Emmanuel Ng'wiza
Member
- Mar 9, 2013
- 5
- 1
Kwa miaka mingi, kampeni nyingi za afya zimekuwa zikitumia jumbe mbalimbali: "Acha pombe, ni mbaya kwa afya yako." Hata hivyo, wataalamu wa afya ya jamii sasa wanakubaliana kuwa ujumbe huu pekee hautoshi. Watu wengi sasa tayari wanajua athari za pombe, lakini bado wanakunywa. Tunaona siri ya mabadiliko ya kweli haipo kwenye vitisho, bali kwenye kuelewa jinsi pombe inavyofanya kazi mwilini na jinsi tunavyoweza kubadili mifumo yetu ya maisha.
Kama wasomaji wa makala hii, ni wakati wa kuangalia suala hili kwa mtazamo mpya na jicho la kiuchambuzi.
Nini hutokea ndani ya mwili anapokunywa pombe? Badala ya onyo la jumla, ni muhimu kujua ukweli wa kibiolojia kwa mtu binafsi. Pombe ina kemikali inayoitwa ethanol. Kemikali hii inajulikana kisayansi kama kichocheo cha saratani (carcinogen) ambacho huharibu mfumo wa vinasaba (DNA) vya binadamu. Tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kuwa unywaji wa pombe huongeza hatari ya kupata angalau aina saba za saratani, ikiwemo ya mfumo wa chakula, ini, na matiti, na inawezekana wengi hawajui. Mtu anapojua angalau sayansi hii, unakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi badala ya kufuata mkumbo.
Kwa sasa kuna mbinu kadhaa za kiusalama zinazoweza kupunguza madhara makubwa mwilini na kijamii ambazo ni:
Ili kuwasaidia vijana kujiepusha na matumizi ya vileo, haitoshi tu kuwakataza. Sote tunapaswa kutengeneza mazingira Rafiki pamoja na nafasi za malezi, kuwekeza kwenye michezo, na sanaa ambazo zitawapa burudani na faraja bila kuhitaji kileo. Kubadili mtindo wa maisha si jepesi na halitokei kwa usiku mmoja, bali huanza kwa kupata uelewa sahihi na kuchukua hatua ndogo ndogo kuelekea maisha yenye afya na usalama zaidi.
Mwandishi: Emmanuel Jacob, Afisa Mfiziotherapia, Mwenyekiti wa Tanzania Physiotherapy Initiative

- Kushushia na Maji: Kunywa glasi moja ya maji baada ya kila glasi ya pombe ili kuzuia mwili kukauka maji (dehydration).
- Kujipangia Kipimo: Kuwa na kikomo cha idadi ya vinywaji kabla ya kuanza, na kwenda polepole.
- Ulinzi Barabarani: Kuwa na dereva asiyekunywa (designated driver) au kutumia usafiri wa umma ili kuzuia ajali.