Polisi yapiga marufuku maandamano ya kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam, Jumatatu Juni 19, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,992
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawatahadharisha wananchi kuhusu taarifa zinazozagaa kutoka kwa mtu mmoja kuwa kutakuwa na maandamano siku ya Jumatatu Juni 19, 2023 kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.

Taarifa hiyo anayodai kuwa aliifikisha Polisi, tayari amejibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano aliyokuwa anataka kuyaratibu na kushauriwa kama ana jambo la msingi atumie vyombo mbalimbali vya kisheria anavyoweza kufika na kuwasilisha hoja zake bila maandamano ili haki zingine za wananchi za kufanya kazi wakiwa huru zisiingiliwe.

Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu kutoshiriki hicho kinachodaiwa maandamano na badala yake mnahimizwa kuendelea na shughuli zenu za kiuchumi na kijamii bila hofu. Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu au kundi la watu linalotaka kuzusha taharuki kwa kuzuia watu wengine kufanya kazi zao.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa 10 wanaodaiwa kuhujumu kwa kuiba miundombinu ya vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu. Watuhumiwa hao wamekanatwa kufuatia opeshereni maalum kali iliyoanza tarehe Juni 5, 2023 na inaendelea katika Jiji la Dar es Salaaam na mikoa ya jirani.

Waliokamatwa ni pamoja na Husein Ally @ Kijingo (32) Mkazi wa Mbande Kisewe akiwa na wenzake 7 ambao wamekuwa wakiiba betri muhimu na vifaa mbalimbali vya minara ya mawasiliano ya simu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na mikoa jirani.

Jeshi la polisi limekamata pia Simon Mangu (33) mkazi wa Ubungo na mwenzake mmoja baada ya kukutwa na vifaa vya minara ya masawailiano ya simu vya wizi vinavyoibwa na kuvificha maeneo ya Mbezi Luis.

Jeshi la polisi katika Operesheni hiyo limekamata jumla ya betri 68 zenye thamani ya Tsh 163,200,000 na vifaa mbambali vya minara ya mawasiliano ya simu vilivyoibwa magari mawili

(2) yanayotumiwa na wezi hao kubebea vifaa hivyo yamekamatwa ambayo ni Toyota Hilux T.850 BDR, Toyota Carina T.112 BRN na pikipiki MC.901 DJQ, pia vifaa mbalimbali vya kuvujia vimekamatwa. Watuhumiwa wote watapelekwa mahakamani haraka iwezekavyo.
 
Mkuu kwahiyo ile Taarifa yangu kwamba kulikuwa na maandamano ambayo ilifutwa kumbe ilikuwa kweli ! basi sawa

Nadhani tulichotakiwa kufanya ni kuweka taarifa zote mbili , ile ya Maandamano yanakopita na hili kanusho la Polisi ili wadau wajue kwamba hili jambo lilikuwepo , haikuwa haki kuiondoa Taarifa ya maandamano na kulibakisha kanusho la Polisi , ikiwa kama habari ya maandamano haikuwa kweli Polisi wanakanusha nini ?
 
Jeshi la Polisi kwanini mmezuia? Ni haki ya wanaoandamana kama ilivyohaki ya wanaondamana kupongeza juhudi za serikali. Kwanini hawa mnawaruhusu?
Kwani familia zenu zipo Uarabuni au Zimbabwe?

Mkataba ule utatuliza wote mimi na nyingi na Watanzania wote wakati Rais Samia atakuwa kastaafu na kazeeka. Hivi mpangaji anaweza kumpa masharti mpangishaji (mwenye nyumba) kiasi kile? Pengine nanyi mmeona mapungufu lakini mnaogopa kulinda tu nafasi twenu. Huo ni uoga.

Watoto wenu, wajukuu wenu na vizazi vyenu vitakuta Tanzania ya hali gani? Kwa masharti yale tuna mashaka na DP kama ni wawekezaji wenye nia nzuri, hivyo waachieni Watanzania wafikishe ujumbe kwa wahusika.

Tambueni kwamba ni sisi tuliwachagua na kuwapa mamlaka hayo. Tusipowaelewa tuna haki ya kuwapinga hadharani kwa mstakabali wa nchi yetu. Wakishupaza shingo leo, uchaguzi unakuja watatupigia magoti na kutubembeleza nasi tutawakataa kwenye sanduku la kura.

Chonde chonde Afande IGP na wasaidizi wako waacheni Watanzania wenye sauti wawa wakilishe wasio na sauti. Mkiwazuia wenye nchi yao kuitetea, Mwenyezi atawauliza siku za mwisho wa uhai wenu.

Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿
 
Nimepita youtube nimemsikiliza police ametoa maelekezo watu wasiandamane kwenda mahali patakatifu Ikulu ya Tanganyika

Watanganyika muheshimuni huyu office wa polisi msiende ikulu

Nendeni mkaandamane zilipo balozi za wale watu wanaovizia kununua nchi yenu!

Mkaandamane pale msitoke

Mmekatazwa ikulu sawa nendeni kwenye ubalozi wao ikiwezekana muwatoe nje
 
Mtu huyo mmoja kuratibu maandamano ana nguvu kama ya Mange Kimbambi? Au alitaka tu atajwe katika taarifa apate umaarufu,si angekula hata kinyesi chake hadharani apate umaarufu.
Nani kamdanganya kuwa kipindi hiki ni cha kuungwa mkono katika maandamano na maisha yenyewe magumu hivi,labda kama atanunua waandamanaji
 
Back
Top Bottom