendelee kumuombea kila mtu kwa imani yake ili Mungu wetu aliye hai na aishiye siku zote aendelee kumlinda, kumpigania, kumtetea na kumpatia nguvu na afya njema ya kuendelea kututumikia watanzania. Tusimkatishe Tamaa mh Rais wetu bali tumpe faraja. Siyo lahisi na jambo jepesi kupata viongozi wenye uthubutu ,uchapakazi aina ya Rais samia,watu aina yake hawazaliwi kila siku na hawapatikani kila mahali.

Watu aina ya Rais samia wenye uwezo wa kumsikiliza kila mtu na kukaa mezani na kila mtu na kumsikiliza ni wachache sana,watu wenye uvumilivu ,subira na moyo wa utulivu kama Rais samia ni wachache sana Dunia, watu wenye madaraka makubwa ya Urais kama aliyo nayo Rais samia kikatiba na kisheria na Bado wakajishusha na kujinyenyekeza kwa watu ni nadra sana kuwapata. Rais samia ni zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Nimejaribu kutuma pesa kwenye namba yako lkn mtandao unasumbua kama vipi tupe namba nyingine ya M-PESA
 
La ovyo. Anapambana na nani?

Tumia akili basi. Teuzi zilishaisha. P** bavu
Hapana ndugu yangu mimi siandiki kwa ajili ya kutafuta uteuzi hapa ,maana kama hilo ndio lingekuwa lengo basi ningekuwa nilisha kata Tamaa na kuacha kuandika hapa jukwaani kwa kuishiwa pumzi,lakini kwa kuwa naandika kwa uzalendo ndio maana nipo na nitaendelea kuwepo kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyojalia uzima na uhai.
 
Njia yako ya kutafuta pesa sio salama mkuu maana Hawa viongozi Wana usemi wao "Kill the dog after the hunting is over" uchawa sio deal
Sitafutii pesa hapa jukwaani maana siyo ofisini hapa au shambani .Najitafutia pesa kwa kufanya kazi shambani kwa juhudi, maarifa na bidii pasipo kubweteka au kusubiri fadhila .
 
Sifa unazotoa kwa serikali iliyofeli hata Samia mwenyewe anakuona ni sawa na dunderhead sababu sifa hizo hana.

Nenda uone kule waziri wa afya kafunga comments kule kwenye mtandao wa twitter na Samia huyo huyo aliwahi kiri kuwa twitter republic ni tishio kwa utawala wake sababu watu wanashusha hoja zenye nguvu sio mapambio kama unayoleta hapa.

Mjadala wa bima umefanya waziri kawafungia watu vioo sasa je hujiulizi waziri anaposhindwa kujibu maswali anakimbilia kupiga komeo mlangoni.
 
Sifa unazotoa kwa serikali iliyofeli hata Samia mwenyewe anakuona ni sawa na dunderhead sababu sifa hizo hana.

Nenda uone kule waziri wa afya kafunga comments kule kwenye mtandao wa twitter na Samia huyo huyo aliwahi kiri kuwa twitter republic ni tishio kwa utawala wake sababu watu wanashusha hoja zenye nguvu sio mapambio kama unayoleta hapa.

Mjadala wa bima umefanya waziri kawafungia watu vioo sasa je hujiulizi waziri anaposhindwa kujibu maswali anakimbilia kupiga komeo mlangoni.
Wengi wao huwa hawatoi hoja bali huporomosha matusi tu.
 
Wengi wao huwa hawatoi hoja bali huporomosha matusi tu.
Una uhakika kwahiyo watu wote mitandaoni wanatukana?

Mbona post za kusifia hazifungii comments?

Waziri analeta siasa kwenye masuala yanayogusa watanzania wengi kwa pamoja hata walio wa chama chake nao wanavurumisha maswali ambayo hajayatolea majibu.

Mjadala umekuwa mkali waziri kaonyesha uwezo duni kama boss wake kaamua kupiga kufuli.
 
Kama kweli mpambanaji mwambie hata Kesho atamke neno “DP-World” uone ….
Yani akisikia hata watu wanatamka anajificha utomsikia anaongelea maana DP-World ni ya moto sana kwake
😂😂😂😂😂
 
Kama kweli mpambanaji mwambie hata Kesho atamke neno “DP-World” uone ….
Yani akisikia hata watu wanatamka anajificha utomsikia anaongelea maana DP-World ni ya moto sana kwake
😂😂😂😂😂
Kwani DP world lina ujinai gani mpaka Rais ashindwe kulitamka? Kwani amelitamka mara ngapi?
 
Back
Top Bottom