Ponda aachiwe mara moja - Lipumba

Ponda aachiwe mara moja - Lipumba

Useme ya huku S/wanga kama huyajui.
Nini chanzo cha kutenguliwa uchaguzi?Chanzo cha hayo kuanza kanisani?Ukipata majibu ya maswali hayo utaacha kuchangia vitu usivyojua.

mkuu nakupa kudos, umempa kubwa yake!!
 
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba ameitaka serikali kumuachilia kwa dhamana Sheikh Ponda Issa Ponda kwani amewekwa ndani kinyume na utaratibu.
Prof Lipumba amedai kusema kwamba Sheikh Ponda alihusika na uchomaji wa makanisa ni uongo na kitendo cha kumkamata ndicho kilichochochea vurugu zilizofanyika wiki iliyopita.Amesema ili kurejesha amani na kunusuru nchi kuingia katika mfarakano ni lazima kwanza kiongozi huyo wa waislam aachiliwe huru.

Source:Mwananchi.

He! Mchumi kawa mwanasheria!! Nasikia Ponda na lipumba ni ndugu
 
Nilitakaa kumwekea dhamana ila sikukidhi masharti ya dhamana ila nadhani kwa mtu kama Prof. Lipumba obvious anakidhi masharti ya dhamana, Prof twende...
 
hapa napata shida kidogo kuelewa kauli ya profesa lipumba kuhusiana na kile serikali imekifanya kwa shehe ponda Najiuliuza ya kuwa kauli hii ni kwa sababu yeye pia ni muislamu au na kama siyo basi kauli hii imeegemea wapi je ni katika haki za raia na mali zao au namna gani Na kama ni haki za binadamu na mali zao je yeye anafurahia uharibifu uliofanywa na hao waislamu kama jibu ni ndiyo basi aeleze moja kwa moja bila kuzunguka watanzania tuweze kufahamu msimamo wake na chama chake kwa ujumla Kwangu mimi ukisema ya kuwa ponda aachiwe huru ina maana ameishahukumu tayari pasipo hata suala la kisheria kuchukua nafasi yake Binafsi namheshimu sana profesa lipumba lakini katika suala hili napata shida kidogo na msimamo wake
 
Sababu ni zipi?CUF ushahidi ni yale ya Arusha mapokezi ya Lipumba kujadiliwa msikitini.
Dr.Slaa ni padre aliasi,hivyo si padre kwa imani ya kikatoliki na wala haruhusiwi hata kufunga ndoa kanisani.

kanisa lipi???
 
Lipumba ni mwanasiasa na kiongozi wa chama halali cha upinzani hivyo ana wajibu wa kumtetea raia yeyote anaekamatwa kinyume cha sheria! baya zaidi ni Serikali kumshikilia mtuhumiwa bila ya kumpa dhamana ambayo ni haki ya mtuhumiwa kwa mujibu wa katiba na utawala wa sheria!

La kushangaza hapa Jamii Forum (the Great thinkers) wanaoshabikia Chadema wanafurahia mtuhumiwa kunyimwa dhamana na ikiwa kiongozi wao Slaa au Mbowe au Lema wakikamatwa na Polisi kwa tuhuma za kuchochea machafuko basi kinachofuata ni laana na kauli za kuleta vita hutoka mdomoni mwa wafuasina wakereketwa wa chadema!

Chadema ni wanafiki kwa sababu wamemtuma Profesa safari kutoa kauli kwa niaba yao badala ya Katibu wao mkuu slaa au Mwenyekiti wao Mbowe! leo Lipumba anapomtetea Ponda aachiliwe kwa dhamana mnamtukana! Jee kama mnatetea Serikali hii ya Jk ikamate raia wake na kuwanyima haki yao ya dhamana, Chadema ikishika Serikali patakalika kweli!

Chadema kama wanataka kupata ridhaa ya wananchi haina budi kujiepusha na kauli za mashabiki na baadhi ya viongozi wao wanaonyesha chuki zao dhidi ya Uislamu

Red: Suala linapofika mahakamani, ni mtu mwenye hadhi ya UWAKILI tu ndio anaweza kumtetea mtu mahakamani, na polisi hawatoi dhamana kwa makosa kama anayoshitakiwa nayo Bw. Ponda, mahakama ndio yenye mamlaka hayo, na kama hatatimiza masharti ya dhamana basi haachiwi! Na sio kila kosa linadhamana. Food for thought, kama Ponda angekuwa anaheshimu katiba na utawala wa sheria, asingefanya hayo yote yaliyosababisha atiwe mbaroni. Na kwasababu Lipumba amezungumzia hilo suala ilihali liko mahakamani, ametenda kosa kisheria, na amevunja katiba kwa kuingilia uhuru wa mahakama kushawishi na kulazimisha Ponda apewe dhamana... Its true u can't judge a book by its cover...cover professor, content, zero brain...
 
Lipumba anaishi dunia gani? Hajui kuwa tunajua kuwa yeye Ponda na Farid na Uangusho lao moja? Go to hell Lipumba na uprofesa wako usiokusaidia hadi unawekwa kinyumba kisiasa na Seif ambaye naye kawekwa rumenya na CCM. Ama kweli waso haya wana mji wao!
 
Mungu saidia Tanzania, watu ambao tunategemea ni wasomi na wenye maono wamekuwa gizani na kutoa kauli kama za wapiga bao mitaani. Hivi huyu angekuwa Rais tungetarajia nini, kwa hiyo watu wakifanya madhambi ya kuharibu amani na nchi na wengine wakaadamana mtuhumiwa anaachiliwa huru. Hii ni hatari na ni hatari kubwa kwa kauli kama hiyo kutolewa na kiongozi tena msomi aliyebobea.

Sasa watanzania tufikirie kwenda kwa mgaga wa kienyeji maana hii hali siyo ya kawaida kauli za viongozi wetu zimekuwa kama ndoto hivi, kwani katika hali ya kwaida ni vigumu kuamini Prof. Anaweza kutoa kauli ya hovyo kiasi hiki. Hii ina maana kuwa yote anayofanya Ponda siyo yeye ila watu kama kina Lipumba.
 
Na yule mwingine ni PADRI sema sasa PADRI mpenda totooz fani zinazomfaa ni za kuongoza KONDOO wa BWANA then awafungishe NDOA halafu aje. Kuiba wake zao kwa hilo ameshinda na PADRI mwenyewe ni huyu hapa chini

Inaonekana ulikuwa unataka kuolewa na unayemuita padri. Umeumizwa sana na kitendo cha kuolewa huyo bibie. Pole bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi tafuta bwana mwingine
 
Nyie Pro-Chadema kwa hiyo mnataka Ponda asiachiwe.
 
Kwan kosa lililomuweka Rumande Ponda ni hilo moja tu?

Au huyu mzee anataka kupotosha na kuchochea kama kawaida ya hawa wenzetu?? Ana ushahid gan Ponda hakuhusika na hilo kosa, alikuwa nae??

Tuna kaz kubwa kuepusha udin nchi hii, maana kama msomi kama huyu ameshndwa kutafakar Je hao wengne wasio na shule huko mtaan watakuwa na mawazo gan??
 
Point of correction: DPP aliwasilisha ombi la kuzuia dhamana ya Ponda siku alipofikishwa mahakamani mara ya kwanza. Bahati mbaya hakimu aliyepangwa kuendesha kesi hakuwepo kutokana na udhuru, hivyo kesi ilipigwa tarehe hadi baada ya wiki2 kama ilivyo taratibu, dhamana itaamuliwa na hakimu siku hiyo.

Prof. Lipumba hayajui hayo?

Amani kwa wote, wakatabahu.
 
Lipumba anaishi dunia gani? Hajui kuwa tunajua kuwa yeye Ponda na Farid na Uangusho lao moja? Go to hell Lipumba na uprofesa wako usiokusaidia hadi unawekwa kinyumba kisiasa na Seif ambaye naye kawekwa rumenya na CCM. Ama kweli waso haya wana mji wao!

Kumbe Lipumba ni pumba za ukweli.To hell na Migamba yao
 
Akafundishe uchumi huko mambo haya awaachie wenye mamlaka yao, na ndo tatizo la wanasiasa wa tanzania ni kurukia mambo ili wajijenge ki siasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom