Ponda aachiwe mara moja - Lipumba

Ponda aachiwe mara moja - Lipumba

Kusema kwamba hahusiki na mashtaka nadhani ni kazi ya mahakama kwa sasa....... nani yuko nyuma ya sheikh Ponda kisiasa?? Kama Profesa anamuunga mkono sheikh Ponda basi atakuwa anafanya makosa makubwa sana...
 
Ukiwa mjinga, hata ujifiche vipi lakini ujinga wako utajitokeza tu!
Ndo haya sasa kwa profesa Lipumba anatoa maoni kama profesa wa ze komedi!
 
Chadema hawakutoa judgement kuwa ponda anahusika ama hawakuhusika ktk uchomaji,iweje lipumba na kauli yake...anataka kudumisha udini as usual,poor Mtemi Pumba

alafu kuna watu humu wanaona cdm ndio chama cha kidini na cuf ndo chama safi...yeye amejuaje kua ponda hakuhusika kwenye uchomaji makanisa..amekua mahakama? ana ushahidi wowote kua hakushiriki...anamtetea kwa sababu ni sheikh sio..ingekua askofu ndio yuko mahakamani angetoa hiyo kauli? chama cha cuf uchaguzi ujao unatakiwa usipewe kura hata moja yaani wasipate mbunge hata mmoja watanganyika amkeni hakikisheni 2015 hakuna mbunge hata mmoja kutoka cuf hiki chama tuhakikishe kinakufa kabisa...hawa ndio wachochezi na wanaovuruga amani tuliyoshaizoea katika nchi hii
 
Wewe ni Profesa wa uchumi, hayo ya ponda ni fani nyingine ambayo unadandia bila kuijua

Lipumba hajawahi kuwa presidential material by any known standard.
Pia kwa matamshi na vitendo vyake mara nyingi amejionyesha kuwa si mtu makini kwa kiwango cha elimu (Prof) alichonacho....hii kauli ni mfano wa nyongeza tu.

Sisemi ni mdini, ila ningemshauri kama angejaribu kugombea ubunge au nafasi ya chini (ambayo realisticly atachaguliwa).
 
Sijui tatizo lenu liko wapi? Lipumba amesema/dai kuwa raia Ponda amewekwa ndani kinyume na sheria, na makosa anayotuhumiwa nayo yanastahili dhamana!
Lengo lake ni kuepusha vurugu zaidi kwani inawezekana si pekee aliye baini hitilafu kwa jinsi suala zima la ponda linavyokwenda huenda wafuasi wake pia wakahisi uonevu na hii itavuruga jamii!
Mi si muunini wa vurugu lakini sheria lazima ifuatwe no matter what~

Acha uoga waislam ni wastaarabu hawatavunja amani kamwe acha ponda apumzike kidogo huko selo atapata pepo.
 
Huyu nae sasa anaelekea kubaya hakika,unamshabikia mtu kama Ponda unaonekana kama kituko.
 
Ni kweli gazeti la dini yao lilimtangaza Ponda atachuana na Mnyika uchaguzi ujao Ubungo.Eti wakadai Ubungo ina Waislam wengi kuliko wakristo kwa hiyo ni lazima Ponda ambwage Mnyika

Ni waislamu wahuni na majambazi ndio watampigia kura huyu gaidi, waislamu wanafahamu maana ya dini ya hawawezi kufanya upuuzi huo.
 
VIPI NA HAWA CHADEMA WENZENU MNAWACHUKULIAJE?KILA WAKATI NASISITIZA TUWE FAIR TUACHE CHEAP POLITICS,IT'S NAT GONNA HELP EITHER...ALICHOSEMA LIPUMBA KINA TOFAUTI GANI NA WALICHOSEMA HAWA MAKAMANDA WENU UCHWARA.?

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekutana na waandisihi wa habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam leo, ambapo wajumbe wa Kamati Kuu, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando, wameweka waziwazi msimamo wa chama hicho kuhusiana na mgogoro kati ya waislamu na serikali na kukamatwa kwa Sheikh Farid huko Zanzibar.

Wanasheria hao wa CHADEMA wamesema kuwa kitendo cha serikali kumnyima dhamana Sheikh Ponda ni kinyume cha katiba na kwamba Chadema kama chama kinachojiandaa kuchukua dola, hakiwezi kuvumilia kuona haki za raia zikivunjwa.

“Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini,” ameeleza Marando katika mkutano huo.

Marando alifika mbali zaidi kwa kusema tatizo lililopo sasa kati ya serikali na waislamu, limetokana na hatua ya serikali kuwalazimisha waislamu wote kuwa waumini wa Bakwata, chombo ambacho wengi wanakiona kinatumika kuwakandamiza.

Naye Profesa Safari alionya matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotumiwa na serikali kwa kisingizio cha kulinda amani, huku akieleza kuwa matumizi ya kijeshi siyo suluhu ya kutatua matatizo yaliopo.

Kuhusu kukamatwa kwa Sheikh Faridi na kumzuia kwa siku tatu, wanasheria hao wamesisitiza kuwa kitendo hicho hakikubaliki.

“Kitendo cha kumkamata na kumshikiria Sheikh Faridi, huku serikali na vyombo vyake vikisema havihusiki, wakati ukweli ni kuwa alikuwa anashikiliwa na watu wa USALAMA wa TAIFA, ni uharamia mkubwa unaopaswa kulaaniwa na wote wanaolitakia mema taifa hili,” ameeleza Marando.

Kuhusu uvunjwaji wa makanisa, Profesa Safari amesema CHADEMA kimelaani hatua hiyo iliyotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi. Amewataka waislamu kuvuta subira.

Hata hivyo, Profesa Safari amesena matatizo yanayotokea sasa, yameletwa na CCM kutokana na hatua yao ya kuwatumia baadhi ya waislamu kupandikiza mbegu ya udini nchini.
 
VIPI NA HAWA CHADEMA WENZENU MNAWACHUKULIAJE?KILA WAKATI NASISITIZA TUWE FAIR TUACHE CHEAP POLITICS,IT'S NAT GONNA HELP EITHER...ALICHOSEMA LIPUMBA KINA TOFAUTI GANI NA WALICHOSEMA HAWA MAKAMANDA WENU UCHWARA.?

...

"Tunaweza kuwa miongoni mwetu, wapo watu wanaomchukia Sheikh Ponda, lakini hatuwezi kuficha ukweli kwamba Sheikh Ponda kama raia wa Jamhuri ya Muungano au mkazi wa Jamhuri hii, anayo haki ya kusikilizwa na kupewa dhamana. Makosa ambayo Sheikh Ponda ameshitakiwa yanadhaminika kwa mujibu wa sheria, hivyo ni makosa kwa serikali kufanya hila kumnyima dhamana kiongozi huyu wa kidini," ameeleza Marando katika mkutano huo.

...



Mkuu acha unafiki. Hivi kweli huoni tofauti kati ya tamko la Chadema na la Prof. Lipumba? Hebu linganisha red katika tamko la Chadema hapo juu na green ya Lipumba hapo chini. Hapo nilipo-underline, tayari Lipumba analo jibu au hukumu! Eti ni uongo; hiyo ni kazi ya mahakama. Tofauti ya matamko hayo mawili iko very clear; lilioenda shule na la kipumbavu yanajieleza yenyewe.



Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba ameitaka serikali kumuachilia kwa dhamana Sheikh Ponda Issa Ponda kwani amewekwa ndani kinyume na utaratibu.
Prof Lipumba amedai kusema kwamba Sheikh Ponda alihusika na uchomaji wa makanisa ni uongo na kitendo cha kumkamata ndicho kilichochochea vurugu zilizofanyika wiki iliyopita. Amesema ili kurejesha amani na kunusuru nchi kuingia katika mfarakano ni lazima kwanza kiongozi huyo wa waislam aachiliwe huru.

Source:Mwananchi.
 
Coming 2015... kwa kuwa udini umetutawala sanaa SISI WAPUMBAVU WAJINGA TUNAO ONGOZWA na GENGE LA WEZI... nashauri CDM wamsimamishe Padri, CUF wamsimamishe Sheikh na CCM wamsimamishe JAMBAZI lolote kama kawa ... Liwalo na liwe!!!
 
Coming 2015... kwa kuwa udini umetutawala sanaa SISI WAPUMBAVU WAJINGA TUNAO ONGOZWA na GENGE LA WEZI... nashauri CDM wamsimamishe Padri, CUF wamsimamishe Sheikh na CCM wamsimamishe JAMBAZI lolote kama kawa ... Liwalo na liwe!!!

Hapo kwenye red; the obvious need no proof! Ndivyo ilivyo na itakavyokuwa.
 
Hapo kwenye red; the obvious need no proof! Ndivyo ilivyo na itakavyokuwa.

Pro CDM wengi hususan humu ndani huwa wanaiharibia sana CDM kwa kuonyesha hisia zao za kidini hata katika vitu ambavyo viko wazi kabisa...ACHENI UDINI ndugu zangu, tunakazi kubwa sana ya kuikomboa nchi hii angalau vitukuu vyetu vije vikute angalau magadi soda!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom