By
Mkandara
Mkuu wangu wewe umeambiwa vipi kuhusu uchomaji moto wa makanisa Mbagala?.. Unaona sasa jinsi mlivyokuwa misinformed na vyombo vya habari kiasi kwamba hamtaki hata kuujua ukweli?..
1. Waliochoma makanisa ya Mbagala ni wahuni wa Mbagala ambao wanasakwa na wanaendelea kukamatwa. Hatujui hadi leo wamekamatwa wangapi na kesi yao hatujui itakuwa lini na kina nani viongozi wao na wanahusika. Na pengine ndio limetoka - Upepo wa kupita hili muulize Kova vizuri..
2. Swala la Ponda linahusiana na kesi ya kiwanja kilichopo Chang'ombe ambacho waislaam walienda kule kusali Ijumaa ile ile ya siku ya machafuko ya Mbagala. Inasemekana waliiba hadi vifaa vya ujenzi vya mwenye kiwanja. Watu 50 walikamatwa na kingozi wao ndiye alikuwa Ponda, hivyo Sheikh Ponda alitafutwa na kukamatwa kutokana na kesi ya Chang'ombe pamoja na swala la kuhamasisha waislaam wasipige kura ikaitwa kuvuruga amani. Ponda hahusiki na Mbagala na nimesema sana humu lakini hamtaki kuelewa kwa sababu tayari mmeisha weka maamuzi yenu juu ya
Ponda ambaye wala sii kiongozi wa Waislaam bali ni mwalimu wa dini. Last edited by Mkandara; 24th October 2012 at 17:52.