Politics is a game of dynamics, Urais, Ubunge, Udiwani turufu ni CCM na TLP Tu, Siasa za Itikadi Tanzania hazipo tena! kikubwa mkono uende kinywani tu

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,545
2,175
Wanasiasa hasa Wa Upinzani naomba mpitie huu Uzi kwa makini sana,

MADA :"Politics is a game of dynamics,Urais,Ubunge,Udiwani turufu ni CCM na TLP Tu,Siasa za Itikadi Tanzania hazipo tena! kikubwa mkono uende kinywani tu"

Jana nimefuatalia kwa kina Mkutano Mkuu Maalum Wa CCM uliofabyika Jijini Dodoma,

Massa 24 baada ya mkutano mkuu ule Naomba kuutangazia Umma kupitia Jukwaa hili mambo yafuatayo;-

1. Tangu CCM iingie madarakani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuwa "CCM MOJA" na ushahidi ni kura 1,822 sawa na 100% alizopata Dk John Magufuli mgombea toka CCM, kumbukeni kinachowadhoofisha CCM wakati wakati wote ni disunity tu hili wamelishinda mwaka huu,

2. Upinzani wasipokuwa makini hawataambulia hata Kata moja hasa CHADEMA na ACT-Wazalendo kwani agenda zao za kumsema vibaya Rais Magufuli ni kama zimekataliwa na Umma hivyo lazima waje na Agenda mpya zenye mashiko na wasimguse kabisa Rais Magufuli kwenye majukwaa yao,

3. Chama cha Mrema kinaonekana kumfurahisha sana Rais Magufuli hasa kwa Sera yake ya Kumtangaza yeye kuwa ndie Mgombea watakao mnadi nchi nzima hivyo huenda TLP ikafanywa Chama Kikuu Cha Upinzani ili kutafsiri uwepo Wa demokrasia ya vyama vingi nchini, Nyie mnaotaka kuwa wabunge na madiwani Wa kupiga makofi ovyo bungeni gombeeni kupitia CCM au TLP mtapita,

4. Wapinzani wasipoungana na kuweka Rais mmoja jumla ya kura zao haziwezi kufika 5% ya kura zote zitakazopigwa ili wafanikiwe zaidi asimame Mhe Bernard Kamilius Membe vinginevyo watapoteana tarehe 25/10/2020 saa 2 Usiku,

5. Rais Magufuli anakuwa Rais Wa Kwanza Tanzania kushinda kwa zaidi ya 90% huu ni Ukweli mchungu kwa wanasiasa hasa Wa Upinzani ila lazima litatokea tu dalili zote zinaonesha, Nashauri Jipangeni kwa 2025,

Ni Jabali la Siasa za Nchi,

Kwa sasa safarini kuelekea Dodoma,
 
Hata Mimi Jana nimeona namna Rais Magufuli alivyomfurahia mzalendo mwenzake Mrema,

Pamoja na matusi mengi anayotukanwa mzee kwenye kumuunga mkono Rais Magufuli nakubaliana naye kwa 90%

Magufuli hakutakiwa kuwa na Mpinzani kwenye uchaguzi huu mkuu ujao,
 
Wewe bado sana kwa uchambuzi wako huu, yaani una define umma wa Tanzania kwa kuangalia wajumbe wa ule mkutano wa CCM wa jana uliompitisha Magufuli kwa 100%

Nakuhakikishia hiyo imani ya uongo uliyonayo hata huyo mwenyekiti wako unaemsifia hapa hana, anajua hali yake ni mbaya huku uraiani zaidi ya maelezo.
 
Ukweli unatabia ya kusimama tu hata kama itakuwa muda gani RAIS MAGUFULI anatisha wazee lazima tukubali tu,

mimi ni Mpinzani Ila Naunga mkono Magufuli
 
Hujamuelewa mtoa mada. Mgombea wa Ccm kapitishwa kwa 100% na hii inaonyesha unity ndani ya Ccm. Acha kukurupuka.
Wewe bado sana kwa uchambuzi wako huu, yaani una define umma wa Tanzania kwa kuangalia wajumbe wa ule mkutano wa CCM wa jana uliompitisha Magufuli kwa 100%

Nakuhakikishia hiyo imani ya uongo uliyonayo hata huyo mwenyekiti wako unaemsifia hapa hana, anajua hali yake ni mbaya huku uraiani zaidi ya maelezo.
 
Siasa Tanzania kwa sasa zinalipa sana,Kule Rorya kunawagombea 60 ili wafike tu Bungeni,

Upinzani tujipange Upya hili game sio letu,
 
Kabisa hakuna tena itikadi ni ili mradi mtu ashibe basi. Jiwe ameharibu sana nchi yetu na kwabahati mbaya watu hawaelewi.
 
Kuna Chama sera yake ni kumtangaza Magufuli?
Halafu kwa uharo huo bado unajiita jabali la siasa!!!?
 
Siasa za mwaka huu hazieleweki kabisa, Unaweza jikuta kweli TLP kinakuwa chama kikuu cha Upinzani na Mwana CCM aliyepandikizwa TLP anakuwa kiongozi Wa kambi rasmi ya Upinzani
 
Siasa za mwaka huu hazieleweki kabisa,Unaweza jikuta kweli TLP kinakuwa chama kikuu cha Upinzani na Mwana CCM aliyepandikizwa TLP anakuwa kiongozi Wa kambi rasmi ya Upinzani,
mawazo ya kusadikika mkuu TLP? hahahahaha yaani mawazo ya babu mrema ndo yatushawishi wenye akili timamu
 
Back
Top Bottom