Polisi Wilayani Rombo mnachafua Utawala wa Rais Magufuli

kamojatu

JF-Expert Member
Dec 6, 2013
723
681
Wakati Mheshimiwa Rais Magufuli akipigania maendeleo na kufanikiwa kuiingiza Tanzania kwenye uchumi wa kati kabla ya muda uliokuwa ukitarajiwa, jeshi la polisi wilayani Rombo limeendelea kulea na kushirikiana na wezi, wauza gongo, wauza bangi na wakabaji hali iliyosababisha wananchi wa vijiji vya Keni, Manda, Mengwe na Mamsera kuishi kwa hofu na kushindwa kujishughulisha na shughuli za maendeleo

Kutokana na ushirikiano wa karibu uliopo kati ya wauza madawa ya kulevya, majambazi na polisi wa kituo cha Mengwe wananchi wamekuwa hawapeleki ripoti za matukio kituoni hapo kwa kuhofia kulipizwa kisasi na vikundi vya uhalifu vinavyopata taarifa toka polisi wa kituo cha Mengwe

Kwa mfano wiki iliyopita wakala wa Mpesa kwenye soko la Kilesi lililopo kijiji cha Keni alivamiwa na majambazi yenye silaha saa 12 jioni na kupiga risasi hewani na kupora tena umbali wa kilomita 1 kutoka kituo cha polisi Mengwe lakini hakuna msaada uliopatikana.

Wananchi wa Kijiji cha Manda wanajifungia majumbani ifikapo saa 12 jioni kisa uhalifu.

Tunaomba serikali itupie jicho utendaji wa polisi wilayani Rombo hususani kituo cha polisi Mengwe ambacho kimekuwa kituo cha ujambazi badala ya kituo cha polisi.

Wananchi wengi wameumizwa kwa kukatwa mapanga na kuporwa mali zao lakini hawapati msaada wa polisi.

Polisi wa kituo cha Mengwe wamekuwa wakivuruga kesi kwa makusudi hali inayosababisha wahalifu kushinda kesi ambazo walistahili kushindwa, hivyo kuongeza hofu miongoni mwa wananchi.

Polisi wilayani Rombo wanafanya kazi kana kwamba sio sehemu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Rais Magufuli.

Tunaomba tafadhali serikali yetu sikivu ichukue hatua za haraka ili kuwanusuru wananchi wasio na hatia dhidi ya uhalifu uliokithiri.
 
Rombo uhalifu upo sana aisee..kuna Jamaa yangu alikuwa na ishu yake huko nikamsindikiza na usiku wakati wa kurudi tukakuta duka la jumla limevunjwa ,majambazi walivunja ukuta na ilikuwa ni mapema tu,,na kituo cha polisi mengwe kipo dakika mbili tu kutoka duka lilipo kama wanatumia pikipiki
 
Rombo utafikiri sio jamhuri ya Tanzania. Watu wana viwanda vya gongo majumbani. Polisi wamafika kuchukua ruzuku
 
Ujambazi ndio usiseme. Wananchi wanajifungia majumbani ikifika saa 12 jioni
 
Jishughulisheni na hao polisi uchwara kama watu wa Kibosho wanavyofanya; mnamalizana nao mmoja mmoja hadi wanakwisha. Watakuwa na adabu. Msisubiri serikali hii wameshiba sifa.
 
Cha ajabu OCD anazo taarifa lakini anafanya siasa. Anafanya mikutano ya hadhara na wananchi na kutoa namba za simu badala ya kukamata wahalifu na kufukuza askari wezi wa kituo cha Mengwe.
 
Rombo ni nyumbani ila nakereka na ujambazi mkubwa uliokithiri! Yani majambazi wanaweza kuvamia mchana kabisa jua likiwaka na wanaweza kuiba hata zaidi ya duka moja na wasipate changamoto yoyote
Silaha za moto sijui wanatoa wapi maana ni karibia kila mwezi kuna tukio au matukio
 
Rombo ni nyumbani ila nakereka na ujambazi mkubwa uliokithiri! Yani majambazi wanaweza kuvamia mchana kabisa jua likiwaka na wanaweza kuiba hata zaidi ya duka moja na wasipate changamoto yoyote
Silaha za moto sijui wanatoa wapi maana ni karibia kila mwezi kuna tukio au matukio
Tatizo ni polisi wanashirikiana nao. Huwezi kuamini ni Tanzania ya Magufuli. Ukiwa Rombo unaishi kama uko Sudan Kusini. Ikifika sa 12 unawahi nyumbani.
 
RPC Kilimanjaro tupia jicho wilayani Rombo. Polisi wako wanakuharibia kazi.
 
Kwakwel rombo kumezd wiz na gongo
Inapikwa nyumban kabsa kwawatu na police hawajali wao n kufka jion kuchukua rushwa na kwenda

Hasa pale usser kituo cha police station usser yani wamegeuza bishara
Mkuu wa kituo katibu tarafa
Maaskar wote. N ktu kimoja
Inaskitisha sana
 
Polisi wa rombo kuna kipindi walibadilishwa kama wote ila hawa waliokuja ndo wanaongoza kwa kupokea rushwa kutoka kwa wapika pombe haramu na kuua kesi za maskini
Yan n kama hua wanaambizana. Wakitoka
 
Back
Top Bottom