KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,601
Kuna baadhi ya mambo ukiyaangalia juujuu bila kufungua mlango wa sita wa fahamu kuyafahamu zaidi, unaweza kuhisi ndivyo yalivyo.
Moja ya mambo hayo ni siasa zetu huku mitandaoni na mitaani. Kwa mara ya kwanza kama hujawahi kabisa kufuatilia siasa na ukaanza kuzifuatilia mitandaoni, utagundua yafuatayo:
Kwanza, utagundua CCM ndio chama Cha upinzani na Upinzani ndio umeshika Dola lakini katika uhalisia mitaani kuna watu hawamfahamu hata kiongozi wa chama kikuu cha upinzani lakini wanawafahamu viongozi wa chini wa CCM.
Pili, utagundua CCM kimejifia zamani na limebaki jina tu lakini katika uhalisia mitaani ni upinzani uliojifia limebaki jina tu.
Tatu, unaweza kuhisi CCM hakuna demokrasia lakini katika uhalisia mitaani demokrasia ya CCM inaaminiwa mno.
Nne, unaweza kuhisi upinzani una sera nzuri na wangekuwa wao madarakani sera zao zingetupeleka nchi ya ahadi lakini katika uhalisia mitaani wengi wanaziona sera za upinzani ni za kilaghai na wengi wanajiuliza kama ubunge na udiwani walishindwa ,vipi kwingine?
Tano, unaweza kuhisi yanayosemwa juu ya nchi kuuzwa ni kweli lakini katika uhalisia mitaani watu wanauliza kama nchi imeuzwa na wanaosema imeuzwa wapo humuhumu na Kila siku wananunua ardhi ,je wananunuaje kitu ambacho kimeuzwa? Je, na wenyewe wameuzwa pamoja na nchi?
Six, unaweza kuhisi Mbowe ni Rais, Lissu ni Makamu wa Rais na wengine ndio wameshika madaraka lakini mtaani wanaowafahamu Mbowe na Lissu ni wakina nani hasa ,ni wale waliobahatika kuwafahamu mitandaoni.
Hayo ndio machache katika mengi, utakayokutana nayo mitandaoni lakini ukweli ni kwamba:
Mitandaoni kuna mtu anakuwa na ID hata 10, ID moja ikitumika kuandika mada ID 9 zilizobaki zitatumika ku-comment na ku-like na kikundi cha watu 50 mitandaoni kinaweza kuchafua hali ya hewa maana zitaonekana comments 500.
Mitandaoni wengi ni watoto na siasa zinafanywa na watoto ambao wengi wao hawajatimiza hata umri wa kupiga kura lakini siasa za mtaani ni ngumu kufanywa na watoto.
Kuna mifano kadhaa juu ya ukweli wa hoja yangu. Kuna baadhi ya matukio yaliratibiwa mitandaoni lakini yakashindwa kukamilishwa kwenye uhalisia Kwa sababu zilizosemwa hapo juu.
Wito, siasa za mitaani sio suala jepesi hata kidogo na ndio kipimo cha uimara wa chama cha siasa, vyama visijifiche nyuma ya mitandao.
Ndio maana naendelea kuamini kwamba sio leo wala kesho CCM kutolewa madarakani kwa sababu CCM hakihitaji kuungwa mkono na maroboti. Nasema maroboti kwa sababu AI itafanya kazi za watu halisi.
CCM kina hitaji kumfikia Kila mtu na kueneza sera zake. Inatumia mitandao kama kiwezeshi cha kufikia watu na sio mbadala.